Kwani kuilinda katiba unaelewaje mkuu?
Mimi nachojua jeshi kuilinda katiba si kufanya maamuzi juu ya utendaji wa kawaida wa viongozi.
Katiba ni sheria mama kwa hiyo jeshi hutekeleza wajibu kulingana na sheria na taratibu zilivyo za nchi na hii ndiyo kulinda katiba yenyewe.
Kumbuka jeshi ni moja kati taasisi nyeti na zinazoongozwa si kwa mihemuko ya kisiasa kama zilivyo taasisi nyingine za kawaida.
Jeshi lina kitabu chake kiitwacho JUZUU kama sijasahau. Humo zipo sheria zote za nchi na sheria za kijeshi hivyo utaratibu unaotumika jeshini wote unapatikana humo.
Kwenye kitabu hicho ndimo kwenye maandishi yanayoainisha maamuzi ambayo yatafikiwa endapo tukio fulani litatokea mf
1.Kama nchi ikivamiwa na nchi nyingine ni utaratibu gani unatakiwa ufuatwe?
2. Ni wakati gani ambapo raisi anaweza kutangaza hali ya hatari na akifanya hivyo jeshi linatakiwa litekelezeje?
3. Ni wakati gani ambapo jeshi linaweza kuchukua jukumu la kuondoa uongozi kwenye madaraka. Na mengine mengi kama hayo.
Ni vizuri kufahamu mambo haya:
Wananchi ndiyo walio iingiza serikali madarakani na pia ndio waliochagua wawakilishi wao wa kuwawakilisha bungeni. Na hii ni kutokana na haki ya kidemokrasia ambayo ni kipengele kimojawapo kwenye hiyo katiba.
Hivyo basi kwakuwa jeshi kazi yake ni pamoja na kuilinda katiba lazima iheshimu wawakilishi wote wa wananchi (Viongozi + wabunge ) bila kupendelea.
Kama pande hizi mbili hazikubaliani kwa hoja bado jeshi halina mamlaka ya kuingilia mpaka wenyewe watakapo patana au kuondolewa na wananchi kwenye nyadhifa hizo kwa njia ileile ya kidemokrasia.
Kulifikiria jeshi kwa maswala ya kisiasa sidhani kama ni njia muhimu ya kufikia malengo yaliyo tarajiwa.
Mwisho naomba nikuulize maswali mtoa mada,
Ulitaka labda jeshi liingilieje mchakato wa katiba?
Kwakuwa serikali imeweka msimamo wake itolewe madarakani kwani jeshi ndilo lililoiweka kwenye madaraka?
Kwakuwa UKAWA wamekataa kuendelea na mjadala wa katiba wapigwe na jeshi na walazimishwe kujadili? Kwani jeshi ndilo lililowachagua wabunge wanaounda UKAWA?
Vipi jeshi likiunga mkono upande mmoja wananchi waliouingiza upande mwingine kwenye hiyo nafasi watakuwa wametendewa haki gani na jeshi linaloitwa JESHI LA WANANCHI?
Mwisho nishauri tu watu tupungize jazba maana hakuna vita kiasi kwamba sasa tuanze kufikiria matumizi ya jeshi.
NB Mwanajeshi anaweza kuwa mkereketwa wa siasa ila hii haimaanishi jeshi lina siasa.
Hapa namaanisha kama mwanajeshi ni mkereketwa wa CDM, CCM, CUF nk haimaanishi jeshi ni la chadema au ccm au Cuf!
Muda mwema!