Juisi ya miwa ni salama?

Juisi ya miwa ni salama?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,478
Reaction score
3,659
Hapa Dar kuna sehemu nyingi tu ambapo juisi ya miwa inatengenezwa. Mazingira ya utengenezaji yanatishia usalama wa afya za watumiaji. Kiukweli ni kuna uchafu mwinngi kwenye maandalizi ya hii juisi. Mamlaka zinazohusika zinajua haya?
 
duu hii kitu ni balaa kama pale kariakoo mtaa wa uhuru kituo cha daladala kongo ni hatari tu ingawa si pazuri kiivyo ila juisi zake tamu balaa..

kwa mambo ya afya hapa ni mungu tu anasaidia..
 
Huwa naona wanaonunua ile juice wana roho ngumu kweli. Unakuta jamaa anayarudishia yale makapi kwenye mashine with bare hands, huku mikono hiyo hiyo akijipangusa kwenye suruali yake chafu au akijikuna au akipangusa jasho na kamasi, na wakati mwingine nzi wanadondokea kwenye juisi na analazimika kuwaondoa, halafu unakuta watu wamepanga foleni kusubiri juisi kwa vikombe vya ku.share, na uoshaji wa kikombe ni wa kutumbukiza kwenye maji na kukiibua, na maji yenyewe ni hayo hayo wala hayabadilishwi! Huwa nawashangaa sana jamaa pale Buguruni-Chama
 
Kiukweli si kama nasema juisi ni mbaya ila wanaoandaa na wanaokunywa hawajui lolote kuhusu madhara yatokanayo na mazingira ya maandalizi ya juisi yenyewe. Unakuta miwa imerundikwa sehemu wk nzima, imeanza kuoza, jamaa wanaichomoa hapo na kuikwangua na visu kisha wanaichomeka kwenye mashine zao.
 
sijawai kunywa juisi ya miwa sio kuwa siipendi la hasha utengenezwaji wake daaaaaaaaa!
sijawahi ona wanaotengeneza hiyo juice kiusafi coz ata kama ye mwenyewe atakuwa msafi lakini ukamuliwaji wake hauridhishi utakuta mabati ya kupeleka juisi kwenye chombo ni kichafu yaani ni full kichefuchefu.
 
Biashara ya wapemba hiyo buguruni, tandika na kariakoo.

Wanasema ni nzuri.. Ila binafsi sio mtumiaji kwakuwa watengenezaji wengi huwa katika mazingira ya uchafu
 
Endeleeeni kunywa Redbull hakuna shida alafu muone kati ya sisi na ninyi nani ataanza kuuguaa !
 
Endeleeeni kunywa Redbull hakuna shida alafu muone kati ya sisi na ninyi nani ataanza kuuguaa !

Hadi nimecheka, dah! Nakushauri uwe unanunua miwa ukale home. Ile juisi ina mengi ndugu, sijui ni kwa nini nyie wanywaji hamwoni.
 
sijawai kunywa juisi ya miwa
sio kuwa siipendi la hasha utengenezwaji wake daaaaaaaaa!
sijawahi ona wanaotengeneza hiyo juice kiusafi coz ata kama ye mwenyewe
atakuwa msafi lakini ukamuliwaji wake hauridhishi utakuta mabati ya
kupeleka juisi kwenye chombo ni kichafu yaani ni full
kichefuchefu.
kuna jamaa pale karibu na usesi bar pale maeneo ya makubur jamaa anatengeneza juice kwa mashine ya kisasa na kwa usafi wa hali ya juu sana,namkubal sana huyu jamaa,tena ni msabato,yupo smat sana.
 
kuna jamaa pale karibu na usesi bar pale maeneo ya makubur jamaa anatengeneza juice kwa mashine ya kisasa na kwa usafi wa hali ya juu sana,namkubal sana huyu jamaa,tena ni msabato,yupo smat sana.
dam nanni kakuuliza upuuzi tu.usimwangie mtu na biashara yake na udini wako.
 
mara ya pili ulikunywa wapi mkuu?

Kibada pale stand. Kuna jamaa wanauza juice na half cake. Napenda sana hii kitu.

Kuna wakati nilitafuta sana mashine yake nikaenda mpaka sido sijaipata, later nikasikia wadau wanasema zinapatikana Magomeni lakini by then nilikuwa nishaamua kupotezea...
 
pia nasikia juice ya miwa ni nzuri na inarudisha heshima nyumbani!
 
Back
Top Bottom