Juma Nyoso unafanya bangi ionekane walioiharamisha walikuwa sahihi

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Kwa nyakati tofauti Mbunge wa Kahama Mh Kishimba na Mbunge wa Geita vijijini Mh Joseph Msukuma waliwahi kuomba bangi ihalalishwe kama zào la Biashara ikilimwa kama dawa.

Lakini kitendo ulichofanya Leo Juma Nyoso kwenye Mechi ambayo timu yako ilishaichukua na kuelekea kushinda, ghafla katika mazingira yasiyohatarisha goli lako unahamisha mpira vizuri na ghafla unamkanyaga mgongoni Kwa makusudi Kipre Junior. Hii bangi uliyotumia Leo ungetuelekeza ulikoinunua ili ndiyo ipigwe marufuku nyingine ihalalishwe.
 
Nyosso bado anacheza mpira mpk leo?
 

Watumiaji ndo wanafanya bangi idharaurike
 
Hii bangi uliyotunia Leo ungetuelekeza ulikoinunua ili ndiyo ipigwe marufuku nyingine ihalalishwe.[emoji23]
 
Hii michezo kwa hapa nchini kuna wachambuzi wa mchongo wanaita "kugongana" ili wahalalishe maamuzi mabovu ya waamuzi waliohongwa.

Kimataifa timu nyingi za hapa kwetu haziwezi kupenya kwani wanasifiwa kwa huu upuuzi.

Acheni watu wacheze mpira kwa uwezo wao sio kuwatishia kuwaumiza.Waamuzi mwendelee kuwaadhibu wachezaji kama hawa ili heshima ya mpira irudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…