Jumaa Aweso, Hussein Bashe, Innocent Bashungwa nyota zinang'ara

Jumaa Aweso, Hussein Bashe, Innocent Bashungwa nyota zinang'ara

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
Hawa ni miongoni mwa Mawaziri wachapakazi na muda wote wanaonekana site kutatua changomoto za zinazowakabili wananchi na kusimamamia miradi inayotekelezwa chini ya Wizara zao.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiwa Kigoma alichukua hatua kwa msimamizi wa mradi wa maji ambaye mkataba ulikuwa wa miezi 9 tangu uliposainiwa 2020 lakini amefika Julai 2022 amekuta mradi bado haujakamilika na wananchi wanaendelea kuteseka na shida ya maji.

Aweso akiwa Babati amebaini ufisadi wa Milioni 600 ujenzi wa Ofisi ya Bonde ambayo hakuridhika na kilichofanyika na kuchukua hatua, amefika Karatu ametatua tatizo la wananchi kulipishwa maji kwa gharama kubwa tofauti na maeneo mengine nchini akapiga marufuku jambo hilo.

Haya anayafanya kwa sababu yuko kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na hayuko hapo kulinda wizi unaofanywa na baadhi ya wakandarasi wanaoshirikiana na baadhi ya watendaji wa Serikali,.

Bashe naye ameonekana hadharani kujutia makosa aliyoyafanya bungeni kuhuiana na mfumo mbovu wa usimamizi wa mbolea hasa pale aliposhauriwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina lakini bahati mbaya Bashe alipanic bungeni na kusema Mpina mpotoshaji kuhusiana na usimamizi dhaifu wa sekta ya mbolea.

Lakini Bashe akiwa Kilosa jimboni kwa Profesa Palamagamba Kabudi, alikiri makosa hayo na kuwaomba wananchi kuwa msimu huu wa kilimo makosa hayo hayatajirudia tena na kwamba Serikali itarejesha mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja yaani BPS.

Bashe pia ameweka wazi kuwa Serikali itarejesha utaratibu wa kuweka bei elekezi ya mbolea na Serikali itaweka usimamizi madhubuti wa sekta ya mbolea ili kuondoa uholela uliokuwepo uliosababisha wakulima kuuziwa mbolea hadi kufikia 140,000 kwa mfuko wa kilo 50 jambo lililosababisha wakulima wengi kushindwa kumudu kulima msima uliopita.

Hapa Bashe ameupiga mwingi amewashtukia wale waliokuwa wanamdanganya bungeni kwamba anahujumiwa.

Innocent Bashungwa, Waziri wa TAMISEMI amefanya ziara wilaya za Kilosa Morogoro na Kiteto Manyara na kubaini usimamizi dhaifu wa shughuli za Serikali ikiwemo miradi na kuchukua hatua kwa wahusika wote na kazi hiyo inaendelea maeneo mengine ni wazi waliokuwa wanamuona Bashungwa ni mpole sasa nadhani mtamjua vizuri zaidi.
 
Ndio kazi zao hizo, hakuna cha kung'ara wala nini. Upuuzi mtupu
 
Nani kawahi kusikia hotuba ya Aweso bila kusema
"... Nani kama mama Samia, piga makofi kwa mama Samia..."Kila baada ya dakika tano
Bootlicker
 
Porojo....mwezio ukimwona site ujue anaingiza posho kwa kila siku
 
Bashungwa hamna kitu,Aweso nae mikwara tu hamna kitu labda bashe
 
Huyu Juma awezo ambaye ameshindwa kutatua tatizo la maji buswelu, wilayani Ilemela mkoa wa mwanza.....mwezi wa tatu wananchi hawana maji...mpaka wasoma mita wanaogopa kusoma tena mita, mean while mkoaw a Shinyanga and Tabora maji ni mengi na wako mbioni kuyapeleka Dodoma.

Unaweza kuwaza kikawaida kabisa una kisima kwako unasupply maji kwa majirani wewe na familia yako na kisima chako mnakosa maji.
 
Back
Top Bottom