Just to test its viability

KijikoYajiko

Senior Member
Joined
May 8, 2012
Posts
106
Reaction score
19
Wakuu salaam?
Nianze tu kwa kukiri kwamba nimetumia muda mwingi kujielimisha kitaaluma na baadaye kupata profession ambayo nadhani bado haijawa msaada kwangu. Dhahiri nakiri hapa huo muda ningeutumia kupata maarifa hapa pengine ningekuwa nimeenda hata hatua moja mbele. Anyway nahisi sijachelewa sana.
Baada ya sakata la kutibuana na mwajiri wangu, niliamua kurudi nyumbani ili kujipa muda walau wakujitizama na kujitafakari huku nikijihoji yakini na mstakabari wangu jambo ambalo nimefanya kwa takribani wiki tatu sasa lakini naona sijapata majibu, God intervene!!
Hata hivyo niishukuru Jf kwani ndiyo amekuwa jamaa na rafiki yangu wa karibu sana (best yangu) kwani ndiye nimekuwa nikimtembelea na yeye kunitembelea. Tumekuwa tukiongea nae tukijadiriana masuala mbalimbali na kupeana ushauri pale inapobidi, na hata kufarijiana. Lakini zaidi ya yote Jf amekuwa Mwalimu wangu mzuri sana. Nimejifunza mengi sana kutoka kwake na kuyaelewa. Uelewa wangu wa mafundisho ya Mwalimu huyu umekuwa wa kiwango cha juu mno na nadhani ni kwa sababu ya mazingira yake ya kufundishia na kujifunza ni mazuri mno. Yana kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya kujifunza. Darasa, vifaa na hata wakufunzi wake ni wakufunzi waliobobea na kwa kweli wamesheheni maarifa ya kutosha. Asante tena Mwalimu wangu Jf.
Sasa basi kutokana na mapitio ya Post nyingi zilizojaa maarifa ya ujasiliamali, nimechota kitu hapa na sasa naanza kukifanyia kazi.
Nimepitia post nyingi za kilimo na kwa vile na mimi ni mtoto wa mkulima zimenivutia na Kunikumbusha wosia wa Baba kuwa ''kama mnataka mali, mtayapata shambani''.
Lipo shamba home owned na lipo pembezoni mwa kamkondo kadogo ka ziwa victoria. Sehemu kubwa ya mwambao wake huwa inafurika hata kwa maji ya kuletwa na mvua zilizonyesha mbali yanayoletwa na vijito vinavyoingia kwenye mkondo huo. Lakini kina cha maji yake hupungua sana na wakati mwingine kukauka kabisa kutegemeana na urefu na ukali wa kiangazi cha msimu ingawa hutokea mara chache sana wastani wa mara moja katika muda wa miaka 15 - 20. Kwa bahati nzuri/mbaya shamba hili lipo kwenye mwinuko mbali kidogo kama meta700 hivi kotoka katikati ya kamkondo haka kiasi ambacho hata mwambao ule ufurike vipi maji hayafikii.
Kusudi langu sasa ni kuliendeleza shamba hili kwa kutumia maarifa aliyonipatia mwalimu wangu huyu.
Nimepanga kuanzisha kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia pampu na kwa kuanzia nataka nitest uwezekano wa pampu nitakayotumia kufikisha maji shambani pale. Nitaanza na eneo kidogo kulingana na mtaji nilionao sasa na nimepanga kuanza na zao la mahindi.
When its viable, I will go for vitunguu maji na matikitimaji as I have lent its is a business which pays plaintfully.
Thank you Jf once again.

 
Tupo pamoja mkuu. Huko uendako ndo kwenye chaguo sahihi kabisa na jambo mujarabu ni kwa wewe kuanza mashambulizi haraka iwezekanavyo.
Thanks kwa kuipa JF-Shule regards za kutosha kabisa.
Nipo hapa kwajili yako, uliza swali lolote kuhusiana na bustani. Ntakujibu kadri ya uelewa wangu.
Wito wangu ni kwamba usiiache JF hata siku moja katika utaftaji wako.
 
Nakupata Kiongozi, namobilize equipment tayari kwa mashambulizi. Nitakuconsult wewe pamoja na wanajamii hatua kwa hatua. Thanks
 
Mawazo mazuri sana mkuu. Tuko pamoja ndugu.
 
hongera sana mkuu. ukikaribia kuvuna nistue.
 
hongera sana mkuu. ukikaribia kuvuna nistue.
Nitafanya hivyo mkuu, na nitashukuru kama utakuwa tayari kunitembelea shambani kwenye kipindi kama hicho ili kuona mafanikio na setbacks na kunishauri cha kufanya kwa ajili ya kuboresha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…