Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532

JUISI YA NDIZI MBIVU
NDIZI ni zao linalotokana na mgomba, zao hili likiwa bichi hutumika kama chakula na likiwa limeiva (ndizi mbivu) hutumika kama tunda ambalo wakati mwingine hutumika kutengeneza juisi.
Kwa hapa kwetu Tanzania ndizi hupatikana kwa wingi mkoani Kagera, Mbeya na Kilimanjaro ambako kwa mkoa wa Kagera na Kilimanjaro kwao ni chakula kikuu. Leo katika safu hii ya mapishi tutajifunza namna ya kutengeneza juisi ya ndizi mbivu.
Mahitaji
• Ndizi mbivu kulingana na hitaji lako
• Maji
• Pasheni kiasi.
Namna ya kutengeneza juisi ya ndizi.
1. Safisha ndizi na pasheni kwa maji safi na salama
2. Menya ndizi, katakata vipande vidogo vidogo.
3. Weka kwenye blenda saga mpaka ilainike vizuri.
4. Kata mapasheni utoe mbegu zilizopo ndani, uhifadhi kwenye chombo safi na salama.
5. Saga mbegu za pensheni sekunde 40.
6. Chuja mapensheni, changanya na juisi ya ndizi.
7. Koroga mchanganyiko vizuri, weka maji kiasi na koroga juisi yako.
8. Juisi itakua tayari.
Faida ya kula ndizi mbivu
Kwa mujibu wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania inasema kuwa, Vitamin B6 iliyomo kwenye ndizi mbivu, hurekebisha kiwango cha sukari kwenye mwili wa binadamu ambacho huweza kuathiri hali ya mtu.
Kama wewe ni miongoni mwa wale akina mama wanaopatwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa hedhi, unashauriwa kula ndizi mbivu inaweza kukusaidia tatizo lako. Ikiwa mama mjamzito atatumia ndizi mbivu mara kwa mara ni wazi kuwa atakuwa mwenye muonekano mzuri na wa kuvutia.
Deusdedit Mahunda blog