Juma "Mensah" Pondamali Alivyoiwezesha Tanzania Kucheza Kombe la Afrika Nigeria 1980

Juma "Mensah" Pondamali Alivyoiwezesha Tanzania Kucheza Kombe la Afrika Nigeria 1980

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
JUMA "MENSAH" PONDAMALI ALIVYOIPA USHINDI TANZANIA KUFUZU KOMBE LA AFRIKA DAG HAMMARSKJOLD STADIUM NDOLA ZAMBIA 1980

Sote tulikuwa kimya tukimsikiliza Juma Pondamali akituhadithia kwanza jinsi Rais Kaunda akiwa na kitambaa chake mkononi alivyokuwa akiwamahamasisha Wazambia walioujaza Uwanja wa Dag Hammarskjold kuishangilia timu yao "Kaunda Eleven."

Timu ya Zambia iliwaandama Taifa Stars toka wanatua Uwanja wa Ndege kwa kuwasubiri wakiwa wamevaa "track suit," zao nadhifu za kupendeza.

Mambo hayakuishia hapo waliwafuata Taifa Stars hadi hotelini kwao na kuwazingira wakati wa chakula cha mchana kula na wao pamoja ingawa wao hawakuwa wanakaa hoteli hiyo.

Mahadhi ikabidi atafute mbinu ya kuwatisha Kaunda Eleven kwa kujifanya yeye "Afisa wa Benchi la Ufundi," katumwa kuwamwagia "vitu."

Lakini haya yalikuwa tisa.

Kumi mambo yalikuwa uwanjani.

Taifa Stars walielemewa sana.

Juma "Mensah" alizuia michomo ya magoli dhahiri kiasi mapumziko hakutaka kurejea uwanjani na bahati mbaya kwake golikipa wa pili Mahadhi na yeye akakataa kuingia uwanjani.

 
Back
Top Bottom