Katibu Mkuu anajibuje waraka unaopingana na maamuzi halali ya vikao?
Kwamba ajipe mamlaka zaidi ya vikao vya kamati kuu, baraza kuu na mkutano Mkuu.
Kiufupi watajibiwa kwa njia waliyoupelekea. Wao kwanza wameanza na kuunda kundi ndani ya Chama na kujipa jina kabisa kinyume na Chama na Taasisi zilizo chini ya Chama mfano mabaraza ya Chama.
Sasa kwa mtindo huu kama wakijibiwa kama G55 hawaoni watafanya kila watu ndani ya Chama wakiwa na agenda yao waunde kakikundi kao?
Utajibuje kikundi ambacho hakitambuliki wala kusajiriwa hata kwenye serikali ya mtaa?
Kuwajibu ni kuhalalisha utovu wao wa nidhamu na kutambua kundi la kihuni ambalo halijulikani na mamlaka zinazohusika na vikundi.
Sasa akiwajibu address yao inapatikana wapi na ofisi zao zinapatikana wapi?