Siri yangu
JF-Expert Member
- Jul 22, 2023
- 2,252
- 4,839
Ndio nami nataka nimsikie maana namjua tangu katavi kuwa ni kiazi mbatataUzoefu wake ni kumuua Mdude
Ngoja tusubirie mkuu kile atakiongea mbele ya wababe wa dunia wanaojua kila kituMaskini Tanzania.
Kwa hoja zipi, mara nyingi wanakuwa wasikilizaji/ wasindikizaji tu.
Huyu ana ni mtuhumiwa kwa Mdude na yule dogo wanamuita ChaulaMtuhumiwa No. 2 wa Utekaji na Mauaji ya Mwanaharakati Mdude Nyangali anaenda Geneva kuzungumzia Haki za Binadamu.
Tena ikiwezekana wamzuie hukohuko wamkamate huyu mshenzi atangulizwe ICC.
Hakuna kitu pale, hizo ni promo tu ili tufahamu kwamba jamaa hajaenda bure.Ngoja tusubirie mkuu kile atakiongea mbele ya wababe wa dunia wanaojua kila kitu
Mkuu hiyo mikutano kwa sasa haina tija, mtu anaweza kwenda huko asiulizwe lolote la maana wala kupata nafasi ya kujadili mambo serious. Wengi hukabidhi maoni yao kwa njia ya maandishi, na hakuna mahali anaulizwa maswali magumu. Wangalau ingekuwa mkutano wa nchi na mwenyeji wake, kidogo ndio huwa na maswali serious, sio hayo makongamano. Hata ukiwa kilaza wa kutupwa unaweza kwenda na ukawa na mikutano ya kupasha vyumba joto, bila lolote la maana kujadiliwa.Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, amewasili jijini Geneva, nchini Uswisi, kushiriki Mkutano wa Ngazi ya Juu katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ulioanza Februari 23, 2026.
Katika mkutano huo Mhe. Homera anatarajia kuwasilisha taarifa rasmi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayofafanua hali ya haki za binadamu na hatua mbalimbali ambazo nchi imepiga katika eneo hilo.
Kabla ya kuanza kwa mkutano huo, Dkt. Homera ametembelea Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania zilizopo Geneva kwa ajili ya maandalizi ya mwisho.
Akiwa ofisini hapo, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkuu wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa, Balozi Dkt. Abdallah Possi, pamoja na Naibu Mwakilishi wa Kudumu, Balozi Dkt. Hoyce Temu, ili kuratibu agenda za nchi katika jukwaa hilo la kimataifa.
Ziara hii ina umuhimu wa kipekee katika kuimarisha taswira ya Tanzania kimataifa kupitia ushiriki hai kwenye majadiliano ya haki za binadamu duniani.
Kupitia mazungumzo hayo na wanadiplomasia wetu, Mhe. Waziri amesisitiza dhamira ya serikali katika kuendeleza misingi ya kisheria na utawala bora, huku akihakikisha kuwa mchango wa Tanzania katika Baraza la Haki za Binadamu unaleta tija kwa taifa na jumuiya ya kimataifa.
CHanzo cha habari ITVView attachment 3547638
Naomba niulize tena huku Juma Homera anauwezo wa kujieleza mbele ya hao manguli au ni kwenda kudanganya tena akidhani lile ni kusanyiko la pale dodoma?
Kazi kula hela tuHakuna kitu pale, hizo ni promo tu ili tufahamu kwamba jamaa hajaenda bure.
🤣🤣🤣🤣 sawa mkuuMkuu hiyo mikutano kwa sasa haina tija, mtu anaweza kwenda huko asiulizwe lolote la maana wala kupata nafasi ya kujadili mambo serious. Wengi hukabidhi maoni yao kwa njia ya maandishi, na hakuna mahali anaulizwa maswali magumu. Wangalau ingekuwa mkutano wa nchi na mwenyeji wake, kidogo ndio huwa na maswali serious, sio hayo makongamano. Hata ukiwa kilaza wa kutupwa unaweza kwenda na ukawa na mikutano ya kupasha vyumba joto, bila lolote la maana kujadiliwa.