JWTZ kufanya kufuru ujenzi wa nyumba

JWTZ kufanya kufuru ujenzi wa nyumba

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,712
Serikali imeanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya wanajeshi kote nchini.

Hayo yalisemwa na Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Josephat Musira, wakati wa ziara ya waandishi wa habari walipotembelea eneo la Gongolamboto jijini Dar es Salaam ambapo sehemu ya mradi huo unatekelezwa.

"Lengo la ujenzi wa nyumba hizi ni kupunguza tatizo la muda mrefu la uhaba wa nyumba kwa ajili ya makazi ya maofisa na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa," alisema Meja Musira.

Akifafanua zaidi Meja Musira alisema awamu ya kwanza ya mradi huo imeanza ambapo nyumba 6,064 zitajengwa kwa kugharimu dola za Marekani milioni 300, utekelezaji wake unaendelea vizuri katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani tayari jumla ya nyumba 3,128 zinajengwa.
Kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Meja Musira alisema nyumba 2,228 zinajengwa katika maeneo ya Lugalo, Gongolamboto, Ukonga, Navy Kigamboni, Ubungo Kibangu, Kunduchi KTC, Mbweni JKT na Kimbiji.

Akieleza zaidi Meja Musira alisema ujenzi wa nyumba 1,160 kwenye maeneo manne ya Lugalo na Gongolamboto umeshakamilika kwa asilimia 100 na ukaguzi na uhakiki umeshafanyika.

Kwa upande wa Mkoa wa Pwani Meja Musira alisema jumla ya nyumba 840 zinajengwa katika maeneo ya msangani, Nyumbu, Kiluvya, Kisarawe na shule ya mafunzo ya awali Kihangaiko.

Maeneo yanayohusika na mradi huu kwa sasa ni Arusha inatarajiwa kujengwa nyumba (792) Tanga (312) Pemba (320) Morogoro (616) Dodoma (592) Kagera (144) na Kigoma (160).

Kwa upande wake Mhandisi wa Wizara hiyo, Stephen Mpapasingo, alisema mradi huo unatekelezwa kwa awamu na unalenga kuondoa kabisa tatizo la makazi kwa Maofisa na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na Jeshi la Kujenga Taifa. Mkandarasi wa mradi huu ni kampuni ya Shanghai Construction (Group) General Company kutoka China


CHANZO: Majira
 
ngoja wawaweke wachina wawalipulie maghorofa kama uyoga ndani ya miez 2 nyumba ya ghorofa 6 imekamilika. Kama ya pale udom yalianza kucleck mengne hata kabla ya kutumika
 
Maana ya kufuru tafadhalini...
Naona hili neno linatumika ndipo sipo!
 
Acheni kutumia hela vibaya jamani jengeni madarasa ,nunuen madawati na vitabu vya kutosha elimu iko taabani
 
tutahaidiwa mengi sana mwaka huu
 
Daaanh, why not SUMA???!!!!


Twajenga kwa jirani kwetu kwabomoka, SUMA au Mzinga walideserve this tender ili wajiimarishe kiuchumi na hii ingeendelea kwa miradi yote ya serikali kama mashule mahospitali madaraja etc, anyway kitulacho kinguoni mwetu.

Lakini si jana tu hapa wamesema tuache kuandika habari za jeshi, sasa inakuwaje wanajitokeza kwa media na kujinadi, is this related to 2015 strategies
 
Tanzania hatuna wakandarasi hadi kuwapa tender wachina? POOR MIND serikali inatuua kiuchumi
 
JKT hawawezi kujenga hayo majengo hadi wawape hiyo Tenda Wachina?
 
Hongereni..wekeni na mpango wa ukarabati wa hizi nyumba na waambieni hao watakao kaa kwenye hizo nyumba..marufuku kufuga Bata kwenye maeneo ya hizo nyumba maana nyie bwana..
 
Hongera. Nimeziona nyumba hizi pale SAM Regiment,Ubungo Kibangu.Zinakaribia kuisha. Kwenye mazuri tusifie. Acheni negativity wakuu!
 
Back
Top Bottom