JWTZ mmetulinda vizuri dhidi ya maadui wa nje, sasa tuna maadui wa ndani wanaopaswa kuchukuliwa hatua

JWTZ mmetulinda vizuri dhidi ya maadui wa nje, sasa tuna maadui wa ndani wanaopaswa kuchukuliwa hatua

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Sio siri kuwa JWTZ inafanya kazi inayotukuka kweli kweli. Maadui wa nje hawafanyi chokochoko tena katika mipaka yetu.

Lakini sasa kuna adui wa ndani ya nchi anateka watu, anawatesa na kuwaua apendavyo. Kuna faida gani mlinzi yuko getini tuu kuzuia azure wa nje wasiingie lakini kama yuko aliyeko ndani anamuacha adhuru walio ndani?

Pia soma: Watu Wasiojulikana: Malisa aelezea tukio la kutekwa kwa Deus Soka na vijana wengine wawili wa CHADEMA

Mashujaa wetu JWTZ mmeona vilio vya mama zenu, shangazi zenu na kaka na dada wakiwalilia wenzenu kaka Soka, Saanane, Sativa nk kama watu wasio tegemeo wakati nyie mpo lakini eti mipakani mkiwasubiri makaburu au manyang'au toka nje?

Nyie sio wa kukodiwa toka mbali (mercenaries) bali ni familia zetu kabisa mnakubalije ndugu zenu waishi kama digidigi?

Pia soma: Simiyu: Wananchi wavamia Kituo cha Polisi wakidai kuna matukio mengi ya Watoto kupotea

TOENI HATA TAMKO.

Tunajua miongoni mwenu wapo wenye fikra kama za huyu!

Bunge tulilotegemea kututetea limetuacha. Mahakama nayo inatoa maamuzi kama vile haioni umuhimu wa haki ya kuishi! Nani sasa þukimbilie kwake? Basi ngoja tujaribu na kwenu.
 
Watatujibu kwambaJWTZ hawaingilii mambo ya ndani, hayo ni madogo tunayaweza wenyewe yaani sisi wananchi tukisaidiana na Police.

Kwa hiyo jibu lipo wazi endapo Police watashindwa kuyadhibiti.
 
Watatujibu kwambaJWTZ hawaingilii mambo ya ndani, hayo ni madogo tunayaweza wenyewe yaani sisi wananchi tukisaidiana na Police.

Kwa hiyo jibu lipo wazi endapo Police watashindwa kuyadhibiti.
Polisi watadhibitije wakat ao ndio watuhumiwa wenyewe?
 
Bunge tulilotegemea kututetea limetuacha.
Mahakama nayo inatoa maamuzi kama vile haioni umuhimu wa haki ya kuishi!
Nani sasa þukimbilie kwake?
Basi ngoja tujaribu na kwenu
Aisee,maisha haya bhana
 
Nani kakudanganya tz imelindwa na maadui kutoka nje? Maadui Kila siku yanatoka nje Kuja kuiba Mali kupitia mikataba ya hovyo
 
Nani kakudanganya tz imelindwa na maadui kutoka nje? Maadui Kila siku yanatoka nje Kuja kuiba Mali kupitia mikataba ya hovyo

Wanaokuja kuiba mali kina nani? JWTZ watafanyaje kama mnasaini mikataba ya magumashi? By the way, Lugumi kama Lugumi sio wao 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Jeshi la polisi haliteki wala kuua watu. Wakija watu wasiojulikana kutaka kukuteka basi jihami kufa kupona, mahambazi hayo, ukiweza kuwaua ua tu. Tena huku ukupiga yowe la mwizi mwizi ili wananzengo waje kukusaidia.
 
Hatua hii tuliyofikia, wawakilishi wetu wanatakiwa kupeleka hoja bungeni kushinikiza kutungwa kwa sheria inayoruhusu mwananchi mmoja mmoja kujilinda mwenyewe kwanza kabla ya kuhusisha polisi. Sheria iende mbele kwa kuruhusu mtu mwenye uwezo wa kununua silaha anununue kama tunavyo nunua magari, na maduka ya silaha yatambulike.
 
Mbuzi wa bwana heri wamekula shamba la bwana heri na kesi kapelekewa Bwana heri
 
Sio siri kuwa JWTZ inafanya kazi inayotukuka kweli kweli. Maadui wa nje hawafanyi chokochoko tena katika mipaka yetu.
Lakini sasa kuna adui wa ndani ya nchi anateka watu, anawatesa na kuwaua apendavyo. Kuna faida gani mlinzi yuko getini tuu kuzuia azure wa nje wasiingie lakini kama yuko aliyeko ndani anamuacha adhuru walio ndani?
Mashujaa wetu JWTZ mmeona vilio vya mama zenu, shangazi zenu na kaka na dada wakiwalilia wenzenu kaka Soka, Saanane, Sativa nk kama watu wasio tegemeo wakati nyie mpo lakini eti mipakani mkiwasubiri makaburu au manyang'au toka nje?
Nyie sio wa kukodiwa toka mbali (mercenaries)bali ni familia zetu kabisa mnakubalije ndugu zenu waishi kama digidigi?
TOENI HATA TAMKO.
Tunajua miongoni mwenu wapo wenye fikra kama za huyu!
Kwa hiyo unasemaje, unapendekeza kuwa JWTZ waipindue serikali ya CCM kama alivyofanya Traole wa Burkina Faso kwa maslahi ya Tanzania?

Kwani CCM haishindi kura kwa haki? Maana kama kuna ushahidi CCM haishindi kura kwa haki na wanavunja Katiba makusudi, basi kweli JWTZ wanapaswa kuwaondoa kwa nguvu ili wasaidie uchaguzi huru na wa haki ufanyike

La sivyo JWTZ watakuambia kama Watanzania wengi wameamua kuwa wajinga wa kuchagua watu wasiofaa na wafijaji wa maliasili za nchi ili wawaongoze, hiyo ni haki yao ya kidemokrasia!
 
Back
Top Bottom