JWTZ yaishindwa makongo high school...

NGALAMU

Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
39
Reaction score
7
Ndugu watanzania katika hali isiyokua ikitegemewa,jwtz ambao ndio wamiliki wa shule hii sasa wanaua elimu kwa kasi kama ifuatavyo; 1.Huu mwezi wa pili walimu hawajalipwa mishahara yao ya octoba na novemba.2.mkuu wa shule kaitelekeza shule kwa msaidiz wake kukwepa madeni.3.poor anual exams invigilation due to teachers boycotting,4.poor food for dom students, etc. je kama makamanda wanatapeli wazazi, je wengine?
 
Maskini! nakumbuka Makongo enzi za Iddi Kipingu ilikua shule ya uhakika.vipi mkuu nawewe ni Teacher wa hapo nini?
 
elimu ya tanzania ilishakufa siku nyingi sana!!

Poleni wazazi na walezi,..
 
Hapo kutakuwa na tatizo kubwa,je uongozi wa juu wa jeshi (TPDF) unataarifa?
 
BIG RESULT NOW hiyooooooooooooooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! inakuja
 
Hiyo shule imeharibiwa na mkuu wake wa sasa. Tangu aingie amekuwa akijigamba kufanya changes ambazo hazina tija. Ameshindwa kusimamia taaluma, maslah ya walimu duni, mbabe, nk
 
yale yale namkumbuka Kipingu kuna kipindi alikua anazama class na anfundisha somo la kiingereza yuko vizuri na aliweza kuiongoza shule vizuri kipindi kile.Marehemu miraji,kamanda Babu chacha bila kumsahau marehemu Meja yeyeye haya majembe yalikua yanazingatia kazi yao
 

Bila kumsahau Mwashiga,Mwaseba,Madhege,Kisarika,Mataula na wengineo wote.
 
HAKIKA UONGOZI WA JESHI UNATAKIWA KULAUMIWA KWA KILA LINALOTOKEA KWA SASA HAPO MAKONGO KWA KUWA NIKIWA MWALIMU HAPO MAKONGO TULIJARIBU KUFIKISHA MALALAMIKO YETU KWA UONGOZI WA JUU WA JESHI NA KUELEZA WAZI UBADHILIFU UNAOENDELEA HAPO SHULENI UNAOFANYWA NA MSARIFU WA SHULE MAJOR KAKUMBI LAKINI TULIONEKANA WACHOCHEZI NA MIKATABA YETU ILIPOISHA WALITUONDOA. WAKATI OFISI YA KURUGENZI YA ELIMU ILIKUWA NA TAARIFA ZOTE ZA UBADHILIFU HUO NA WALIPATA MUDA WA KUTEMBELEA SHULE NA TULIWAELEZA YOTE. NASHANGAA MPAKA SASA MKUU WA SHULE LT. MWANGASI NA MSARIFU MAJOR KAKUMBI BADO WAPO LAKINI WALIMU WANATAABIKA. NASHAURI MKUU WA MAJESHI ACHUKUE HATUA KUINUSURU SHULE HII ILIYO KUWA NA HESHIMA KUBWA.

