Chanzo: onlymyhealth.com
Hedhi huanza kutokea kwa wanawake pindi wanapopevuka. Katika kipindi cha hedhi wanawake wanahitaji kujisitiri vizuri ili kuhakikisha wanakua safi na salama wakati wote wakiendelea kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Hedhi sio jambo la hiyari kwa mwanamke, ni jambo ambalo kila mwanamke mwenye afya njema lazima apitie pindi atakapopevuka.
Katika kipindi cha hedhi mwanamke anahitaji kujisitiri vizuri kwa kutumia taulo za kike ambazo huuzwa. Lakini kwenye jamii zetu wapo watoto wa kike na wanawake walio kwenye familia zenye vipato vya chini visivyomudu gharama za kununua taulo za kike. Jambo hili hupelekea kushindwa kujisitiri vizuri kwenye kipindi hicho hivyo kuathiri utekelezaji wa shughuli zao. Kwa kutambua hili imetengwa tarehe 28 Mei kila mwaka kwaajili ya kuadhimisha siku ya hedhi duniani.
Utafiti uliofanywa na AAPH huko Tanga uliopewa jina “Harnessing longitudinal data and digital technologies to improve adolescent health in Tanzania” ulionyesha kuwa zaidi ya theluthi moja (35%) ya wasichana walikuwa wakitumia kitambaa au vipande vya nguo, na takriban 20% ya wasichana walikosa shule kwa sababu ya ukosefu wa bidhaa za usafi na 12% kwa sababu ya hofu ya kuvuja.
Tatizo jingine ni kwamba hedhi inachukuliwa kuwa jambo lisilo la kawaida katika jamii zetu, na hivyo ni vigumu kwa wasichana kutafuta msaada na wanaona aibu wanapokuwa katika hedhi. Pia ukosefu wa mfumo wa msaada kwa wasichana/wanawake wakati huu; takriban 15.9% ya wasichana waliripotiwa kukosa shule kwa siku 1 mpaka 2 kwa sababu ya hedhi, haswa kwa sababu ya maumivu, ukosefu wa vyumba vya kubadilisha nguo, ukosefu wa vifaa safi na vinavyofaa katika maliwato, na ukosefu wa maji, lakini hakukuwa na mfumo elekezi wa kuwasaidia ili kulipia masomo yaliyokosa
Changamoto hii imepelekea kujitokeza kwa wafadhili na mashirika mbalimbali wanaojitoa kununua na kuchangisha michango ya kununua taulo za kike kwaajili ya kuwasaidia wanafunzi wa kike kwakua huathirika zaidi na changamoto hii. Jambo hili ni zuri la kuungwa mkono kwasababu huhakikisha mtoto wa kike hapotezi vipindi vya masomo kutokana na kushindwa kujisitiri vizuri wakati wa hedhi.
Serikali ipo wapi kwenye hili?
Serikali ni kama bado haijajikita vizuri upande huu kwa kuamua kumsitiri mtoto wa kike na mwanamke wakati wa hedhi. Hii ni kwasababu bado bei ya taulo ya kike sio rafiki kwa watu wote na hakuna jitihada zozote kutoka serikalini za kupunguza bei hii ili iwe nafuu na stahimilivu mpaka kwenye familia zenye vipato vidogo.
Kwanini jitihada zinahitajika kwenye jambo hili?
Jitihada za serikali zinahitajika kwenye jambo hili kwakua serikali inahusika kusimamia na kuhakikisha afya bora kwa raia. Lakini pia kupitia mapato yanayokusanywa na serikali yanaweza kutumika kuhakikisha miundombinu bora na unafuu wa bei za vifaa (taulo za kike) ili kuhakikisha hedhi safi na salama kwa watoto wa kike na wanawake nchini.
Serikali inapaswa kulipa kipaumbele suala hili ili kuwazidishia morali wafadhili wanaojitolea kusambaza taulo za kike mashuleni. Itasaidia wanawake kupata vifaa vya kujisitiri kwa urahisi na unafuu jambo litakalowasaidia kuendelea na majumu yao bila bugudha watakapoingia kwenye hedhi wawapo mahali popote.
