Juma Duni Haji

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
JUMA DUNI HAJI

Nilikutana na Juma Duni Haji kwa mara ya kwanza chumbani kwa Maalim Seif Starlight Hotel mwaka wa 1995 CUF ikiwa katika harakati za Uchaguzi Mkuu wa kwanza baada ya kurejeshwa vyama vingi.

Juma Duni alikuwa ndiyo kawasili kutoka masomoni Uingereza na kaja moja kwa moja akitokea uwanja wa ndege kuonana na Maalim.

Katika chumba kile kulikuwa na watu wengine pamoja na mimi.

Tulikuwa katika kikao kizito.

Maalim akatutambulisha kuwa Juma Duni ni mgombea wake mwenza Zanzibar.

Urafiki wangu na Juma Duni ulianzia hapo na siku ile.

Juma Duni yupo katika shajara zangu na katika maktaba yangu ya picha.

Nilikuwa nafatilia haya yaliyotokea na leo nilipoletewa taarifa kuwa kaliondoa jina lake katika kugombea nafasi ya uenyekiti sikushangaa.

Juma Duni Haji katoka mbali na harakati za ukombozi na kapita ndani ya tanuri la moto.

Juma Duni Haji anajua faida ya subra, ustahamilivu na nguvu ya umoja katika chama na ndani ya chama.

Juma Duni Haji kaona yote kwa macho yake na akiwa mchezaji wa duru la ndani.

Juma Duni Haji hajapata kuwa mchezea pembeni.

Juma Duni Haji kasaidia kukiongoza chombo hadi bandarini kwa salama na amani.

Haya ni mepesi ikiwa nia ni kuwapa ushindi wanachama na kuipa ushindi nchi yetu.

Leo ACT Wazalendo imeshinda na sote ni washindi.

Tumekuwa washindi siku zote.
Historia yetu inajieleza wenyewe.

Hakika kutoka 1995 hadi leo 2024 ni mwendo mrefu.


Juma Duni Hajji akihutubia mkutano Korogwe
Uchaguzi Mkuu 1995 kushoto ni Akida Mbaruku Nyenga

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba akihutubia mkutano wa kampeni Korogwe pembeni yake ni Juma Duni Haji.

Kushoto: Mohamed Omari Mkwawa, Juma Duni Haji na Prof. Ibrahim Haruna Lipumba nyumbani kwa Mama Ummy bint Anzuani, Ngamiani Tanga Mdhamini wa CUF Uchaguzi Mkuu 1995.


Prof. Lipumba na Juma Duni wakiwa White Rose Hotel Tanga, Uchaguzi Mkuu 1995.​
 
Ahsante umetujuza vema, kumbe ni wewe ni mwanachama wa ACT-Wazalendo.
 
Ahsante umetujuza vema, kumbe ni wewe ni mwanachama wa ACT-Wazalendo.
Nguruvi3,
Nilikuwa CUF sasa niko ACT Wazalendo.


Kushoto Juma Duni Haji, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba na Mwandishi (Mohamed Said Salum Abdallah) nyumbani kwa Mama Ummy bint Anzwani (Mdhamini wa CUF), Ngamiani Tanga, Uchaguzi Mkuu 1995.​
 
Duh sijawasikia wala kuwaona Wagalatia,Ustadhi kila sehemu waliojazana wavaa makubazi wewe upo.

Uongozi wa ACT kama Baraza la Ulama.
 
Kipindi cha jiwe uliufyata usingethubutu kusema we Cuf au ACT
 
Kipindi cha jiwe uliufyata usingethubutu kusema we Cuf au ACT
Mdukuzi,
Mjadala unapendeza ikiwa tunajadiliana kwa adabu.

Tunakuwa na staha baina yetu.

Maneno "kufyata," hayapendezi kumwambia mtu.

Ni matusi.

Ungeweza kuniambia kuwa nisingeweza kusema mimi CUF nk.

Ungeeleweka.

Swali hili nimelijibu mara kadhaa kuwa mimi niko hapa kwa maandishi, sauti na picha nikitumia jina langu halisi.

Sijapatapo kujificha na sijajificha kuwa niliipigania CUF.

Fanya search utakuta makala zangu pamoja na picha.
 
Umeandika wasifu wa Duni Haji vipi kafariki?
 
Umeandika wasifu wa Duni Haji vipi kafariki?
Shoto...
Juma Duni ameondoa jina lake katika kugombea nafasi ya Uenyekiti wa ACT Wazalendo.

Wengi katika vijana wanachama hawamjui.

Ndiyo nimeandika historia yake wamfahamu.
 
Kwenye picha ya mwisho huyo jamaa wa pili kushoto ndiye yule alikuwa Mbunge wa Lindi Mjini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…