JUST JOKES

kunguni wa ulaya

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
4,131
Reaction score
6,111
Hii nimeikuta sehemu...


UTANI USHAANZA KWA WALIMU


Konda : cheke cheke! abilia nauli

Abiria: mi mwalimu

Konda: onyesha kitambulisho

Mwalimu: (anashika mfukoni) hiki hapa

Konda (anakichukua kile kitambulisho na kukikodolea macho pande zote mbili)....

Konda: (anarudisha kitambulisho) sasa mbona umekalia siti

Mwalimu : kwani kuna tatizo?

Konda: hebu wapishe waliolipa nauli wakae

Mwalimu: (kwa hasira) hebu acha kunizalilisha kijana

Konda: (akimuangalia mwalimu usoni) hivi we unaona ni haki kukaa wakati alielipa nauli amesimama?

Mwalimu (kimya)

Konda: kwanza nyie walimu nina hasira na nyie sana

Mwalimu (kwa ghadhabu) hasira?

Konda: eeh kwanza mlinichapa sana bado nifeli.... na leo unapanda gari yangu huna nauli..

abiria wengine: hahahahahaha

Konda: dah yani sipendi kupakia hizi chenga kubwa

Mwalimu: nani chenga?

Konda : yan wewe ni chenga kuliko huyo mwanafunzi unaemfundisha

Mwalimu: (kwa tabasamu la aibu) kivipi?

Konda : we umekalia siti hujalipa hata mia lakin dogo kasimama na amelipa 200..

Konda (kwa kejeli) sasa sema wewe na dogo nan chenga?

Mwalimu (kwa hasira anafungua pochi na kutoa sh 5000 ) kata mia nne yako mbwa wewe.
 
walimu wakiwa wanapanda daladala bure inamaana mshahara wao utakuwa unafanya kazi gani?
Na wakati huo mwanafunzi ambaye hana hata kazi analipa nauli.
 
Waongezewe mshahara labda 30 au 50 special kwa ajili ya nauli.
 
Huu ubunifu mkubwa sana, tena unafanana na ukweli. Nimecheka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…