Julai 28: Siku ya Homa ya Ini Duniani (World Hepatitis Day)

Julai 28: Siku ya Homa ya Ini Duniani (World Hepatitis Day)

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Homa ya Ini (Hepatitis) ni Ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya aina mbalimbali. Virusi vinavyosababisha Homa Ya Ini vipo katika makundi matano: A, B, C, D na E

Maadhimisho ya Mwaka 2022 yamejikita katika uhitaji wa kuleta Huduma za Homa ya Ini karibu zaidi na Vituo vya Afya na Jamii ili Wananchi wapate Matibabu bora zaidi

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) takriban 90% ya watu waishio na Homa ya Ini hawafahamu kuwa wanaugua Ugonjwa huo

1658989621646.png

DALILI ZA HOMA YA INI

Baadhi ya dalili za Ugonjwa ni Homa, Kukosa Hamu ya Kula, Kuharisha, Kichefuchefu, Maumivu ya Tumbo, Macho kuwa ya Njano, Kutapika, Maumivu ya Misuli, Uchovu na Mwili kukosa nguvu

Pamoja na dalili hizo, Wataalamu wa Afya wanasema idadi kubwa ya watu walio na Homa ya Ini au 'Hepatitis' A, B, C, D au E huonesha dalili kidogo au kutoonesha dalili kabisa

MAAMBUKIZI YA HOMA YA INI (HEPATITIS)

Miongoni mwa njia kuu za maambukizi ya Homa ya Ini (hutofautiana kulingana na aina ya Kirusi) ni pamoja na Maji/Chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha mtu mwenye maambukizi, kujamiiana bila Kinga na mtu mwenye Ugonjwa

Pia, maambukizi yanaweza kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto wakati wa kujifungua na kuchangia matumizi ya vitu vyenye ncha kali ikiwemo sindano

Damu na majimaji mengine ya mwili kutokwa kwa mtu mwenye maambukizi ikiwemo mate yanaweza kusambaza Ugonjwa huu

UNAWEZAJE KUJIKINGA NA HOMA YA INI?

1) Usichangie matumizi ya vitu vyenye ncha kali vikiwemo viwembe

2) Kunywa Maji na kula Chakula kilichoandaliwa katika mazingira safi na salama

3) Jua Afya yako kwa kufanya vipimo vya Homa ya Ini

4) Matumizi salama ya sindano katika Vituo vya Afya

5) Tumia Kinga kwa usahihi wakati wa kujamiiana

6) Watoto wachanga wapelekwe kupata Chanjo ya Homa ya Ini (B)

======

World Hepatitis Day is observed each year on 28 July to raise awareness of viral hepatitis, which causes inflammation of the liver that leads to severe disease and liver cancer

The world is currently facing a new outbreak of unexplained acute hepatitis infections affecting children. WHO, together with scientists and policymakers in affected countries, are working to understand the cause of this infection that does not appear to belong to any of the known 5 types of hepatitis viruses: A,B,C,D, and E.

This new outbreak brings focus on thousands of acute viral hepatitis infections that occur among children, adolescents and adults every year. Most acute hepatitis infections cause mild disease and even go undetected. But in some cases, they can lead complications and be fatal. In 2019 alone, an estimated 78 000 deaths occurred worldwide due to complications of acute hepatitis A to E infections.

Global efforts prioritize the elimination of the hepatitis infections B, C and D infections. Unlike acute viral hepatitis, these 3 infections cause chronic hepatitis that lasts for several decades and culminate in over 1 million deaths per year from cirrhosis and liver cancer. These 3 types of chronic hepatitis infections are responsible for over 95% of hepatitis deaths. While we have the guidance and tools to diagnose, treat, and prevent chronic viral hepatitis, these services are often out of reach of communities and are sometimes only available at centralized/specialized hospitals.

On World Hepatitis Day 2022, WHO is highlighting the need for bringing hepatitis care closer to the primary health facilities and communities so that people have better access to treatment and care, no matter what type of hepatitis they may have.

WHO aims to achieve hepatitis elimination by 2030. To get there, WHO calls on countries to achieve specific targets:
  • Reduce new infections of hepatitis B and C by 90%;
  • Reduce hepatitis related deaths from liver cirrhosis and cancer by 65%;
  • Ensure that at least 90% of people with hepatitis B and C virus are diagnosed; and
  • At least 80% of those eligible receive appropriate treatment.
Source: WHO

Pia soma >>> Ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis B): Dalili, ushauri wa kinga na tiba yake
 
Mwaka 2018 Kaka yangu alifariki muhimbili kwa homa ini.alikuwa Yuko chuo mwaka wa mwisho UDOM computer science aliugua homa ya ini akapelekwa general hospital Kisha wakampa rufaa kuja muhimbili.Alikuja na baba wakanikuta niko chuo ikabidi niwe nawasindikiza kwenda Muhimbili kitengo Cha magonjwa ya mfumo wa chakula.kiukweli alikuwa halali usiku analia maumivu ya tumbo pembeni mwa kitovu.

Baada ya vipimo kufanyika dokta alituita Mimi na baba ofisini kwake akatuambia ndugu yenu haponi Tena hepatitis imemla kiasi kwamba imedevelop kuwa cancer hivyo Hana muda mrefu kuishi ana mwezi mmoja tu na taasisi Yao haina msaada mwingine labda tujaribu njia nyingine.Baba alimchukua mgonjwa kuelekea arusha kwa ajili ya maombezi ambayo hayakumpa nafuu baba alitamani aanze kutembea kwa waganga.alipokuwa safarini katika basi kutoka arusha mgonjwa aliomba chipsi mayai akaonja kidogo Kisha akampa baba amalizie akalala begani kwa baba na kulala mazima.
Mgonjwa hakuwahi kutumia kilevi chochote kile maishani mwake.Nawashauri vijana wenzagu ambao mnajijua mna maisha ya rough na mpo kwenye risk twendeni tukapatiwe chanjo ya homa ya ini.
 
Dah so sad.

Poleni sana
 
Ila huu ugonjwa sema unatesa mno.

Alafu kutojua TU .Mimi naifahamu dawa ya kuutibu na nimetibu wengi mno wamepona. Ebu mwenye tatizo hili tuwasiliane 0717707565
 
Back
Top Bottom