Jumuiya ya Madola 2022: Tanzania yajihakikishia medali, Bondia aingia nusu fainali

Jumuiya ya Madola 2022: Tanzania yajihakikishia medali, Bondia aingia nusu fainali

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Bondia Yusuf Changalawe amemtoa kwa TKO, Arthur Lingelier kutoka Visiwa vya St Lucia na kutinga Nusu Fainali katika michezo ya Jumuiya ya Madola Jijini Birmingham Nchini Uingereza.

Kutokana na matokeo hayo, Tanzania imepata uhakika wa medali katika michezo hiyo.

Kabla ya hapo, Changalawe alifanikiwa kuingia Robo Fainali kwa ushindi wa pointi dhidi ya Curlin Richardson kutoka Visiwa vya Anguila.
 
Daah! tena mashindano yanafanyikiwa Birmingham...?
Gwajima asingeleta siasa kwenye utekelezaji wa aliyowaahidi wapiga kura wake,bondia Changalawe angepata washabiki wa kutosha huko anakopambania medali,all in all kudosi kwa Changalawe.Mandonga aje ale kozi fupi,Changalawe akitua Bongo.
 
Babake naye alikuwa kocha wa timu ya Ngumi mkoa wa Mwanza Meja Changalawe alikuwa Ofisa wa jeshi kambi ya Nyegezi.Sina uhakika kama alishastaafu Jeshi au bado .Wakati anafundisha timu ya mkoa wa Mwanza alikuwa na cheo cha Meja.
 
Wanajeshi wameamua zamu hii kwenye ngumi ,hata kidunda naye kafanya maajabu juzi , siyo kama raia hawa wa kawaida kama kina Mandonga
 
Daah! tena mashindano yanafanyikiwa Birmingham...?
Gwajima asingeleta siasa kwenye utekelezaji wa aliyowaahidi wapiga kura wake,bondia Changalawe angepata washabiki wa kutosha huko anakopambania medali,all in all kudosi kwa Changalawe.Mandonga aje ale kozi fupi,Changalawe akitua Bongo.
Birmingham aliyoahidi mkono wa baunsa ni ya Marekani,hii ya mashindano imo Uingereza.
 
Hongera nyingi kwake ila mbona wapinzani wake wote ni wala ulojo kutoka tuvisiwavisiwa km kule zenji
 
Usikute hata bendera ya tanzania hana kaenda kwa njia za panya.
 
Back
Top Bottom