Juice ya kabichi

mikumiyetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2016
Posts
1,312
Reaction score
944
Habari za asubuh nimejaribu kutengeneza juice ya kabichi kwa ajili ya vidonda vya tumbo,sasa baada ya kusaga naona ni nzito niongeze maji au nakunywa ivyo ivyo,msaada tafadhali
 
Habari za asubuh nimejaribu kutengeneza juice ya kabichi kwa ajili ya vidonda vya tumbo,sasa baada ya kusaga naona ni nzito niongeze maji au nakunywa ivyo ivyo,msaada tafadhali View attachment 827423
Hivo vidonda vya tumbo umepima H.Pyroli test(Kipimo cha damu) au umefanya Fecal Antigen test(kipimo cha choo) ndo wakakwambia una vidonda vya tumbo?
Au je ulifanya OGD(kipimo cha camera unayoingiziwa mdomoni)?

Kama ni kwa njia hizo mbili za mwanzo na zilikua positive mbona ni rahisi sana kuvitibu hivo vidonda.

Kwa nini mnahangaika mpaka kunywa juice ambazo hazi exist?

Hivi unajua Vidonda vya tumbo asilimia kubwa vinaletwa na Bacteria anaitwa H.Pyroli?

Na unajua hilo kabichi lako linamwagiliwa na maji ya mto msimbazi kama wewe ni mkazi wa Dar?
Na hata kama halimwagili na maji hayo maji mengi yanakua na Bacteria wa hivo na tafiti kibao zishafanyika zinasisitiza watu wasitumie matunda au Mboga hizi bila kuzichemsha.

Nachokiona hapo unaendelea kula H.Pyroli kwa kunywa juice ya tunda usilojua limetoka wapi na unaendelea kujiumiza kwa jina la kutuliza vidonda vya tumbo.

Kwa nini watanzania hatupendi kutumia tiba za hospitali?

Au labda Mh. Ummy Mwalimu itabidi aanze kuweka watalaamu walau madaktari wenye degree hata ngazi za chini za vituo vya afya ili kiwasaidia watu kama hawa ambao labda hana access na hospitali kubwa.

Asilimia kubwa ya Vidonda vya tumbo vinavyoletwa na H.Pyroli vinatibika vizuri sana... sababu huyo bacteria ukishamuua umemaliza kazi.

Nakushauri nenda hospitali achana na kujitesa bora umeze dawa week mbili kumjua huyo mdudu.

Na usipoenda hospitali kuna mda utakua inaenda Pharmacy unanua dawa ambazo zinazidisha vidonda vya tumbo....kuna dawa za kuepuka na kuna vitu vya kuepuka ukiwa na vidonda vya tumbo...Hii elimu hautoipata usipoenda hospitali utaishia kuishi kwa Umbea wa mtaani usokua na evidence kisayansi.
 
Dooo mtakuja kula vitu vya ajabu sana nyie mjue!!
 

Kwasababu tumekata tamaa nazo. hakuna matibabu kitu hapa kwetu.
 
Kwasababu tumekata tamaa nazo. hakuna matibabu kitu hapa kwetu.

sasa ndo unywe juice ya kabichi!

Mtakuja kuambiwa mle na nyaa zenu mtakula!

Watanzania lazima mjue pia level za kuomba intervention unataka uende kutibiwa vidonda vya tumbo katika dispensary?
Vidonda vya tumbo inabidi uende hospitali walau yenye ngazi ya kuitwa hospitali ya wilaya!

Usipojua kwamba kila ngazi ya health facility inaugonjwa wake utaishia kusema hakuna tiba!
 
Mkuu nilipima kwa njia ya choo nikaambiwa na vidonda vya tumbo nimetumia dawa nyingi za hospital lakin hamna unafuu tumbo linawaka moto hadi mgongoni juzi juzi tu hapa nikaenda pima kipimo hicho cha H.pyroli nikaambiwa sina huyo bacteria,naomba msaada wa ushauri zaidi mkuu nateseka sana
 
Kwenye hiyo fomu yako hakuna majibu.

