Juzi nilikuwa Posta, Mwendokasi mida ya jioni ni kisanga. Serikali hamwoni? Nusura nipate kilema

Yaani posta hapo unasema mwendokasi kisanga
Wewe ukienda gerezani jioni si utazirai kabisa Mkuu

Katika route yenye ustaarabu angalau ni Kivukoni.
Huko kwingine ndio kivumbi.


Tumeongea humu hadi tumechoka..
Jitu linakuja kukujibu kuwa upande daladala.
Sasa Mbezi posta sijui utapandaje daladala.
 

Serikali iache kupuuza raia wake.
 
Watu warudi Mikoani. Mjini wako wachoma mihogo, mahindi, na biashara kibao. Huku Mikoani kutupu hakuna watu wote wamekimbilia Dar kutafuta Maisha. Makonda angeendelea kuwa Mkuu WA Mkoa Dar kungenyooka. Mji gani kila MTU mchuuzi.

Inawezekana lakini Siku zote Watu hujuma wapi kwa Wafaa kupata Riziki zao
 
Siku moja nilisema niipumzishe gari yangu aina ya Bentley flying Spur ya rangi nyekundu iliyokua na mafuta full tank na tairi mpya nikaenda kupanda mwendokasi

Nilimuona demu mmoja mzuri sana bahati mbaya tulikua tumebanana sana kama ndizi kiasi kwamba hata usiposhikilia popote na ukasinzia huwezi kuanguka, kila nikijitahidi kumsogelea yule mrembo ambae kwenye maisha yangu sijawahi kumshuhudia kama yeye watu wanapiga kelele we usinikanyage.

Hali hiyo ilisababisha nimpoteze kwenye macho yangu na sikujua kashukia wapi nikawa sina uhakika bado yupo kwenye gari au kashukua ikabidi niende hadi kimara mwisho ila sikufanikiwa kumuona tena
 
Serikali iache kupuuza raia wake.
DART wapo humu,hakuna cha maana wanachofanya zaidi ya kupuyanga tu


Kiukweli watu tunaishi kama tupo kuzimu.

Fikiria hiyo kero wewe umeipata siku moja tu,ila Kuna watu asubuhi tumetoka kuteseka na jioni tunakwenda kuteseka hapo Kivukoni na ndio maisha yetu ya kila siku lazima tupande hayo magari.
Gari jingine kuja ni dakika 20 na kuendelea..na hapo foleni si haba...
Ukisema usubiri kukaa hesabu masaa mawili hapo ndio utapata gari la siti...ukisema usimame ndio hivyo njiani unaweza kuzirai kwa huo mbanano maana Posta,jiji nyomi la watu linasubiri gari hilohilo lililojaa tangu ferri.


Njia nzuri angerudi tu mjerumani au muingereza watutawale...ila wabongo sisi kwa sisi imeshindikana kabisa kujiendesha..mfano mzuri ndio huko kwenye mradi wa mwendokasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…