Jux amlilia Vanessa Mdee

Jux amlilia Vanessa Mdee

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Msanii wa muziki bongo fleva Juma Jux aonyesha bado anahitaji uwepo wa aliyekuwa mpenzi wake msanii Vanessa Mdee, kwa kushindwa kuvumilia maumivu ya kuachana na kuweka bayana kwamba atafarijika sana endapo atamuona tena kwa mara nyingine.

IMG_0089.JPG

Msanii Jux​

Jux amebainisha hayo kupitia ukurasa wake Instagram ambapo ameandika ujumbe unaohusu kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, na kusema miaka ya nyuma alikuwa hafanyi sherehe kutokana alikuwa na mpenzi wake Vanessa kwenye siku hiyo nakujiona kama amesherehekea lakini kwa sasa hayuko naye tena anatamani hata aende kuhudhuria tu kama rafiki na itakuwa faraja kubwa kwake.

" Sikuwahi kufanya 'party' yoyote tena sababu nilikuwa na rafiki, mpenzi na mtu wa karibu kuliko mtu yoyote kwenye maisha yangu. Sasa hatuko tena karibu kama mwanzo, tumebaki kuwa marafiki wa kawaida tu. Uwepo wake tu ulikuwa ni zaidi ya chochote kwenye siku yangu ya kuzaliwa, kuongea na yeye au ujumbe wake tu ilitosha kukamilisha siku yangu. Ila sasa sidhani kama itakuwa kama mwanzo, nitafarijika sana kama nitamuona hiyo siku", aliandika Jux.

Jux hivi karibuni akiwa kwenye mahojiano na kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, amekiri kuwa bado ana hisia juu ya Vanessa Mdee, ambaye pia alishawahi kusikika akikiri bado anampenda Jux na ataendelea kumpenda.

Kwa hisani ya EATV
 
Vanesa alikuwa mtu muhimu kuliko mtu yeyote kwake?! Kwani Jux huna wazazi?! Any way hilo ni funzo ukimpa mwingine ukampenda usifanye tena mapenzi ya KISELA..
 
Vanessa akiimba kuna neno uwa anachombeza, sijui anasema NYUFA, hivi maana yake nini?
 
wanaume wa daresalama bwana!
Yaani unapigwa chini na mwanamke unalia lia kiasi hicho! tena hujazaa nae hata mtoto wala kufunga nae pingu za maisha!

Mtakua lini nyie watu??
 
wanaume wa daresalama bwana!
Yaani unapigwa chini na mwanamke unalia lia kiasi hicho! tena hujazaa nae hata mtoto wala kufunga nae pingu za maisha!

Mtakua lini nyie watu??
Hapo ndo wananikata stimu, demu mwenyewe anatiwa tu na masela wengine ,we bado unalialia kutaka kurudiana. dogo wacki sana huyu.
 
Back
Top Bottom