Dar es Salaam. Jukwaa la Katiba (Jukata) limeitaka Serikali kutangaza kwenye gazeti la Serikali tarehe ya kuanza upya kwa mchakato wa Katiba mpya.
Mwenyekiti wa Bodi ya Jukata, Deus Kibamba amewaeleza waandishi wa habari leo kuwa Serikali pia inatakiwa ipeleke bungeni miswada miwili ili kuhuisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 pamoja na Sheria ya Kura za Maoni 2013.