Mwakitobile
JF-Expert Member
- Oct 4, 2012
- 452
- 120
Ni mkakati maalumu, wala suala hapa siyo uzalendo wa graduates. Sikumbuki ni mwaka gani ilikuwa ila, waziri wa mambo ya nje wa china alimweleza rais wake kuwa mpango wa kupeleka watu wao (wachina) nje kusoma ulikuwa siyo mzuri kwani katika watu 100, ishirini tu ndiyo waliweza kurudi baada ya kuhitimu. Lakini cha ajabu, yule rais alimwambia, ili warudi wengi inabidi idadi iongozeke mara kumi. Basi wachina waliongezwa kwenda nje na wengi wao walifikia hatua wakawa wanarudi.
Nachotaka kusema hapa, idadi ya graduate kwenye jeshi letu ni ndogo mno, na kama inshu ni uzalendo mi naona siyo sababu!! JWTZ waongeze udahili wa magraduate ili jeshi liwe kisasa zaidi. Vinginevyo nionavyo mie ni kuwa watoto wa wakubwa wameshajaa basi wanasubiri kupeana vyeo. Na ili hilo lifanikiwe, basi graduate zaidi wasiajiriwe.
Kwa elimu ya kuunga unga ndugu yangu tutaendelea kuwa tegemezi, kumbuka technolojia nyingi huanzia jeshini kwenye nchi zilizoendelea. Sasa unaposema waliopo waendelezwe kwanza ni sawa na kuanza kujivuta tulipo kurudi nyuma. Angalia pia nchi nyingi zilizoendelea walivyowekeza kwenye jeshi!! its not about creating a small defence arm force eti la kisasa bila kuajiri graduate wa kutosha. Anyway, Labda hii habari siyo ya kweli hapo.Najua waweza kuwa ni mmoja waliokuwa na nia ya kwenda huko,basi hakijaharibika kitu nakushauri anzia kwanza kuomba jkt kama wewe ni mzalendo kweli,pia futa kauli yako ya kusema jeshi lina wasomi wachache,amini kuna program maalum ya kuwaendeleza askari kitaaluma,nje na ndani ya nchi,kauli mbiu ya jeshi kwa sasa ni "kuwa na jeshi dogo la kisasa" hasa katika vitendea kazi vya ulinzi na usalama
Top 10 Most Powerful Countries - YouTubeNajua waweza kuwa ni mmoja waliokuwa na nia ya kwenda huko,basi hakijaharibika kitu nakushauri anzia kwanza kuomba jkt kama wewe ni mzalendo kweli,pia futa kauli yako ya kusema jeshi lina wasomi wachache,amini kuna program maalum ya kuwaendeleza askari kitaaluma,nje na ndani ya nchi,kauli mbiu ya jeshi kwa sasa ni "kuwa na jeshi dogo la kisasa" hasa katika vitendea kazi vya ulinzi na usalama
Na ndiyo point mkuu, kuna ndugu yangu huwa anasema kabisa vijana wengi wanaoajiriwa wenye elimu wanasumbua wazee kwa kuwa hawa wazee wengi wako nyuma ya mambo, hawajui mambo mengi!! vijana hawaogopi kuhoji wwakiona mambo sivyo! lakini pia askari wengi walishakuwa wakubwa kiumri, sasa ku-mtrain mtu kama huyo inahitaji moyo. Sana sana ni kuwapeleka shule ili waendelee kuwa watiifu kwa mambo ya kijinga, pia kuwafanya wapate kiinua mgongo angalau cha maana lakini si kwa ajili ya ufanisi wa National Defence.kwa hili jwtz litaendelea kuwa nyuma, kwanza uzalendo haupimwi hivyo.
Pili ni vigumu kuwaendeleza waliopo coz mfn kama mtu aliingia akiwa kamaliza form 6 au 4 kuna uwezekano mkubwa kuwa alifeli, mnamuendelezaje mtu kama huyo?
Pili huwezi kupeleka wanajeshi wengi kwa wakati mmoja masomoni, itabidi waende kidogo kidogo na kusoma kunachtkua muda mfn miaka 3 au zaidi, mpaka waloenda warudi ndo waende wengine.
Kwa namna hiyo ni lini jeshi litakuwa na wasomi wa kutosha?
Itachukua zaidi ya miaka kumi.
Wao wangefanya kama polisi, mnawaajiri graduats lakini waanze vyeo vya chini ila kuwalipa muwalipe kwa mujibu wa elimu zao.
Wenzao polisi wameanza kufanya hivyo, mwaka huu pekee wanaajiri wasomi takriban 500 wa ngazi za cheti, diploma na bachela takriban 200.