Pia kutokana na madhara anayoweza kupata mwanamke kutokana na kushindwa kujisitiri vizuri kipindi cha hedhi ikiwemo maambukizi kwenye mfumo wa uzazi, Kushindwa kujiamini, na upotevu wa muda hali inayowapelekea kurudi nyuma kimasomo na kimaendeleo. Kutokana na haya ni vizuri suala la hedhi kupewa kipaumbele ili kuhakikisha hedhi safi na salama kwa mtoto wa kike na mwanamke wa Tanzania.
Nini kifanyike kutoka serikalini?
- Kuondoa kodi kwenye taulo za kike.
Serikali isihofie mapato itakayopoteza kutokana na kuondoa kodi kwenye taulo za kike, bali ifikirie jambo hili litakavyoweza kuleta unafuu kwenye bei ya taulo za kike. Jambo hili litawasaidia wafadhili wa taulo za kike kuweza kununua kwa wingi taulo hizo na kuwafikia wanawake wengi zaidi. Itasaidia kwa kiasi kikubwa kuhakikisha hedhi safi na salama kwa watoto wa kike na wanawake.
- Kuweka ruzuku kwenye taulo za kike.
Kutokana na mapato yanayopatikana nchini itawezekana kutoa ruzuku kwenye taulo za kike ili kuhakikisha yafuatayo,
i. Utoaji wa bure wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na hata vyuo vya kati na vyuo vikuu.
Serikali ya Tanzania inabidi kuungana na baadhi ya nchi kama Zambia, Uganda, Botswana, Kenya na Afrika kusini zinazohakikisha wanafunzi wa kike wanapatiwa taulo za kike bure ili kuhakikisha hedhi salama. Itasaidia kwa kiasi kikubwa watoto wa kike kupata elimu ya uhakika na kuepuka kukosa baadhi ya vipindi kutokana na kuingia kwenye hedhi pindi wakiwa shule na hawajajiandaa.
ii. Upatikanaji wa taulo za kike bure kwenye baadhi ya maeneo ya umma kama vituo vya mabasi, hospitali na ofisi za umma.
Itawasaidia wanawake waliopo safarini na kwenye maeneo ya umma kwaajili ya shughuli mbalimbali pindi watakapoingia kwenye hedhi wakiwa hawajajiandaa kupata taulo za kike kwa urahisi na bure kabisa. Jambo hili litawasaidia kuendelea na shughuli kwa kujiamini kutokana kujisitiri vyema.
iii. Punguzo la bei za taulo za kike
Ruzuku itasaidia pia kupungua kwa bei ya taulo za kike na hata familia za kipato cha chini kuweza kuhimili bei hiyo. Hivyo, itawasaidia wanawake wote nchini kuweza kujisitiri vizuri kipindi cha hedhi na kuhakikisha hedhi safi na salama.
iv. Kuhakikisha miundombinu rafiki kwa wanawake kujisafisha na kujisitiri wakati wa hedhi kwenye maeneo ya umma
Serikali inatakiwa kuhakikisha wakati wa kujenga miundombinu kama shule, hospitali, vituo vya mabasi na ofisi za umma zinajumuisha sehemu ambayo mwanamke ataweza kujisafisha na kujisitiri ikiwemo kubadilisha taulo walizotumia wakati wa hedhi. Pia kuhakikisha sehemu hizo zinapatikana taulo za kike bure ili kuwasaidia wale watakaoingia kwenye hedhi na kutokua nazo kwa wakati huo.
Jambo hili litaepusha wanawake kusitisha shughuli zao na kurejea nyumbali ili kujisafisha na kujisitiri endapo wataingia kwenye hedhi wawapo kwenye maeneo hayo.
Kwaiyo, serikali isichukulie hili kama upotevu wa mapato ya serikali, kwasababu mapato ya serikali yanatokana na shughuli za raia na rasilimali za nchi. Hivyo, mapato hayo ni kwaajili ya kuwahudumia pia wananchi. Wananchi watakaposaidiwa na mapato ya nchi yao itawazidishia ari ya kushughulika na kulipa kodi bila shuruti. Kutumia mapato ya nchi kwaajili ya wananchi isichukuliwe kama upotevu wa mapato hayo. Serikali inabidi kutambua ni wajibu wao kuhakikisha hedhi safi na salama kwa wanawake nchini na kuepuka kuwaachia jukumu hilo wafadhili na mashirika yasio ya kiserikali wakipambana wenyewe.

Upvote
5