Dr Msaka Habari
Member
- Apr 9, 2022
- 66
- 32
Na. Mwandishi Wetu, Dar
Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri kimeomboleza kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein (AS) aliyeuawa kikatili huko mji wa Kerbala nchini Iraq na Jeshi la Yazid.
Ambapo umeunga mkono uchangiaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama , Kampeni ya Kuhamasisha Uchangiaji Damu.
Akizungumzia juu ya Imam Hussein Shabani Ally ameziomba taasisi na jumuiya nyingine kuiga mfano wa Jumuiya hiyo kwa kujitoa kuchangia damu ili kusaidia wagonjwa wenye mahitaji.
“Tunaamini katika Imam Hussein kiongozi aliyejitoa kuwapigania wanyonge tutaendelea kupinga uonevu wowote kwa kuhimiza amani na utulivu kwa waislamu wote,” amesema Ally.
Aliongeza kusema kuwa uchangiaji uliofanywa na taasisi hiyo umeonyesha ni kwa jinsi wanavyojitolea kusaidia watu wenye mahitaji ya damu bila kujali itikadi rangi na dini.
Maandamano yamekuwa yakiudhuriwa na wabunge , vingozi mbali mbali ambapo kwa siku za nyuma Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki (CCM), Ibrahim Raza alionekana mara kwa mara kuweza kuhudhuria.
Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithnasheri Alhaj Azim Dewji amesema wameweza kutoa huduma ya kambi ya macho hivyo wenyechangamoto wafike kujua afya zao katika viwannja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam ambapo mahadhimisho hayo yanafanyika kwa siku tatu.
Naye Kiongozi wa Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheri Tanzania Sheikh Hemed Jalala amekuwa akiwaasa waamini wa dini zote kuvumiliana na kuendeleza amani na umoja uliopo huku akiwasisitiza kuheshimiana ili kudumisha utulivu.