Juma Mpogo na Jack Simela tangu waondoke, mnanda nao umepotea

junky

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2017
Posts
413
Reaction score
978
Tokea hawa waimbaji mashuhuri wa mnanda wafariki hakika mnanda nao umeenda zake ,ladha na utamu wa mnanda umepotea ..Wameondoka mapema Sana ikiwa fani bado inawahitaji.

1.Juma Mpogo lupozi "seven survivor"

2.Jack Simela "Jagwa "

 
Kuna wakati utafika Bongo sanaa itapotea kabisaa.
 
Mola Ndo Ajuaye.

R.I.P Jack Simela... Your good music lives forever!

-Kaveli-
 
natafuta wimbo wa baba asha sungu sungu
 
Kuna ule wimbo unaelezea "narudi nyumbani Chalinze".

Nishautafuta sana bila mafanikio.

-Kaveli-
 
Miziki ya wasela na wahuni hii

Singeli imeharibu soko lao naona

Ova
 
"Narudi nyumbani Chalinze" huu wimbo waliimba kundi gani? Nautafuta sana.

-Kaveli-
 
Heshima na upole wako Asha ulinifanya nikaandika barua, nia na madhumuni yangu Asha, nilitaka nikuoe
Ashaaaaaaaaa

Nyie mnanda hautatokea...

mmesahau Chaukucha kucha Kondakta kaja juu
 
Heshima na upole wako Asha ulinifanya nikaandika barua, nia na madhumuni yangu Asha, nilitaka nikuoe
Ashaaaaaaaaa

Nyie mnanda hautatokea...

mmesahau Chaukucha kucha Kondakta kaja juu

"Kondakta kaja juu anasema haiwezekani, limeruhusiwa jeshi la polisi"

Hahahaa mnanda mtamu sana walai.

Mkuu kuna ile 'Mama Ashura' by Jagwa... ni noma hiyo ngoma.

-Kaveli-
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…