Jumia ya Sasa mnaielewaje katika kutimiza haja ya mteja?

Mr Sanguine

Member
Joined
Dec 29, 2017
Posts
77
Reaction score
44
Baada ya kupata mwanga kuhusiana na Epson printer, Sasa ni wakati wa kuagiza mzigo unifikie.

Kwa mujibu wa Jumia, Printer waliyo nayo ni mpya kabisa yenye Bottles 4 zenye wino wa kutosha ku-print kurasa 13,000 in black na 6,500 in colour.

Zaidi, wanakuongeza Two black bottles kama akiba.

Kwa kuangalia hili, nimetokwa na mate ya hamu ya kutaka kuinunua toka kwao hasa baada ya kupata elimu hapa kuhusiana na Printer hiyo.

Sasa kwa wale mliowahi kuagiza kitu na mnaoagiza mpaka sasa naomba mnipe mchaganuo wa iwapo mzigo wangu utafika mikoani bila shida baada ya kulipia Ela hiyo au mna Shaka yoyote.

Kinachotatanisha ni kuwa Jumia sasa haina option ya PAY AFTER DELIVERY ambayo ingenipa ujasiri wa kununua kiulaini. Ukiangalia wingi wa matapeli na maisha yalivyo magumu, napata ukakasi kidogo kulipia mzigo huo.

Hivyo, WAKUU, NALILETA JAMBO HILI KWENU MNISAIDIE.
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
[emoji121]
MKUU,

USIJISUMBUE HUKO,

HIZO PRINTER ZIPO NYINGI KARIAKOO,
NA UTAZIPATA BILA USUMBUFU WOWOTE!!!
 
[emoji121]
MKUU,

USIJISUMBUE HUKO,

HIZO PRINTER ZIPO NYINGI KARIAKOO,
NA UTAZIPATA BILA USUMBUFU WOWOTE!!!
Mkuu mimi nimenunua printer frani jumia bei ilikua cheee kabisa jumla na shipping fee nilipoenda kuulizia madukani nikakuta bei ipo juu zaidi ya 40%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…