MJ nakusifu sana kuwa mtu wa harakati za Watanzania kwa kweli umeonyesha upendo wa nchi kwa vitendo na unahitaji kusifiwa na Watanzania hasa vijana wa kitanzania. Nilikuwa nashauri mambo machache kuhusu chombo chako cha habari .
1. Ningeomba uwahusishe Watanzania walioko marekani zaidi. Kuna Watanzania wengi duani kote wanataka kutusikia Watanzania tulio marekani tuna mawazo gani na chombo chako kingeweza kutumika mfano. unaweza kuweka topic na tukatoa mawazo kwa simu au tuka post video kama youtube halafu utataarifu kwamba mawazo yao yatarushwa hewani.
2. Anzisha section ya mahojiano na mipango ya kufanya umoja wa watanzania Amerika (mpaka canada) na uruhusu watu wa post plan zao za umoja wa Watanzania Marekani na watu wachangie.
3.Kuna Watanzania wengi hapa Marekani wamefanikiwa kufanya kazi sehemu nyeti mfano kuna Mtanzania ambaye ni Vice president kwenye Microsoft, na mwingine yuko kwenye Bill gates foundation, wengine ni ma dean na vice president wa vyuo mbalimbali. Ningeomba uwatafute hawa watu kwa mahojiano kwani maendeleo ya nchi yetu yatatoka kila mahali.
Kwa ufupi MJ nilikuwa naomba uwahusishe Watanzania wa hapa kwani tuna talent nyingi sana ambazo hatuzitumii vilevile maisha siyo siasa pekee. Nitafurahi kama utachukua mawazo yangu MJ. THANKS