Juma Nkamia, kauli yako kuhusu Mecky Mexime haijanifurahisha

Musharaf

Senior Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
183
Reaction score
66
Akihojiwa katika kipindi cha Jambo (TBC 1) cha leo tarehe 5/6/'15, waziri mwenye dhamana ya michezo nchini ametoa maoni yake kuhusu kocha msaidizi wa timu ya taifa, Taifa Stars- Mecy Maxime kuwa hafai kwa sababu bado mdogo, na kama angeulizwa yeye kuhusu kocha msaidizi angependekeza mtu kama Abdalah Kibadeni.

Kwangu mimi, naona hoja yake haina mashiko kwa kuwa kazi ya ukocha si ya kubeba matofali, bali ni ujuzi. Wapo kina Pep Guardiola ni vijana na wanafanya vizuri. Hata hao aliowataja yeye kuwa wanafaa wamekuwa makocha siku nyingi lakini sioni kigezo cha kuwapa timu ya taifa kwa kuwa hakuna jipya walilowahi kufanya hadi kustahili nafasi hiyo.

Namshauri waziri aache kufanya mambo kwa mazoea.
 
Hajitambui huyo Nkamia ndio maana aliponea chupuchupu kupigwa jimboni kwa kauli chafu
 
Tatizo la Mkamia ni usimba na yanga hadi kwenye masuala ya kitaifa.Lingine ni watu wajinga kupewa dhamana kubwa ya taifa.Hapa kosa si lake bali kwa yule aliyemteua.
 
Ni mzigo hasa kataika baraza la mawaziri, lipi la maana alilofanya? Ukiona mtu anatoa matusi hadharani jua tu akili yake ina mushkel, kama uzee ndio sifa ya kufundisha na ujuzi kwa nini uzee usiwe kigezo cha kupewea kazi ya ualimu wa shule zetu?
 
Nkamia hana uwezo kabisa,amesoma kwa kodi za watanzania hasara tumepata. huwa simsikilizi kabisa akionekana ktk tv huwa nabadilisha chaneli..
 
ingawa huyu jamaa simfagilii ukweli mecky mexime hafai ila hata kibadeni hafai cha muhimu kocha wa timu ya taifa aachwe achague msaidizi anayemtaka,Tanzania kila kitu tunakichukulia rahisi rahisi
 
Kama inshu ni Ujuzi;
Abdalah King Kibadeni ni kocha ambae yupo kwenye gemu tangu kitambo. Ameanza kufundisha soka mwishoni mwa miaka ya 80 ambapo Maxime alikua chekechea. Katika miaka yote hiyo amefundisha timu za vijana, timu za ligi kuu, timu ya taifa.. na pia anamiliki akademi yake mwenyewe.

Kama inshu ni Mafanikio;
Abdalah King Kibaden Mputa ni kocha pekee mzawa toka Tanzania mwenye mafanikio makubwa katika michuano ya Africa.. kwani aliifikisha fainali Simba Sc katika kombe la Shirikisho mwaka 1993. Amechukua kombe la chalenji jijini mwanza akiwa na timu ya taifa. Hapo sijataja idadi ya makombe ya ligi kuu, klabu bingwa africa mashariki aliyochukua.

Sasa kwa CV hii jamani, unapataje uthubutu wa kumlinganisha huyu "gwiji" Abdalah King Kibaden Mputa na "mwanae" Maxime??? Inabidi ujitoe akili ili ufanye mlinganyo huo.

Ni vyema Maxime alivyopata "shavu" la kuonja ukocha wa timu ya taifa.. ila ni kosa la jinai kusema Maxime ni bora kuliko Abdalah King Kibaden Mputa.
 
Huyu nkamia hata huo uwaziri cjui alipewaje au sijui ni uswahiba, huyu jamaa ana maneno kuntu sana, tena amuombe msamaha maxime kwa kumdharau kijana mdogo aliyeonyesha anaweza na amepambana na makocha wakubwa na wazoefu, kwanza yy kaifanyia nn nafasi aliyopewa:what:
 
Kauli namna hiyo inaweza kuwa sahihi kwa Nkamia kama mwananchi yeyote alivyo na haki ya kutoa maoni yake. Lakini haiwezi kuwa sahihi kwa Nkamia Kama Naibu Waziri wa Michezo, kwa sababu anaisemea Serikali ambayo haipaswi kupendelea raia mmoja na kumchukia mwengine. Ila hofu yangu ni kuwa Nkamia alitoa kauli ile kama shabiki wa Simba. Hapo atakuwa amekitumia chombo cha habari cha umma sambamba na kiongozi wa umma (yeye mwenyewe) kwa masalahi ya Simba. Sio haki.
 
