#COVID19 Jumamosi Hospitali ya Amana hawatoi chanjo ya Covid lakini Aga Khan wanachanja, hii ipoje?

BURUTA

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2015
Posts
631
Reaction score
809
Wiki iliyopita nilijiandikisha online kupata chanjo ya Covid Amana Hosp leo Jmosi Aug 7. Lkn nilipofika pale tuliambiwa leo hawatoi chanjo hadi J'tatu.

Baadaye jamaa alinitonya niende Aga Khan. Nikaenda, sikuchukua dak 15 nikapata chanjo.

Inakuwaje private hospital wanajali zaidi wananchi kuliko govt hospital?

Na hili suala la kujiandikisha online kumbe magumashi tu.
 
Kama umeshachanjwa basi jipongeze,mengiene tuachieni sisi.
 
Institutional Poverty imekomaa sana mizizi ni mirefu mnoo..
 
Vipi sababu za kutozitoa chanjo hawakusema mkuu?

Hakuna aliyekuwa tayari kuongea pale. Walinzi wa geti walinionyesha sehemu wanapochanjia niende nikaulize, nilipoenda hakukuwa na mtu mabenchi tu ya kusubiria na sehemu za kundikisha pasipo wahudumu.

Kiliniuma zaidi ni uhuni wa online registration - aibu tupu.
 
Wiki iliyopita nilijiandikisha online kupata chanjo ya Covid Amana Hosp leo Jmosi Aug 7. Lkn nilipofika pale tuliambiwa leo hawatoi chanjo hadi J'tatu.

Baadaye jamaa alinitonya niende Aga Khan. Nikaenda, sikuchukua dak 15 nikapata chanjo.

Inakuwaje private hospital wanajali zaidi wananchi kuliko govt hospital?

Na hili suala la kujiandikisha online kumbe magumashi tu.
Ipo hivyo hivyo.
 
Pole sana mkuu, ni changamoto sana. Muhimu umeshafanikisha hitaji lako la kupata chanjo.
 
Labda wahudumu walikuwa njiani, na wewe uliwahi..

No hurry in Africa.
 
Muhimbili wanachanja hata jumapili mwisho saa sita mchana
 
Chanjo milioni moja bado tu hazijaisha mpaka leo?

Wabunge 320 X wategemezi wao
Vigogo 500 x wategemezi wao
Jeshi
Afya
Wagonjwa
Wazee

Haiwezekani iwe mpaka leo zoezi linaendelea kwa chanjo hizo milioni, au zimeshakuja nyingine kimya kimya?
 
Tulichanganya na maji ili iwe dozi nyingi, zile dozi 1m jumlisha na maji Lita 1000.
 
Chanjo milioni moja bado tu hazijaisha mpaka leo?

Wabunge 320 X wategemezi wao
Vigogo 500 x wategemezi wao
Jeshi
Afya
Wagonjwa
Wazee

Haiwezekani iwe mpaka leo zoezi linaendelea kwa chanjo hizo milioni, au zimeshakuja nyingine kimya kimya?
Kichupa kimoja wanachoma watu 5..
 
Kichupa kimoja wanachoma watu 5..
Kwahiyo waliposema wamepokea chanjo milioni 1, walikuwa na maana ya kuwa wanategemea kuchanja watu milioni 5 au milioni 1?

Na hizi ni zile kwa hisani ya mabeberu sio? Tumeshaagiza nyingine kwa pesa zetu? Najua alisema ameagiza ndege ya mizigo, Dar pekee si ina wakazi takribani milioni 6?

Kama tuko serious kweli, ama tupime wote au tuagize za almost wote.
 
Wewe unahitaji PhD kujua ya kwamba siku za weekend wafanyakazi wa serikali huwa hawafanyi kazi?

Lakini kwa nini waliruhusu kuregister watu online for Saturdays? Tuanzie hapo mkuu.
 
Wiki iliyopita nilijiandikisha online kupata chanjo ya Covid Amana Hosp leo Jmosi Aug 7. Lkn nilipofika pale tuliambiwa leo hawatoi chanjo hadi J'tatu.

Baadaye jamaa alinitonya niende Aga Khan. Nikaenda, sikuchukua dak 15 nikapata chanjo.

Inakuwaje private hospital wanajali zaidi wananchi kuliko govt hospital?

Na hili suala la kujiandikisha online kumbe magumashi tu.
Mkuu ni dozi ngapi inatakiwa kukamilisha chanjo kamili ?

Na muda gani unapita tangu dozi ya kwanza na inayofuata ?
 
Back
Top Bottom