Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,319
Wakati tunaulizana wenyewe kwa wenyewe ilikuwaje Kamati ya Ushindi inayoongozwa na wanasiasa wa soka ikaahidi Wachezaji wa Stars fedha ambayo hawakuwa nayo, ningependa tujadili nafasi yetu katika Soka la kimataifa.
Kwa kitambo kidogo tumekuwa na changamoto ya idadi ndogo ya wachezaji wanaocheza kwenye Ligi kubwa na zenye ushindani.
Wachezaji wa Tanzania wamekuwa ni maarufu wa mitaani kwa muda mrefu, na wakimaliza zama zao za soka huishia kufanya shughuli za Watanzania wengine kama vile biashara za kawaida kabisa.
Wachache ambao walishawahi kutoka nje hawakufika anga ambazo tunaziota kila siku, na wengine wakafanya kichekesho cha kurejea nchini kwa kukimbia kodi, kama Haruna Moshi Shaaban.
Kwa sasa tunao wachache wanaotuwakilisha kwenye ligi kuu za hapa Afrika, na makumi wengine ambao wanachezea mataifa ya watu kama raia wao, wakati ni watoto wetu, mfano Ali Hafif wa Qatar.
Mpira umekuwa na pande mbili, wachezaji na uongozi, na kila mmoja ana anayotakiwa kuyafanya ili tusonge mbele, na wachezaji kwa nafasi na uwezo wao wamejitahidi pakubwa, tatizo liko upande wa pili.
Wakati tunahamasishana kutoa wachezaji kwenda kwenye Ligi za Kimataifa, wachache tulio nao huko ama TFF wamewapuuza, na wadau wengine hawana habari nao kabisa.
Timu ya ZESCo anayochezea Juma Liuzio ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Zambia, na hii ni timu ya Shirika la Umeme na uchumi wake una nafuu kidogo.
Liuzio sio mchezaji muhimu kuliko wengine Zesco, lakini hakija wanamhitaji na ndio maana bado yupo nao na anacheza idadi ya mechi za kutosha kumweka fiti.
Ni zaidi ya mwaka sasa tangu Juma ajiunge na vigogo hao wa Zambia, lakini uwepo wake ni kama usiofahamika sana miongoni mwa Watanzania akiwa mchezaji wa Ligi Kuu ya nje anayeitwa mara chache mno kwenye kikosi cha Taifa.
Hadi anaondoka Mtibwa Sukari, mwezi Julai mwaka 2014, alikuwa mmoja kati ya washambuliaji mahiri wa timu hiyo, akiwa na kumbukumbu ya kufukuzana bega kwa bega na amisi Tambwe wa Simba kwenye ufungaji bora wa Ligi Kuu.
Pengine Juma ana bahati mbaya kuwa alikwenda nje akitokea timu isiyopewa uzito sana na karibu kila anayehusika nchi hii, Mtibwa. Wapo wachezaji ambao kuitwa kwao timu ya Taifa kulikuja baada tu ya kusajiliwa na Yanga, mfano Deus Kaseke na Malimi Busungu.
Kwa kuwa tabia ya kuita timu ya Taifa kwa misingi ya timu anayotoka mchezaji ni komavu, sina wasiwasi sana kuwa Juma anahujumiwa kwa kuwa hatokei kwenye timu tatu vipenzi, Azam, Simba na Yanga.
Nina kumbukumbu za kutosha wakati Henry Joseph anajiunga na Kongsvinger IL Toppfotball ya Norway, magazeti, redio, na viongozi wa soka nchini walihamishia mahaba yao kwa timu hiyo na mchezaji wao, na walifurahi nayo ilipopanda daraja kwenda Ligi Kuu.
Sana hazikuishia hapo, wakati Haruna Moshi anaenda Gelfe ya Sweden, kucheza mechi tano pekee na kisha kurudi nchini kimazabe, bado watu walikuwa pamoja nae, wakimfuatilia na kupata mapichapicha yake, lakini sio Juma au mwingine ambaye hatokei kwenye malisho mazuri.
Juma ndie anayeonekana kwa macho, kwa kuwa ni mchezaji mkubwa, lakini wapo wachezaji ambao wanacheza nje, hawatazamwi wala hakuna anayejali wamefanyaje huko, hata washabiki.
Zamani kidogo niliwahi kuonana na mchezaji mmoja wa Ligi Kuu (jina nalihifadhi) Kituo cha Mabasi Ubungo, akiwa na malapa akiomba nauli ya kwenda Chalinze kwa rafiki yake, kwa kuwa TFF hawajampa kibali cha uhamisho wa kimataifa (ITC) ili akacheze Afrika Kusini, na fedha zimemuishia hadi akauza viatu.
Jamaa hakuishia kulialia, akaniambia mipango yake ya kwenda Rwanda, huko atapata ITC kirahisi, atachukua uraia na hata timu ya taifa hakutakuwa na mizengwe kama hapa, akaniambia kuwa na jina la Kinyarwanda ameshapata (akanionesha kitambulisho chake cha Ligi Kuu Bara).
Hakuna asiyejua ukarimu wa Rwanda kwa wageni ambao wamechoka na nchi zao, si mpira tu, hata siasa zao huwa zinakaribisha wageni kuzitumikia kwa faida.
Ninyi sio wageni na visa vya shirikisho letu kuwasumbua wachezaji na vibali vya uhamisho, watu kama hawa wanapotakiwa wafuatilie maendeleo ya wachezaji walioko nje, ambao hapo mwanzo waliwakwamisha, tusitarajie tofauti kubwa.
Kuna wakati tulijitia - tia kumfuatilia Adam Nditi aliyekuwa akicheza timu ya vijana ya Chelsea ya Uingereza, kwa kuwa wazo lile halikuasisiwa na TFF, au kilabu kimoja kipendwa, mpango ule ukafa.
Sisi tunataka maendeleo ya Soka, lakini rasilimali zilizopo hatuzijui, hatuzithamini na hatuna mpango nazo... Huku kila mmoja akilazimisha kwa namna yake Soka la Bongo liendeshwaje!
Chanzo: Mwananchi