London
Makao Makuu
Jumuiya ya Madola
Kikao cha 71 CMAG Desemba 2025 Taarifa ya Kuhitimisha ya
Jumuiya ya Madola
Muktasari wa Mkutano wa Sabini na Moja wa Kundi la Mawaziri la Jumuiya ya Madola
5 Desemba 2025
1. Kundi la Mawaziri la Jumuiya ya Madola (CMAG) lilifanya mkutano wake wa sabini na moja mnamo Desemba 5, 2025. Mkutano huo wa maalum ulifanyika kwa njia ya mtandao na kuongozwa na
Mheshimiwa Dkt. Ian Borg, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Utalii wa Malta. Mawaziri na wawakilishi kutoka nchi za Antigua na Barbuda, Botswana, Kanada, Grenada, Malaysia, Mauritius, Samoa, na Zambia walihudhuria.
2. Kundi hilo la mawaziri wajumbe lilisisitiza tena umuhimu wa kuzigatiwa makubaliano ya maadili na kanuni za msingi za Jumuiya ya Madola kama ilivyoainishwa katika Mkataba (charter) wa Jumuiya ya Madola.
3. Mawaziri walisisitiza kuunga mkono Ofisi bora ya Katibu Mkuu, utaratibu wa kulinda na kukuza maadili na kanuni za Jumuiya ya Madola.
4. Mawaziri walionyesha wasiwasi mkubwa kuhusu vitisho vinavyoongezeka dhidi ya demokrasia, utawala wa sheria, uhuru wa mahakama, haki za binadamu, na nafasi ya kidemokrasia inayokabiliwa na
nchi nyingi ndani ya familia yetu ya Jumuiya ya Madola. Wanachama walithibitisha tena kwamba taasisi za kidemokrasia na miundo ya utawala thabiti, na heshima kwa utawala wa sheria na haki za binadamu, ni muhimu kwa maendeleo endelevu na jumuishi ya kiuchumi,
usalama na kwa ajili ya kukuza amani.
5. Kundi lilipokea ripoti kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mbunge).
6. Kuhusu
suala la
Tanzania, Mawaziri walielezea wasiwasi wa pamoja wa Jumuiya ya Madola kuhusu ripoti za
uvunjwaji wa
maadili na
kanuni za msingi za Jumuiya ya Madola, ikiwa ni pamoja na heshima ya
haki za binadamu na
uhuru wa kujieleza,
demokrasia,
utawala wa sheria, na utawala
bora. Wanachama walielezea wasiwasi mkubwa kuhusu hali iliyoripotiwa kuzorota kabla na baada ya uchaguzi (October 2025).
7. Mawaziri walimpongeza Katibu Mkuu kwa tathmini ya haraka ya hali hiyo na uamuzi wake wa kutoa ushirikiano wa Ofisi zake Bora kupitia uteuzi wa Mjumbe Maalum nchini Tanzania, Mheshimiwa Dkt.
Lazarus Chakwera, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Malawi.
8. Kundi liliamua kwamba Tanzania iwekwe kwenye
Ajenda Rasmi ya CMAG kwa mkutano ujao
Machi 2026, kwa uamuzi wa CMAG kuhusu Tanzania.
Uamuzi wa CMAG utategemea kutimiza masharti, vigezo na kanuni zifuatazo:
a. Kwamba Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu apewe uwezo wa
ufikiaji kamili na huru kwa wadau wote husika haraka iwezekanavyo;
b.
Kuondolewa kwa
vikwazo dhidi ya uhuru wa kukusanyika na kujieleza, asasi za kiraia na vyombo vya habari;
c. Kufanyika kwa jukwaa la
mashauriano kati ya vyama ili kukubaliana kuhusu mfumo wa pamoja kuhusu njia ya kuelekea uchaguzi ujao;
Page 1
d. Utekelezaji wa michakato ya kisheria na kiutawala
iliyo wazi ili kuwawajibisha wale wote wahusika wa(violence)
vurugu na matokeo yake na
kuwalipa fidia waathiriwa, inavyofaa.
9. Kundi limeomba Serikali ya Tanzania impatie Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, kwa ajili ya taarifa ya kikao kijacho cha CMAG, hadidu
za rejea
za Tume
ya Uchunguzi
iliyoanzishwa na
Serikali . (Iliyo chini ya wenyekiti wa Jaji Chande)
10. Kundi lilimwomba Katibu Mkuu kutoa ripoti kamili kuhusu maendeleo yaliyopatikana kuhusu masharti hayo hapo juu kwa CMAG katika mkutano wake ujao.
11. Mawaziri walimwomba Katibu Mkuu aendelee kushirikiana na Serikali ya Tanzania na kuendelea kuunga mkono kazi yake ya kuwezesha kuimarisha sera zinazoimarisha utawala wa sheria, (ugatuzi wa mihimili) mgawanyo wa madaraka, kuheshimu katiba, na utawala bora kama ilivyoainishwa katika
Hati ya Jumuiya ya Madola .
12. Kundi pia liliihimiza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupata / kupewa usaidizi wote wa kiufundi unaopatikana kutoka Jumuiya ya Madola ili kuongeza
amani ,
utulivu wa kidemokrasia , na utawala
bora .
13. Kundi la mawaziri wajumbe lilipokea na kumshukuru Katibu Mkuu kwa ripoti zake kuhusu masuala muhimu kwa CMAG.
14. Ilikubaliwa kwamba mkutano ujao wa CMAG utaitishwa mnamo tarehe 7 Machi 2026 katika Wiki ya maadhimisho ya Jumuiya ya Madola huko London.
Page 2
MWISHO
Imetolewa:
5 Desemba 2025