Akihojiwa katika kipindi cha Jambo (TBC 1) cha leo tarehe 5/6/'15, waziri mwenye dhamana ya michezo nchini ametoa maoni yake kuhusu kocha msaidizi wa timu ya taifa, Taifa Stars- Mecy Maxime kuwa hafai kwa sababu bado mdogo, na kama angeulizwa yeye kuhusu kocha msaidizi angependekeza mtu kama Abdalah Kibadeni.

Kwangu mimi, naona hoja yake haina mashiko kwa kuwa kazi ya ukocha si ya kubeba matofali, bali ni ujuzi. Wapo kina Pep Guardiola ni vijana na wanafanya vizuri. Hata hao aliowataja yeye kuwa wanafaa wamekuwa makocha siku nyingi lakini sioni kigezo cha kuwapa timu ya taifa kwa kuwa hakuna jipya walilowahi kufanya hadi kustahili nafasi hiyo.

Namshauri waziri aache kufanya mambo kwa mazoea.

Huyo jamaa mpuuzi sana. Kamtaja Kibaden kwa kuwa anajua ni Simba damu kama yeye. Unaweza kumtoa mtu shamba kumleta mjini lakini huwezi kuutoa ushamba wake. Harafu huyo ni Naibu Waziri!
 
Hivi Juma Nkamia hajatangaza nia ya kugombea urahisi? urais hauwezi maana hata huo ubunge anachechemea tu.
 
Bunduki ndio muokozi wa taifa hili maana bunduki itaua wapumbavu wengi wanaochelewesha maendeleo kwenye taifa hili!!!!
 
ingawa huyu jamaa simfagilii ukweli mecky mexime hafai ila hata kibadeni hafai cha muhimu kocha wa timu ya taifa aachwe achague msaidizi anayemtaka,Tanzania kila kitu tunakichukulia rahisi rahisi

Mecky Mexime amekuwa kapteni kipindi ambacho Taifa Star imekuwa na mafanikio japo si ya vikombe. Ni logic kuwa katika benchi la ufundi. Kuna ambacho a naweza kuchangia katika timu kuliko ambayo wazee kama King Kibaden, Mkwasa, Au wazee wengine ambao waliwahi pewa timu bila mafanikio yoyote ya maana.
 
Na yeye nkamia ni mdogo asingekuwa naibu waziri.aende zake huko mm sizungumzi na mbwa na zungumza na mwenye mbwa ahaha
 
Kama inshu ni Ujuzi;
Abdalah King Kibadeni ni kocha ambae yupo kwenye gemu tangu kitambo. Ameanza kufundisha soka mwishoni mwa miaka ya 80 ambapo Maxime alikua chekechea. Katika miaka yote hiyo amefundisha timu za vijana, timu za ligi kuu, timu ya taifa.. na pia anamiliki akademi yake mwenyewe.

Kama inshu ni Mafanikio;
Abdalah King Kibaden Mputa ni kocha pekee mzawa toka Tanzania mwenye mafanikio makubwa katika michuano ya Africa.. kwani aliifikisha fainali Simba Sc katika kombe la Shirikisho mwaka 1993. Amechukua kombe la chalenji jijini mwanza akiwa na timu ya taifa. Hapo sijataja idadi ya makombe ya ligi kuu, klabu bingwa africa mashariki aliyochukua.

Sasa kwa CV hii jamani, unapataje uthubutu wa kumlinganisha huyu "gwiji" Abdalah King Kibaden Mputa na "mwanae" Maxime??? Inabidi ujitoe akili ili ufanye mlinganyo huo.

Ni vyema Maxime alivyopata "shavu" la kuonja ukocha wa timu ya taifa.. ila ni kosa la jinai kusema Maxime ni bora kuliko Abdalah King Kibaden Mputa.

Maxime ndo kwanza anaanza Tumpe muda sawa na Kibaden then tujaji.
 
Mkuu hapo umenena. Mexime ni kocha bomba sana.. tunatakiwa tumpe mda afanye kazi, na si kuanza kumlinganisha na "magwiji".
 
Back
Top Bottom