Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani


Mjomba maelezo yako ni kielelezo tosha kwamba Juma Njemba alikuwa anatisha .
Maana ana karibia miaka 20 chini ya ardhi lakini bado wamuogopa ..

Nilichoongea sijaongeza chumvi hata kidogo..Juma Njemba hakuwa MTU wa mchezomchezo ..Alikuwa hatari sana na suala la kuoa ameoa wanawake wengi sana wengi walikuwa wanaenda kilingeni kwake kama wateja na alikuwa akivutiwa nao tu basi wanakuwa wakeze..

Mke wa kwanza wa Juma Njemba ninae mfahamu Mimi aliitwa " Mkamiti Mwanalugondo" bibi wa kinyamwezi kutoka Urambo Tabora ambae na yeye alikuwa fundi kama mumewe ..Huyu alifariki akiwa mkoani Mwanza mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili.. Huyu Mwanalugondo alikuwa anatoka kwenye familia ya kichawi pia...Yeye na babu yangu kizaa baba angu walizaliwa kijiji kimoja na mwaka mmoja 1918 ambao ndio mwaka aliozaliwa Juma Njemba ..

Alikuwa na wanawake wa Kirundi kibao, wanawake wa kiarabu ndio usiseme ..Mfano pale Nzega na Tabora mjini ana watoto wengi tu ambao amezaa na wanawake wa kiarabu.

Halafu jua kuwa Juma Njemba ni kikongwe rika la kina bibi fisi wa Mwanza..

Wanafunzi wake wengi ni watu wazima kwa sasa na wengi wao wamechuja kabisa wamebakiza uchawi tu wa kuumiza watu ..Nawajua wengi tu akina Athumani Balichako na Ali Zaidi hawa wapo kanda ya ziwa lakini hawana lolote kwa sasa ...
 
Hakufa wapo wawili sio mkoba Bali elimu ya kitabu na kuburi tu. Hats wachungaji wapo wenye nguvu na uwezo wa Mungu katika kuitikiwa maombi
Labda kama unataka kuibia watu mzee
 

Siamini aisee
 
Kaka Mimi naomba kujua kifo chake alikufajee?
 
mimi niluwahi kwenda kwa huyo mzee lakini niliogopa kumalizia zindiko la milango saba ya ziwa tanganyika, nikaondoka kwa kutoroka tukiwa mlango wa tatu , nadhani umenikumbusha mbali mno wala hujakosea kitu.
Loh ulikuwa unataka nini vivo?
 
Labda kama unataka kuibia watu mzee
Kuibia watu kivipi inamaana alichokiandika kuhusu wakeze majina yao na watoto na Mahala walipo watoto wake ni uongo??
Ila
Ukweli ni yeye kuwa na wake mia 2 na kuua watu??

Tunasubiri muendeee kutiririka tupate kumjua Mzee Juma Njemba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…