Jukwaa gani unapendelea na kwanini ?

kitalembwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2014
Posts
3,607
Reaction score
9,430
Hapa JF kuna majukwaa mengi, kila mtu ana uhuru wa kupitia jukwaa analopenda kulingana na maudhui ya anachotaka kujifunza/kusoma mfano mambo ya elimu, siasa, mapenzi n.k

Binafsi napenda sana majukwaa yafuatayo

1. Jamii Intelligence
Hapa napata madini mengi sana, pia najifunza vitu ambavyo pengine sikudhani ningekuja kujifunza kwenye maisha yangu.

2. Biashara, uchumi na ujasiriamali
Huku najifunza mambo kadha wa kadha na fursa za kujikwamua kiuchumi..

3. MMU
Huku najifunza na kupata uzoefu wa maisha ya mahusiano kwa ujumla kuanzia uchumba mpaka ndoa.

4. Habari na hoja mchanganyiko
Huku napita randomly ili kupata zile habari ambazo pengine sizipati majukwaa mengine, kwa namna moja naweza kuzipata hapa.

5. Jukwaa la elimu
Huku pia najifunza vitu kadha wa kadha. Kwa sasa kuna ule uzi wa bwana mkubwa shebby tunakula madini adimu kuhusu abcd za ndege.

Majukwaa mengine yaliyobaki huwa napita kwa nadra sana, muda mwingine nikiwa free naweza pita chit chat walau kurefresh akili. Pia JF Doctor napitaga mara chache. Siasa napita mara chache mpaka kuwe na trending story kama ile ishu ya Lissu. Celebrity huko nako napita kwa nadra sana, mwezi unaweza kupita bila hata kuingia huko.

Kuna jukwaa kama la kilimo naweza maliza mwaka sijapita huko.

Kwa kifupi hayo ni majukwaa yangu matano pendwa hapa JF. Wewe unapenda majukwaa gani na kwanini?
 
Jukwaa la habari na hoja mchanganyiko
Napenda sana Mada zinazowahusu diaspora ,
 
Jukwaa la habari na hoja mchanganyiko
Napenda sana Mada zinazowahusu diaspora ,
upo sahihi mkuu, hizo mada zinafunza na kuelimisha kiasi chake, japo kebehi zipo anghalabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…