YAFUATAYO NI MADAI YA WALIMU TULIYO PELEKA KWA UONGOZI WA JESHI AMBAO ULIPUUZA NA KUMSIKILIZA MKUU WA SHULE NA MSARIFU WAKE KUWA SISI NI WACHOCHEZI IWAPO MKUU WA MAJESHI ATAHITAJI TUTOE USHAIDI MIMI NIKO TAYARI WAKATI WOWOTE ILI MRADI HAKI ITENDEKE NA WABADHILIFU WOTE WAFIKISHWE KATIKA MIKONO YO SHERIA:
MCHANGANUO WA MAPATO NA MAPENDEKEZO YA WALIMU RAIA KWA UONGOZI WA JESHI ILI KUBORESHA USTAWI WA SHULE NA KIPATO CHA WAFANYAKAZI KWA UJUMLA
Kumekuwa na tabia inayojitokeza mara kwa mara shule kuishiwa Fedha za kugharimia shughuli za kila siku (malipo mbalimbali) kutokana na kukosa kipaumbele na pia matumizi mabaya ya Fedha. Kutokana na hali hiyo tumeona ni vyema kuainisha vyanzo vyote vya mapato ya shule ambavyo kama vikisimamiwa vizuri vitaiwezesha shule kuendesha shughuli zote ikiwa pamoja na kuboresha maslahi ya walimu na wafanyakazi wake ili waweze kuishi maisha ya staha.
(a) ADA YA WANAFUNZI WA KUTWA
Ili kuonesha vizuri mapato ya shule ni vizuri kujua idadi ya wanafunzi wote na ada wanayolipa kwa mwaka.
IDADI YA WANAFUNZI NA ADA WANAYOLIPA KIDATO CHA I-IV
Ifuatayo ni idadi ya wanafunzi kuanzia kidado cha I hadi cha IV na kiasi cha mapato (ada inayolipwa kwa mwaka kwa kila kidato):
KIDATO CHA KWANZA
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 60"]
S/NO.
[/TD]
[TD="width: 110"]
DARASA
[/TD]
[TD="width: 104"]
IDADI YA WANAFUNZI
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
1.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-1
[/TD]
[TD="width: 104"]
55
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
2.
[/TD]
[TD="width: 110"]
B-1
[/TD]
[TD="width: 104"]
56
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
3.
[/TD]
[TD="width: 110"]
C-1
[/TD]
[TD="width: 104"]
60
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
4.
[/TD]
[TD="width: 110"]
D-1
[/TD]
[TD="width: 104"]
55
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
5.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-2
[/TD]
[TD="width: 104"]
60
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
6.
[/TD]
[TD="width: 110"]
B-2
[/TD]
[TD="width: 104"]
55
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
7.
[/TD]
[TD="width: 110"]
C-2
[/TD]
[TD="width: 104"]
61
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
8.
[/TD]
[TD="width: 110"]
D-2
[/TD]
[TD="width: 104"]
64
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
[/TD]
[TD="width: 110"]
JUMLA
[/TD]
[TD="width: 104"]
466
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Kila mwanafunzi wa kidato chaI anatakiwa kulipa ada ya shilingi 600,000/- kwa mwaka. Kwa hiyo idadi ya wanafunzi 466 x 600,000/- unapata shilingi milioni 279,600,000/- kwa mwaka.
KIDATO CHA PILI
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 60"]
S/NO.
[/TD]
[TD="width: 110"]
DARASA
[/TD]
[TD="width: 104"]
IDADI YA WANAFUNZI
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
1.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-1
[/TD]
[TD="width: 104"]
75
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
2.
[/TD]
[TD="width: 110"]
B-1
[/TD]
[TD="width: 104"]
78
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
3.
[/TD]
[TD="width: 110"]
C-1
[/TD]
[TD="width: 104"]
80
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
4.
[/TD]
[TD="width: 110"]
D-1
[/TD]
[TD="width: 104"]
74
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
5.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-2
[/TD]
[TD="width: 104"]
62
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
6.
[/TD]
[TD="width: 110"]
B-2
[/TD]
[TD="width: 104"]
70
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
7.
[/TD]
[TD="width: 110"]
C-2
[/TD]
[TD="width: 104"]
74
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
[/TD]
[TD="width: 110"]
JUMLA
[/TD]
[TD="width: 104"]
513
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
KIDATO CHA TATU
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 60"]
S/NO.
[/TD]
[TD="width: 110"]
DARASA
[/TD]
[TD="width: 104"]
IDADI YA WANAFUNZI
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
1.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-1
[/TD]
[TD="width: 104"]
68
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
2.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-2
[/TD]
[TD="width: 104"]
70
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
3.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-3
[/TD]
[TD="width: 104"]
70
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
4.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-4
[/TD]
[TD="width: 104"]
60
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
5.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-5
[/TD]
[TD="width: 104"]
60
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
6.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-6
[/TD]
[TD="width: 104"]
50
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
7.
[/TD]
[TD="width: 110"]
S-1
[/TD]
