Julio aikacha Kilimanajaro Stars

Mwanagandila

Senior Member
Joined
Oct 9, 2011
Posts
182
Reaction score
100
Kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars Jamhuri Kiwelu (Julio) ameikimbia timu hiyo jana jioni na kuelekea Uarabuni.
Kocha huyo ameikimbia timu hiyo baada ya kufanya vibaya na kuzomewa na mashabiki kwa soka lake bovu toka siku ya wake wa kwanza dhidi ya Rwanda.
Kilimanjaro Stars leo inacheza dhidi ya Sudan kusaka mshindi wa tatu.
Swali kama alimfukuza Boban & Taita timu hiyo kwa utovu wa nidhamu, je na yeye kitendo alichokifanya anastahili kupewa adhabu kwa utovu wa nidhamu?
 
Hapo ndipo tunapopata nafasi ya kujua which is which. Aliwataja hao "wateule" wake kwa mbwembwe sana, na miongoni mwao ni wale walioonekana na makocha maprofesheno kuwa hawana nidhamu. Wao wakawakumbatia, na kama usemayo Mwanagandila ni ya kweli then na yeye imemghalimu maana wamemuambukiza utovu wa nidhamu. Mpira si kupiga danadana, chenga na magoli tu, kuna vitu vingine vingi vya ziada ambavyo bahati mbaya sana inaonekana bado hatujavigundua umuhimu wake. Nenda Julio kwa waarabu na sie tunakutoa nenda!
 
Julio kaishia darasa la saba,ni vigumu sana kuweza kufanya chochote kwa kiwango cha elimu ya julio
 
Hawa wakina Julio walikuwa wanampiga sana majungu Maximo kuwa hawezi kazi; wamepewa nafasi wenyewe matokeo ndio hayo wanakimbia hadi timu. Tatizo la wabongo tumepoliticize hadi football. Hii hali itatughalimu sana mbeleni.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…