Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Wakuu salaam,
Kadri siku zinavyozidi kwenda Jumuiya ya Aftika Mashiriki inazidi kukua kwa kuongezeka nchi Mwananchama.
Kihistoria Jumuiya ya Afrika Mashariki ilizaliwa mnamo mwaka 1967 ikiwa na nchi tatu. Soma: kama inavyooneshwa katika ramani hapa chini.
Picha: Ramani ikionesha nchi tatu Waasisi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 2000
Licha ya nchi hizi kupitia changamoto kadhaa ikiwamo kuvinjika kwa Jumuiya hii mnamo mwaka 1977 kwa sababu mbalimbali Soma: Wakati EAC inavunjika, nani alipata nini? na kufufuliwa upya mnamo Julai 7, 2000. Tangu kufufuliwa upya nchi tatu (Tanzania, Kenya na Uganda) zimeendelea kuwa nchi mama za Jumuiya hii mpaka Leo.
Mnamo mwaka Tarehe 18/06/2007 Jumuiya ya Afrika Mashariki ikatanuka kufuatia kuongezeka kwa nchi mbili Rwanda na Burudi katika Jumuiya hii. Soma: KAMPALA: Rwanda na Burundi zajiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki | DW | 18.06.2007 Tazama kielelezo Cha ramani hapa chini.
Picha: Ramani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya Rwanda na Burundi kuwa Mwanachama
Zaidi ya hayo, mnamo tarehe 15/04/2016 nchi ya Sudani Kusini ilikubaliwa kuwa Mwanachama mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo kupeleka Jumuiya hii kutanuka na kuwa na Jumla ya mwanachama 6. Soma Sudan Kusini yajiunga rasmi na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Rais Magufuli ashuhudia utiaji wa saini Tazama Katika Ramani hapa chini:
Picha: Ramani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya Sudani Kusini kuwa Mwanachama mpya
Aidha mnamo mwaka Desemba 22, 2022 Jumuiya ya Afrika Mashariki ikatanuka zaidi baada ya viongozi wake kuipokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa Mwanachama mpya wa Jumuiya hii na kupeleka Jumuiya kufikisha nchi Saba. soma: DR-Congo yawa mwanachama wa EAC Tazama ramani hapa chini:
Picha: Ramani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya DR Congo kuwa Mwanachama mpya
Mjadala: Suala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendelea kukua imekuwa jambo bora na la msingi sana katika kuimarasha siasa, uchumi na Utamaduni wa nchi Wanachama wa Jumuiya hii.
Zaidi ya hayo kukua kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kunamaanisha kuongezeka kwa nafasi ya fursa mbalimbali kiuchumi, Kisiasa na kijamii.
Swali langu: Je, Watanzania kama Wanachi na Tanzania kama taifa (serikali) inafanya jitihada gani katika kuhakikisha tunanufaika na ukuaji wa Jumuiya hii? Je, kukuwa kwa Jumuiya hii kumekuwa kunanufaisha nchi Wanachama kwa namna yoyote? Je, kuna nchi inanufaika zaidi ya nyingine?