[TD="width: 104"]
75
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
8.
[/TD]
[TD="width: 110"]
S-2
[/TD]
[TD="width: 104"]
70
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
9.
[/TD]
[TD="width: 110"]
C-1
[/TD]
[TD="width: 104"]
70
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
10.
[/TD]
[TD="width: 110"]
C-2
[/TD]
[TD="width: 104"]
65
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
[/TD]
[TD="width: 110"]
JUMLA
[/TD]
[TD="width: 104"]
658
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
KIDATO CHA NNE
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 60"]
S/NO.
[/TD]
[TD="width: 110"]
DARASA
[/TD]
[TD="width: 104"]
IDADI YA WANAFUNZI
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
1.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-1
[/TD]
[TD="width: 104"]
50
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
2.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-2
[/TD]
[TD="width: 104"]
54
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
3.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-3
[/TD]
[TD="width: 104"]
60
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
4.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-4
[/TD]
[TD="width: 104"]
55
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
5.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-5
[/TD]
[TD="width: 104"]
56
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
6.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-6
[/TD]
[TD="width: 104"]
70
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
7.
[/TD]
[TD="width: 110"]
S-1
[/TD]
[TD="width: 104"]
57
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
8.
[/TD]
[TD="width: 110"]
S-2
[/TD]
[TD="width: 104"]
64
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
9.
[/TD]
[TD="width: 110"]
C-1
[/TD]
[TD="width: 104"]
69
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
10.
[/TD]
[TD="width: 110"]
C-2
[/TD]
[TD="width: 104"]
70
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
11.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-7
[/TD]
[TD="width: 104"]
60
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
12.
[/TD]
[TD="width: 110"]
A-8
[/TD]
[TD="width: 104"]
58
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
[/TD]
[TD="width: 110"]
JUMLA
[/TD]
[TD="width: 104"]
723
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Kila mwanafunzi wa kidato cha Pili, kidato cha Tatu na kidato cha Nne anatakiwa kulipa ada ya mwaka kiasi cha shilingi 580,000/- . Ukijumlisha idadi ya wanafunzi wa kidato cha II, III na IV (513+658+723=1893) Unapata Jumla ya wanafunzi 1893. Idadi hii 1893 X 580,000 unapata shilingi 1,098,520,000/-
KIDATO CHA TANO
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 60"]
S/N0.
[/TD]
[TD="width: 110"]
KIDATO
[/TD]
[TD="width: 104"]
IDADI YA WANAFUNZI
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
1.
[/TD]
[TD="width: 110"]
EGM
[/TD]
[TD="width: 104"]
14
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
2.
[/TD]
[TD="width: 110"]
PCM
[/TD]
[TD="width: 104"]
10
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
3.
[/TD]
[TD="width: 110"]
HKL
[/TD]
[TD="width: 104"]
32
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
4.
[/TD]
[TD="width: 110"]
HGL
[/TD]
[TD="width: 104"]
29
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
5.
[/TD]
[TD="width: 110"]
HGK
[/TD]
[TD="width: 104"]
13
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
6.
[/TD]
[TD="width: 110"]
ECA
[/TD]
[TD="width: 104"]
4
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
7.
[/TD]
[TD="width: 110"]
HGE
[/TD]
[TD="width: 104"]
10
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
8.
[/TD]
[TD="width: 110"]
PCB
[/TD]
[TD="width: 104"]
14
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
[/TD]
[TD="width: 110"]
JUMLA
[/TD]
[TD="width: 104"]
126
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
KIDATO CHA SITA
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 60"]
S/N0.
[/TD]
[TD="width: 110"]
KIDATO
[/TD]
[TD="width: 104"]
IDADI YA WANAFUNZI
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
1.
[/TD]
[TD="width: 110"]
EGM
[/TD]
[TD="width: 104"]
28
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
2.
[/TD]
[TD="width: 110"]
PCM
[/TD]
[TD="width: 104"]
38
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
3.
[/TD]
[TD="width: 110"]
PCB
[/TD]
[TD="width: 104"]
32
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
4.
[/TD]
[TD="width: 110"]
HKL-1
[/TD]
[TD="width: 104"]
29
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
5.
[/TD]
[TD="width: 110"]
HKL-2
[/TD]
[TD="width: 104"]
33
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
6.
[/TD]
[TD="width: 110"]
HGL
[/TD]
[TD="width: 104"]
28
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
7.
[/TD]
[TD="width: 110"]
HGE
[/TD]
[TD="width: 104"]
28
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
8.
[/TD]
