Juma Kiroboto 'Nature': Watu wanahonga ili nyimbo zangu zisipigwe

Mshamba wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2015
Posts
2,857
Reaction score
3,593
Ukizungungumzia historia ya muziki wa Bongo Flava, haiwezi kukamilika bila kulitaja jina la mkongwe Juma Kassim Nature aliyewahi kutamba ngoma kama ‘Jinsi Kijana’, ‘Hili Game’ na zingine kibao.

Hatimaye mkongwe huyo amaibuka na kudai kuwa kuna watu wanahonga ili nyimbo zake na za TMK Halisi zisichezwe redioni. Nature amesema kuwa miongoni mwa watu hao ni uongozinwake wa zamani lakini hakuwa tayari kuwataja kwa majina.

“Sasa hivi kuna urasimu, kuna watu wanaenda kuhonga nyimbo zangu zisipigwe za Halisi zisipigwe, wapo watu wanafanya issue kama hizo na tayari tumeshaingia in deep kujua nini tatizo kwanini nyimbo hazichezwi,” ameniambia Nature nilipozungungumza naye nyumbani kwake Temeke.

Ikumbukwe Nature alikuwa akifanya kazi chini ya kundi la Wanaume Family kundi linalomilikiwa na Said Fella kabla ya kujitoa kwenye kundi na baadhi ya wasanii wengine waliokuwa kwenye kundi hilo na kuanzisha kundi lao jipya
linalofahamika kama Wanaume Halisi.
 
Yaani Fella apoteze hela kwa ajili ya hizo nyimbo za kupumbav? Basi Fela anapesa za mchezo
 
Jinsi kijana anavyobadili tabia aise nurture ni msani sahihi makini nature ni namba 1 kwangu
 
Akubali tu alibugi alipoachana na fella!
 
Anatafuta kiki tu, basi atangaze anatembea na zari ili apate kiki watu wataanza mkumbuka
 
akina ally kibakuli wapo wengi
 
wakongwe kama hawa watulie tu,Nature mbn amefanikiwa xn kupitia music,angestaafu tuu,sasa kiki kamahz c haibu kwa mtu km yeye
 
Kila zama na zama zake nyimbo zake na staili yake zilishapita asome soko linataka nn,
 
Mziki umebadilika sana, awe tu mbunifu kwani kazi nzuri ni nzuri tu.
 
Kwa jinsi wasanii wakongwe wa Tz walivyo na mtazamo hasi kwa wenzao wa sasa, nauona ugumu wa wasanii wasasa kufanya alichofanya Nick minaj kwa Lauryn Hilly.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…