Juma Mgunda we ni kocha mzuri wa mpira ila....

Pesanyingi

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2023
Posts
1,157
Reaction score
1,983
Kwako Juma Mgunda. We ni kocha mzawa na umejitengenezea heshima yako katika soka la Tanzania kwa siku za karibuni.

Ushauri wangu kwako usikubali kuwa kocha wa deiwaka kama Simba wanavyokutumia Sasa. Uwezo wa kuifundisha Simba unao kwani tayari ulishaonesha hilo, ila timu hawataki kukupa hadi mambo yao yakishabuma we ndiyo wanakuona unawafaa.

Jitenge na club ya Simba kwakuangalia mustakabali wako. Siku Simba inapopita katika changamoto kama Sasa na kupoteza uelekeo na wewe inaweza kuchafua ubora wako hata timu zenye nia ya kweli kukupa kazi zikaona umeshuka au hauna kiwango.

Ni bora ukafundishe hata Kibondo FC kuliko kuwa kiraka hapo clabuni Simba.
 
Mgunda hawezi ifundisha timu yeyote kubwa tofauti na Simba, labda KMC, Namungo, Ndanda n.k
hakuna klabu iliyo serious itampa mkataba wa miaka miwili Mgunda

Simba yenyewe haiwezi, labda akae kwa muda.
 
Maokoto unayajua wewe

Zaidi ya Azam na Yanga hakuna club ya kumlipa milioni saba anazolipwa Simba
 
Jamaa umeandika thread ila unamjua vizuri Mgunda... au ni mihemko tu, unaujua mpira. Unaijua vzuri ligi yetu ya Tanzania.
 
Tatizo la makocha kama Mgunda ni mashabiki wa timu zingine hachelewi kuwauza mnapocheza na timu yake anayo ipenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…