Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
JUHUDI ZA MBUNGE WA JIMBO LA SINGIDA MASHARIKI MHE. MIRAJI MTATURU ZAFANIKISHA UJENZI WA CHUO CHA VETA CHA KISASA CHA BILIONI 2.4 IKUNGI.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu mnamo tarehe 22 Februari 2023 amefanya ziara yake ya Kukagua Mradi wa ujenzi wa Chuo cha VETA cha Ikungi. Juhudi za Mbunge Mhe. Mtaturu zimefanikisha Ujenzi wa Chuo cha VETA cha Ikungi, Ujenzi wa Chuo hicho cha kisasa kimefikia 97% ili kukamilika.
Aidha, katika ziara hiyo, Mhe. Mtaturu amenukuliwa akisema; "Namshukuru sana Rais wa Awamu ya Sita Mama yetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Kufuatia kutupatia fedha za ujenzi wa Chuo, Fedha za Kitanzani Bilioni 2.4. Chuo hiki ni Muhimu sana kwa ajili ya Vijana wetu"
Mhe. Mtaturu amesema; "Nimekuwa nikikisemea Bungeni Chuo hiki na nimekuwa nikiuliza maswali Mengi kujua ni lini Chuo chetu kitaanza kazi na nimeambiwa kuanzia mwezi Machi 2023. Hata sasa kwa hatua kilichofikia Kinatupa matumaini makubwa sana wanaikungi na Watanzania kwa Ujumla"
Sambamba na hayo Akitoa taarifa afisa wa VETA Ndugu Chimala Lehemo ameeleza hatua ya sasa wanakamilisha mambo madogo yaliyobakia ikiwemo uwekaji wa Vigae na Vitanda, Mifumo ya Maji Safi, Maji Taka na Umeme ili masomo yaanze kwa vijana kupata mafunzo ya ujuzi.
Chuo hicho kinaenda kuwa Mkombozi na majawabu kwa vijana wa Ikungi na watanzania kwa Ujumla na kikikamilika kitakuwa kinatoa fani (Course) nane (8).
#KaziIendelee
#IkungiYaMtaturu