Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 351
- 887
MJUE GAIUS JULIUS CAESAR MWASISI WA DOLA HIMAYA NA MILIKI KUU YA ROMA AMBAYE JINA LAKE “CAESAR” LILIFANYWA CHEO KILICHOTUMIKA BAADAE KWA VIONGOZI WAKUU WA DOLA HIYO IKIWA NI PAMOJA NA KUTANGAZWA KUWA MUNGU.
Na Comred Mbwana Allyamtu.
Sunday- 8/10/2017
Dola la Roma Kwa karne kadhaa lilikuwa milki kubwa katika nchi zinazopakana na bahari ya Mediteranea. Itakumbukwa kuwa Dola ya Roma ndio iliyokuwa Dola himaya na miliki kuu ya ulimwengu ya nne (4) (The 4th World Super-Supremacy Empire “4th Hegemony”) iliyoitwaa dunia baada ya anguko la ile iliyokuwa miliki ya Ugiliki.
Dola ya Roma ilianza kwenye mji mkuu wa Roma na baadae kuenea mpaka rasi ya Italia ikaendelea kuunganisha makabila na mataifa ya nchi nyingi kwenye mabara matatu ya Ulaya, Afrika na Asia. Kuanzia karne ya 1 KK (KK –inamaanisha kabla ya kristo) Watawala wa Dola wakaitwa makaisari na jina hili Kaisari jina ambalo lilitokana na Muasisi wa dola hiyo aliyeitwa Julius Caiser, ambaye tunakwenda kumpebua hapo baadae.
Kimsingi jina ‘’Kaizari’’ ni cheo cha mfalme mkuu. Neno la Kiswahili limetokana na lugha ya Kijerumani "Kaiser", lakini asili yake ni lugha ya Kilatini "Caesar" neno lenyewe linatokana na neno Lenye asili ya Kiroma Asili ya cheo hiki ni muasisi wa dola hii aliyeitwa ni Julius Caesar au Gaius Julius Caesar kama anavyoitwa ambaye makala hii itakwenda kudulufu historia yake kwa upembuzi yakinifu juu ya kiongozi huyu aliyekuwa kiongozi wa Dola la Roma aliyeifanaya dola yake kuja kuwa Miliki kuu na Dola himaya ya nne (4) iliyokuja kuogopewa na dunia nzima lakini kubwa ni athira yake imetamalaki Dunia mpaka leo.
Gaius Julius Caesar aliyekuwa kiongozi wa Dola la Roma hadi kuuawa kwake na wapinzani mwaka 44 KK. Watawala waliomfuata walianza kutumia jina la Caesar Kwa heshima yake hadi jina likawa cheo kilicho tumika baadae kwa viongozi wakuu waliomfuata.
JE JULIUS CAESAR NI NANI?
Julius Caesar alikuwa ni Kiongozi mkuu wa dola ya Roma ambaye baadae alikuja kufanywa Mungu wa dola hiyo, kwa majina yake alitambulika kwa jina la Gaius Julius Caesar (Tamka Gayus yulius kaesar aliyezaliwa mnamo mwaka 100 KK - na kufaliki kwa kuuwawa mwaka 44 KK) alikuwa kiongozi wa kisiasa na wa kijeshi wa Roma ya Kale (Rome Empire). Anakumbukwa hasa kwa mafanikio mbalimbali yanayoonekana kuathiri dunia hadi leo. Baadhi ya mafanikio hayo ni Kama kiongozi wa kijeshi aliteka eneo la Gallia (leo: Ufaransa) na kuifanya jimbo la Kiroma. Kutokana na hiyo lugha ya Kifaransa ni karibu sana na Kilatini, ambayo ni lugha ya Roma ya Kale.
Waroma wa Kale walimheshimu kushinda viongozi wote waliomfuata au kutangulia hivyo akatangazwa kuwa mungu. Jina lake lilipata kuwa neno Kwa ajili ya cheo cha watawala wa Kiroma waliomfuata. Kutokana na badiliko hilo la jina "Caesar" kuwa cheo, lugha mbalimbali zilipokea cheo hicho kama vile Kijerumani ("Kaiser"), Kirusi ("Tsar") na Kiswahili ("Kaisari" - kutokana na neno la Kijerumani).
Aliunda kalenda ambayo imekuwa msingi wa kalenda ya kimataifa ya leo inayotambulika kama Kalenda ya Juliasi (Julia calendar). Kwa heshima yake, mwezi wa saba unaitwa Julai. Kutokana na jina lake Katika historia ya Roma alifunga kipindi cha Jamhuri na kilichofuata ni Dola la Roma aliloliwekea misingi kama himaya kuu na miliki kama dola.
