KWELI Juma Raibu Meya aliyevuliwa Madaraka Moshi akanusha madai ya kung'oa miundombinu aliyoiweka alipokuwa madarakani

KWELI Juma Raibu Meya aliyevuliwa Madaraka Moshi akanusha madai ya kung'oa miundombinu aliyoiweka alipokuwa madarakani

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia kwenye Jumatatu hii ya Pasaka , Kwamba Mheshimiwa Juma Raibu aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro , kabla ya kung'olewa hivi karibuni , ameanza kampeni kabambe ya kuondoa miundo mbinu yote aliyojitolea akiwa madarakani .

Wakati wa madaraka yake alisaidia kutengeneza miundo mbinu ya maji kwenye uwanja wa Mandela uliopo Kata ya Pasua , ili kusaidia vijana wanaotumia uwanja huo , Sasa baada ya kung'olewa kwenye Umeya naye akaamua Kama Mmbwai basi iwe Mmbwai tu , kang'oa miundo mbinu yote ya maji aliyosaidia .

Zipo Taarifa kwamba anapanga kung'oa mabati yote aliyosaidia kwenye mashule mbalimbali pamoja na Zahanati .
1658126209730.png


Akijibu tuhuma hizo, Juma Raibu amesema: “Siwezi ondoa misaada niliyotoa kwa wananchi ni dhambi kubwa na haina maana yoyote sasa hayo mapipa nitayapeleka wapi!

“Bora nijiuzulu nafasi yangu ya Udiwani na nyingine nilizo nazo ikiwa nitafanya kitendo cha kuondoa miundombinu ya maji na hata yale mapipa niliyotoa kujikinga na UVIKO-19.
 
Back
Top Bottom