JWTZ iwekeze katika teknolojia ya ndege zisizo na rubani(Drones)

JWTZ iwekeze katika teknolojia ya ndege zisizo na rubani(Drones)

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Sasa ni wakati wa kubadilika, mambo yatokeavyo huko majuu ni matumizi ya ndege zisizo na rubani katika medani za vita.

Jeshi letu ili lisije likachelewa lijikite katika kutumia, kutengeneza na kuzidhibiti aina ya ndege hizi, ndege ambazo sasa ni maarufu sana.

Zinatumika kufanya doria usiku na mchana, kwa hapa TZ zinaweza kutumika kufanya doria katika hifadhi za Taifa, kufanya doria katika bandari bubu, yaani huko duniani kila kitu ni drone, mambo ya kutumana frnt line yamepungua.

Jeshi sasa lianze kutengeneza hivi vitu, tena ni vitu ambavyo vilianza kuuzwa kama toys tu.

Huko vita ya Urusi na Ukraine hakuna anaYemsogelea mwenzake, ukisogea tu drone inatoa habari wazee wa vipimo wanakuangushia mzigo.

Ndio mkaona hii vita inanendelea mapigano ni kurushiana misaili tu.

Drone ndio habari iliyoko huko ulimwenguni.

Itakuwa mmenielewa, tusipitwe.
 
Siyo lazima wote tufanane, hayo tunawaachia wazungu, wahindi, wachina, walatino na waarabu, sisi tumechagua kuwekeza kwenye ujenzi wa frames za maduka kuzunguka Kambi zetu za jeshi.
 
Huku uraiani tumeweza kutengeneza hata baiskeli, mpaka wanajeshi waweze kutengeneza ndege.
Wanajeshi wanazaliwa na kizazi gani, wamekulia wapi wamesoma nchi gani.

Maendeleo ya nchi ndiyo maendeleo ya jeshi, na wenyewe wanategemea bajeti.
 
Siyo lazima wote tufanane, hayo tunawaachia wazungu, wahindi, wachina, walatino na waarabu, sisi tumechagua kuwekeza kwenye ujenzi wa frames za maduka kuzunguka Kambi zetu jeshi.
Inasikitisha sana kambi kuzungukwa na frame za kuuza fegi. Siku hizi kila nikisoma kuwa IQ ya Watanganyika ni 75 sibishani tena na hao watafiti
 
Kitu unachatakiwa kuwa na kiwanda Cha chuma na teknolojia ya chuma.

Silaha zitatengenezwa hapa,magari ya kivita,kibiashara,meli,vifaru na mengineyo.

Ndio nyie mnanichekesha unakuta mtanzania anaangaika na helikopta wakati mfumo wa ndege ya kawaida yenye unampiga chenga
 
Kitu cha muhimu nachoona wanafanya ni kupanda miti wanapokua na vijana wa JKT wakati Ukraine wanatengeneza drones wakiwa vitani sisi tupo busy kuangalia nguo zenye rangi ya jeshi mwanzo nilidhani huko kuna watu smart kumbe hamna kitu...
Kila kinategemea uchumi wa nchi, mbali hivyo vitu vya kijeshi, kiwanda cha kuunda baiskeli nchi mzima kiko wapi.
 
Kwetu kule,ukilamba AJIRA mpaka unastaafu bwashee.
Na tunachojua Nchi yetu imebarikiwa kuwa na amani MILELE,maana hakuna hata kakikundi ka waasi kule kwetu.
Na mwananchi anaenidai kutengeneza aina yoyote ya uvumbuzi!,jela linamhusu.

Na hatuwazi mabadiriko bwashee na Wala kuhisi kuwa yanayotokea kuleeee yanaweza tokea hapa mda wowote,wale wanajua Mungu ni wao tu kule hakuna Mungu bwashee.

Ila one day,tutajipata
 
Ngoja tumalize zoezi letu la kusaka nguo zenye sare zetu

Ova
Afu tupate na katiba mpya kwanza.. afu hizo doria za kwenye mbuga na bandari bubu si tunaweza kuwatuma hata hao hao wahusika wakapambane na maharamia.. Ndugu zangu mmenisikia[emoji445] in profesa Jay's voice
 
Kwanza waanze kuwekeza kwenye Elimu ya askari wao, sio mtu akifeli la saba au kidato cha nne anakimbilia jeshini kiwango cha Elimu kujiunga jeshini kipandishwe juu zaidi ili tuone madaktari, mainjia na wasomi wenye maarifa katika kada tofauti tofauti za kielimu wakijiunga na jeshi kwa wingi kabisa, ujinga wa msomi mwenye digrii sio sawa sawa na ujinga wa wenzangu na mimi darasa la saba
Baada ya hapo sasa ndio wajikite kwenye mambo ya teknolojia ambayo ndio msingi na uti wa mgongo wa majeshi yote ya kisasa duniani, waki wekeza kisawa sawa kwenye teknolojia hapo ndipo watakapo tengeneza magari, ndege vita na vifaa vingine vya kijeshi bila kusahau vifaa vya kijamii kama zana za kilimo na vinginevyo na hapo nchi itaanza kupata faida pamoja na kuokoa fedha nyingi zinazo tumika kuagiza nje lakini pia kutengeneza faida kwa kufanya biashara ya zana hizo
 
Bado bila man to man battle ujashinda vita.
USA na ulaya ni wazuri kwenye technology lakini vita vya mtaa kwa mtaa hawawezi,hio kazi ya Wagner group thus USA alishindwa vita syria
 
Back
Top Bottom