KUZALIWA, KUJIHUSISHA NA SIASA MPAKA KUWA KIONGOZI
Gaius Julius Caesar Alizaliwa katika familia ya makabaila (feud Lord) wakati huu dunia ilikuwa chini ya mfumo wa feudalism (ukabaila) na familia yake ilikuwa ni makabaila wenye nafasi katika Senatus ilivyoitwa bunge la Roma kwa wakati huo. Senatus ilikuwa ndio bunge kuu la doya ya roman a Katika dola ya Roma kwa wakati huo ilitambulika kama ya jamhuri.
Kwa karne zilizofuata Waroma walifuata katiba iliyolenga kuzuia asitokee mfalme mpya. Hivyo katiba hiyo iliipa mamlaka bunge la Roma (Senatus) kuteua Vyeo vyote vya nchi hiyo hivyo vyeo vilitolewa kwa muda tu kwa njia ya uchaguzi. Madaraka yaligawiwa kati ya ngazi na vyeo mbalimbali. Vyeo vingi vilitolewa kwa watu wawili kwa kipindi kilekile kwa sharti la kwamba hao wapatane na kuangaliana. Kila mtu aliruhusiwa kuwa na cheo fulani kwa muda wa mwaka 1 pekee, Hakuruhusiwa kuwa na kipindi cha pili kwenye cheo kilekile, Aliyechaguliwa kupata cheo hakuruhusiwa kugombea cheo kingine mara moja, Kila cheo kilikuwa na nafasi mbili.
Hao watendaji wawili waliochanga cheo kimoja walipaswa kupatana; kila mmoja aliweza kufuta maazimio ya mwenzake., Mgombea wa cheo fulani alipaswa kutangulia katika utendaji wa cheo cha chini kabla ya kupanda juu, Kati ya kugombea vyeo viwili mgombea alipaswa kupumzika mwaka mmoja.
Kulikuwa na cheo kimoja pekee kilichotekelezwa na mtu mmoja tu kilichoitwa dikteta. Dikteta aliweza kuchaguliwa katika kipindi cha dharura kama vita kwa muda wa miezi sita. Katika kipindi hiki alifanya maazimio peke yake. Kwa kawaida watendaji wakuu walikuwa makonsuli ("consules") waliochaguliwa kwa muda wa mwaka 1.
Kutokana na katiba hiyo Gaius Julius Caesar Aliingia katika siasa, akachaguliwa kwa vyeo mbalimbali kwa vipindi vya kawaida wa miezi kadhaa hadi mwaka moja. Baadae Cheo chake muhimu cha kwanza kilikuwa mkuu wa koloni la Kiroma la Hispania.
Alifaulu kushinda ghasia ya Wahispania wenyeji waliojaribu kuwafukuza Waroma kutoka nchini mwao. Caesar aliporudi Roma alitajirika na kujipatia sifa kama kiongozi wa kijeshi pia mwanasiasa aliyeokoa koloni muhimu la Hispania jambo hili lilimfanya awe imara sana kisiasa.
Baadaye Gaius Julius Caesar au ‘’Caesar’’ kama alivyo tambulika alijiunga na wanasiasa wawili wengine waliofahamika kwa majina ya Gnaeus Pompeius Magnus aliyekuwa mkuu wa wanajeshi na mwingine aliyefahamika kama Marcus Licinius Crassus aliyekuwa tajiri kushinda Waroma wote. Wote watatu kwa pamoja waliunda umoja ulioitwa "Triumviratus", yaani umoja wa wanaume watatu, wakashika mamlaka katika dola. Caesar alichaguliwa kwa cheo kikuu yaani Konsul kwa mwaka 59 KK.
Baada ya mwisho wa kipindi chake alijipatia cheo cha Prokonsul au gavana wa eneo la Gallia ya Kiroma (Italia ya Kaskazini na eneo dogo la Ufaransa ya Kusini).
KUIBUKA VITA YA GALLIA (UFARANSA) NA KUIMALIKA KWA GAIUS JULIUS CAESAR
Alitumia nafasi hii kuanzisha vita dhidi ya makabila ya Gallia huru yaani eneo lote la Ufaransa, Uswisi na Ubelgiji ya leo. Katika miaka minane ya 58 - 51 KK alitwaa Gallia yote. Aliingia pia ndani ya Germania (Ujerumani) na kuvuka bahari aliposhambulia upande wa kusini wa Britannia. Aliandika kitabu cha "De bello gallico" (yaani Vita ya Gallia) akieleza mapigano yake. Kitabu hicho kina habari muhimu za kihistoria juu ya utamaduni wa makabila ya Gallia, Germania na Britannia aliyopigana nayo.
