Jumanne Sagini atoa ufafanuzi sakata la waendesha bajaji Mbeya

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Jumanne Sagini, ametoa ufafanuzi kuhusu vurugu zilizojitokeza kwa baadhi ya waendesha bajaji mkoani humo kukaidi maagizo ya Serikali na kuamua kujichukulia sheria mkononi kwa kuanzisha vurugu.

Akizungumza katika TBC Aridhio leo Oktoba 20, 2026, Sagini amesema mnamo Oktoba 12 mwaka huu, Uongozi wa Mkoa huo uliketi kikao cha pamoja na madereva wa daladala, bajaji, bodaboda pamoja na wadau wengine wa usafiri kwa ajili ya kuwapanga katika maeneo maalumu ili kupunguza msongamano katikati ya barabara kuu ya TANZAM.

Amesema baada ya maamuzi hayo, wapo madereva walioonyesha kutoridhishwa na maamuzi hayo hali iliyopelekea kuamua kujichukulia sheria mkononi kwa kuwashambulia madereva wa bajaji ambao walifuata maagizo yaliyotolewa.

Hata hivyo, Sagini amesema Jeshi la Polisi mkoani humo limeimarisha ulinzi katika maeneo yaliyokuwa na vurugu ambapo kumekuwa na hali ya usalama hadi sasa huku akisisitiza yupo tayari kuwasikiliza madereva hao wenye malalamiko kwa kufuata utaratibu.
Chanzo : Tbc Digital


Your browser is not able to display this video.
 
dalili ya El Nino je nini? maana hadi leo haijaja na walisema kuanzia mwezi wa 10
Mjomba, dalili yake ni ile ya kutumia bilioni 700+ kufukua mitaro na makaravati kadhaa kwenye baadhi ya maeneo kote nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…