Kuna dawa unatumia za mda mrefu hapa na target zile za maumivu?
Unaweza kuonesha au kutaja baadhi ya hizo dawa ulizotumia mpaka sasa?

Kuna vidonda ambavyo haviko associated na H.Pyroli(ambavyo ndo asilimia kubwa)
Yaani kuna vile ambavyo viko associated na kutumia dawa kama Diclofenac,Aspirin kwa mda mrefu(hizi dawa zinaua kuta za tumbo)
Na kuna ambavyo viko associated na utoaji wa Acid nyingi uko tumboni.
Unakua na ki Uvimbe kwenye Kongosha kinaachia acid nyingi ambazo zinaharibu kuta za tumbo.

Itabidi ku Opt kufanya kipimo cha OGD ku confirm hivo vidonda kwa kupigwa camera kabisa.

Maana yake wewe utaitaji kuonwa na Daktari Bingwa wa Matumbo na Ini wanaitwa GastroEnterologist ndo anaweza kufanya hicho kipimo cha OGD na aka establish kisababishi cha hivo vidonda vya tumbo nje na hiyo sababu ya kila siku!
 
Nazozikumbuka kwa harakaharaka kwa majina ni jamii za omeprazole na dawa inaitwa hyplori kit nadhani,sasa iko kipimo cha OGD kinapatikana hata hospital za mkoa au
 
Nazozikumbuka kwa harakaharaka kwa majina ni jamii za omeprazole na dawa inaitwa hyplori kit nadhani,sasa iko kipimo cha OGD kinapatikana hata hospital za mkoa auView attachment 827657
Hii ni dawa nzuri ya kutuliza acid.
Ukienda Hospitali za Mkoa watakupa rufaa kwenda kwenye Tertialy hospital kama Mlongazila,MNH,Bugando,KCMC au Mbeya Referal.
Maana huko ndo kuna ma super specialist.
Underline neno Super Specialist.
Ni vizuri ukienda ueleze kwa undani kuwa ulishafanya H.Pyroli test ikawa Negative na ungependa ufanye OGD.

Golden Standard ya ku diagnose vidonda vya tumbo ni kufanya OGD unaingiziwa Endoscopy inavimulika unaviona live bila chenga.

Ila kama ulishatumia dawa kuna chances huyo Mdudu wa H.Pyroli ulishamu eliminate hivo inakubaki kutumia Hizo Rabeprazole na inashauliwa utumie zaidi ya walau week 8.

Na kuna chances ulipewa hiyo H.Pyroli Kit kumu eradicate wakati haukua nae.


Meanwhile ukiwa unatafuta daktari bingwa lazima ubadilishe life style ya maisha kama ulikua unakula vyakula vyenye maanjumati mengi kama pilipili upunguze pamoja na vyakula vikali kama hivo.
Kama unavuta sigara au kunywa pombe sio nzuri kabisa.

Nikukumbushe tu kuwa Vidonda vya tumbo vina complications kuu tatu.

1. Perforation i.e vinaweza kutoa tumbo
2. Gastric Outlet Obstruction i.e kipindi vinajaribu kupona kuta mbili zenye vidonda zinaweza kupona kwa kushikana na kuzuia chakula kutoka tumboni au sehemu ya utumbo kusomga mbele.
3.Hemorrage i.e Vinaweza kuanza kutoa damu na ukaanza kutapika damu au kutoa choo cheusi kama mkaa na inaweza kukufanya uishiwe damu kila mara.
 
Dhaa asante sana mkuu yaan vitu kama mapombe,masigara sijawai tumiaga ila mapilipili,maharage,vitu vichachuvichachu nilishaacha kutumia,sasa mkuu iko kipimo kinaweza gharimu bei gani labda ili niitafute nikapime
 
OGD daah upimaji wake ulinishinda kabisa yan. Ile camera kuingizwa kooni duuh.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…