Juma Kaseja anatafuta kiki kwa Djigui Diara

Nyanda Banka

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
304
Reaction score
1,054
JUMA KASEJA: KILA KITU DIARRA ANACHOFANYA MIMI NILISHAKIFANYA ENZI ZANGU.

Nyota wa zamani wa klabu ya Simba Juma Kaseja ameweka wazi kuwa ubora anaouonyesha nyota wa klabu ya Yanga Djigui Diarra, yeye aliwahi kuuonesha mapema.

"Diarra ni golikipa mzuri sana.Vitu ambavyo anafanya ndani ya klabu ya Yanga ni vikubwa sana lakini hata mimi enzi zangu nilikuwa navifanya."

"Mimi kabla ya kuwa golikipa nilikuwa mchezaji wa ndani kwa hiyo kuwa nina uwezo mzuri mguuni kwa sababu kabla ya kuwa golikipa nilikuwa mchezaji wa ndani

- Juma K Juma, nyota wa zamani wa Yanga, Simba na timu ya Taifa ya Tanzania.

Unakubaliana na Juma kaseja?
 
Attachments

  • FB_IMG_17183000407436865.jpg
    FB_IMG_17183000407436865.jpg
    217.8 KB · Views: 4
JUMA KASEJA: KILA KITU DIARRA ANACHOFANYA MIMI NILISHAKIFANYA ENZI ZANGU.

Nyota wa zamani wa klabu ya Simba Juma Kaseja ameweka wazi kuwa ubora anaouonyesha nyota wa klabu ya Yanga Djigui Diarra, yeye aliwahi kuuonesha mapema.

"Diarra ni golikipa mzuri sana.Vitu ambavyo anafanya ndani ya klabu ya Yanga ni vikubwa sana lakini hata mimi enzi zangu nilikuwa navifanya."

"Mimi kabla ya kuwa golikipa nilikuwa mchezaji wa ndani kwa hiyo kuwa nina uwezo mzuri mguuni kwa sababu kabla ya kuwa golikipa nilikuwa mchezaji wa ndani

- Juma K Juma, nyota wa zamani wa Yanga, Simba na timu ya Taifa ya Tanzania.

Unakubaliana na Juma kaseja?
Hata mimi namfagilia Diarra
 
Ajilinganishe na Manula mwenzake kavuka boda analipwa kwa dollar
Ana medali ya cafcc
Kafika robo Afcon
Kafika robo ya cafcl
Wakati wake alijitahidi ila asijilinganishe na Diara
Ameshajilinganisha halafu wewe unasema asijilinganishe. Tukio la kujilinganisha limeshatokea na kigezo alichotumia ni mfumo wa kipa kuchezea mpira, kutoa pasi n.k sio hizo medali. Hata Diara mwenyewe sidhani kama ana tatizo na hilo.
 
Kaseja aache uongo. Magolikipa wa zamani kama yeye walikuwa ni bora zaidi kwenye kudaka tu mipira, huku foot work zao zikiwa ni mbovu/za kawaida. Yaani kiufupi magolikipa wengi wa zamani walikuwa ni waoga sana kwenye kuchezea mpira (kuwa sehemu ya mchezo kwa kuanzisha mashambulizi, kuanzisha pasi za nyuma, nk)

Hii aina ya magolikipa kama Djugui Diarra, Andre Onana, nk. Imeanza kuonekana kwenye soka miaka ya hivi karibuni.
 
Basi Diara yuko zaidi yake
 
Kaseja akiwa katika ubora wake 2008/2009 ashawahi chezeshwa no 8 kwa dakika kadhaa, Simba ikiwa ya moto na uhakika wa ushindi. Kaseja alikuwa mzuri ila alikuwa katika era isiyo na mafanikio makubwa kimataifa.
 
Kila zama na kitabu chake, hata Mwameja alifanya vema kuliko Kaseja.
Wachezaji karibu wote wa zamani, ukiwasikiliza wanaonekana walikuwa na vipaji extraordinary, vijana wa sasa wanacheza tu, mpira ulikuwa zamani.

Lakini ukiangalia mafanikio ya vilabu vyao kwa ngazi za kimataifa au timu ya Taifa, ni ZERO.

Huo uwezo wao walikuwa wanauonesha wapi?
 
Kaseja aache uongo. Magolikipa wa zamani kama yeye walikuwa ni bora zaidi kwenye kudaka tu mipira, huku foot work zao zikiwa ni mbovu/za kawaida. Yaani kiufupi magolikipa wengi wa zamani walikuwa ni waoga sana kwenye kuchezea mpira (kuwa sehemu ya mchezo kwa kuanzisha mashambulizi, kuanzisha pasi za nyuma, nk)

Hii aina ya magolikipa kama Djugui Diarra, Andre Onana, nk. Imeanza kuonekana kwenye soka miaka ya hivi karibuni.
Ndugu ulimuona juma kaseja akicheza ? Mpaka faulo alikuwa anapiga na penalty ndani ya dk 90 ni za kwake au ulikuwa unasiliza kupitia redio ,juma kaseja alikuwa anageuza washambuliaji wa team pinzani anavyotaka yeye,kiufupi kafanya mengi ,kwenye short stopping, penalty saving aliiuwa extra miles
 
Back
Top Bottom