Pia baada ya kuitwa himaya yote ya magaharibi kuliibuka Vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya miliki ya Rome Baada ya kufanikiwa Gallia na kujenga jeshi kubwa tena hodari, wanasiasa wengine huko Roma walianza kumwogopa wakajaribu kumzuia asirudi Italia.
Mwenzake Crassus alikuwa amekufa tayari vitani mashariki mwa dola mwenzake Pompeius aliomwogopa Caesar akajaribu kushawishi viongozi wengine kumsimamisha. Lakini mwaka 49 KK Caesar aliongoza wanajeshi wake warudi Italia. Pompeius na wapinzani wake walitoka Roma wakaenda Ugiriki iliyokuwa jimbo la Kiroma.
Mwaka 48 KK Caesar akachaguliwa tena kuwa Konsul. Akamfuata Pompeius kwa jeshi lake akamshinda katika mapigano. Pompeius alikimbia kwenda Misri lakini mfalme Ptolemaio XIII wa Misiri alimwogopa Caesar akamwua Pompeius akampatia Caesar kichwa chake alipofika Misri. Caesar alikutana na dada yake Ptolemaio aliyeitwa Kleopatra akampenda na kumfanya mpenzi wake ambaye pia aliamua kuzaliana naye mwana wake pekee. Kutokana na hali hiyo baadae akamsaidia Kleopatra kuwa malkia na mtawala wa Misri.
GAIUS JULIUS CAESAR KUCHAGULIWA KUWA DIKTETA HADI KIFO CHAKE
Gaius Julius Caesar baadae alirudi Roma kutoka Misri akiwa mshindi dhidi ya wapinzani wote. Bunge la Senatus lilimpa cheo na madaraka ya dikteta kwa miaka 10. Baada ya ushindi mwingine dhidi ya wapinzani huko Hispania bunge lilibadilisha azimio hilo kumpa cheo cha dikteta wa maisha. Ikiwa ni pamoja na kupitisha azimio la Caesar kuwa kiongozi wa taifa na dola, itakumbukwa kuwa Gaius Julius Caesar alikuwa binadamu wa kwanza aliyeonyeshwa kwenye sarafu za Roma. Hata hivyo Caesar alipokea azimio hili.
Kutokana na kuimalika kwa Gaius Julius Caesar katika siasa za Roma Sasa sehemu ya wabunge waliogopa ya kwamba nia yake ilikuwa kuwa mfalme wa Roma jambo lililokuwa marufuku katika jamhuri ya Roma. Kikundi cha wabunge wote makabaila (Feud Lord) wa familia za kale kiliunga mikono wakamwua Caesar bungeni tarehe 15 Machi 44 KK tarehe hii hukumbukwa katika historia ya Roma kama anguko la Nuru ya dola kwa kumdunga kisu mara 23. Gaius Julius Caesar anasemekana alimtambua mpwa wake aliyetambilika kwa jina la Brutus akamwuliza kwa maneno yake ya mwisho kwa kusema "Hata wewe mwanangu?"
Caesar hakuwa na watoto ila huyu mwana wa Kleopatra asiyekuwa Mroma aliyemzaa na malikia wa Misir. Kabla ya kifo chake alikuwa amempanga mtoto ambaye alikuwa ni mpwa wake aliyeitwa Oktaviano (Agusto Gaius Julius Caesar). Huyu Oktaviano aliyejulikana baadaye kama Augusto na mtawala wa kwanza wa Dola la Roma alilipiza kisasi chake katika kipindi cha vita ya wenyewe kwa wenyewe na kuua wapinzani wote wa Caesar walio shiliki kumuua mjomba wake Gaius Julius Caesar.
Hata hivyo kufuatia kifo chake Miaka miwili baada ya kifo chake bunge lilimtangaza Caesar kuwa mungu. Ikiwa ni pamoja na jina la Caesar Kwa heshima yake hadi jina likawa cheo kilicho tumika baadae kwa viongozi wakuu waliomfuata katika Himaya kuu na miliki ya dora la Roma na toka hapo tarehe 15 Machi 44 KK ya kifo chake imefanywa kuwa tarehe ya kumbukizi yenye heshima mpaka leo huko Italy
[emoji768]Wako Mjuvi wa Historia ya dunia na mambo ya dipromasia ya dunia......
Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com.