[TD="width: 110"]
KLF
[/TD]
[TD="width: 104"]
4
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
9.
[/TD]
[TD="width: 110"]
ECA
[/TD]
[TD="width: 104"]
20
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
10.
[/TD]
[TD="width: 110"]
HGK
[/TD]
[TD="width: 104"]
25
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 60"]
[/TD]
[TD="width: 110"]
JUMLA
[/TD]
[TD="width: 104"]
265
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Ada inayolipwa na kidato cha V ni shilingi 680,000/- kwa mwaka na kidato cha sita ni 650,000/- kwa mwaka. Kidato cha V.....................680,000 X 126 = 85,680,000/- Kidato cha VI....................650,000 X 265 = 172,250,000/- Kutokana na mchanganuo huo wa madarasa kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato cha sita Jumla ya mapato yanayotokana na ada ya wanafunzi wa kutwa ni ka ma ifuatavyo:
Kidato cha I.......................................shilingi....279,600,000/-
Kidato II,III na IV...............................shilingi..1,098,520,000/-
Kidato cha V na VI............................Shilingi.....257,930,000/-
Jumla ya mapato ya ada ya kutwa..Shilingi..1,636,050,000/-
Malipo ya ada ya shule yanalipwa kupitia Account number: 049103001193 (School fees), NBC
(b ) PRE-FORM V (WANAFUNZI WANAORUDIA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
Mwaka huu (2012) shule imepokea wanafunzi wapatao 310 na kila mwana funzi analipa ada ya shilingi 450,000/- Jumla ya mapato ni shilingi.......................139,500,000/- Mshahara kila mwezi ni shilingi 7,000,000/- kwa miezi saba inaleta Jumla ya shilingi 49,000,000/- Gharama za stationary..........................5,000,000/-
Malipo ya ada ya Pre- Form Five yanalipwa kupitia Account number:01J1095787400 ( CRDB- MLIMANI CITY) (c)ADA YA WANAFUNZI WA BWENI
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 57"] S/NO
[/TD]
[TD="width: 227"]
WANAFUNZI
[/TD]
[TD="width: 123"]
IDADI
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 57"] 1.
[/TD]
[TD="width: 227"] WASICHANA-KAWAIDA
[/TD]
[TD="width: 123"]
176
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 57"] 2.
[/TD]
[TD="width: 227"] WASICHANA-WANAMICHEZO
[/TD]
[TD="width: 123"]
29
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 57"] 3.
[/TD]
[TD="width: 227"] WAVULANA-KAWAIDA
[/TD]
[TD="width: 123"]
248
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 57"] 4.
[/TD]
[TD="width: 227"] WAVULANA-WANAMICHEZO
[/TD]
[TD="width: 123"]
48
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 57"]
[/TD]
[TD="width: 227"] JUMLA
[/TD]
[TD="width: 123"]
501
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Wanafunzi wa bweni wanalipa kiasi cha shilingi 900,000 X 501 = 450,900,000 kwa mwaka. Haieleweki Gharama za uendeshaji na kiasi kinachobaki na kinafanyiwa nini.
Account number: 040103002064 (Makongo Boarding School)
Kipato hiki cha ada bila kujali vyanzo vingine vya mapato ( kama vile Adult Education, Veta ) iwapo kingesimamiwa vizuri kingeweza kuendesha shughuli zote za shule na kulipa mishahara iliyo mizuri na kuwafanya waishi maisha ya staha ili kuweza kufanya kazi vizuri na kuijenga shule ili kurudisha heshima yake ikizingatiwa kwamba shule inasaidiwa Gharama mbalimbali za uendeshaji kama vile maji, umeme na mishahara ya walimu askari na maofisa inalipwa na jeshi la wananchi wa Tanzania. Kilichopo sasa ni ubadhirifu uliokithiri unaofanywa na ofisi ya msarifu wa shule na kuifanya shule kushindwa kumudu kuwalipa wafanyakazi wake kwa uhakika. (d) VYANZO VINGINE VYA MAPATO AMBAVYO KIASI CHAKE CHA PESA HAKIJULIKANI
(e) FREMU ZA BIASHARA
Fremu za biashara zilizojengwa kuzunguka shule zisizopungua 24 zikisimamiwa vizuri itakuwa ni moja ya chanzo cha mapato ya shule na kuondoa hali ambayo inaikuta shule ya kuishiwa kabisa na kuanza kuhangaika kulipa mishahara ya watumishi wake hasa mwishoni mwa mwaka. Hata hivyo makusanyo ya kodi za pango za fremu kilikuwa hakieleweki hadi kufikia tarehe 1 /08 / 2012, wapangaji waliagizwa kwa barua kuwa walipe kupitia benki kwa akaunti NUMBER: 040103002027 NBC (MAKONGO HIGH SCHOOL PROJECT FUND)
(f) MIRADI YA SARE ZA SHULE, VIATU NA SARE ZA BWENI
Inashauriwa kuwa mradi wa sare za shule, viatu na sare za bweni usimamiwe moja kwa moja na shule kwa kuwa shule ina kitengo cha ufundi. Hii itaweza kuongeza kipato cha shule na kuweza kugharimia shughuli zake mbalimbali. Kwa sasa kuna watu wamepewa kazi ya kushona nguo hizo lakini haieleweki shule inafaidika vipi kutokana na biashara hiyo. Pia tunashauri mradi wa kantini (vinywaji baridi-soda na maji n.k.) uendeshwe na shule yenyewe moja kwa moja badala ya kuwaachia watu binafsi kama ilivyo hivi sasa. Pia kuanzishwe duka la shule kwa ajili ya kuuza bidhaa mbalimbali kwa wanafunzi, walimu na jumuia inayoizunguka shule kwa ujumla. 2. VIGEZO VYA ULIPAJI WA MISHAHARA
Kumekuwa na tofauti katika viwango vya mishahara baina ya watumishi/wafanyakazi. Kutokana na jambo hili tunashauri ukaguzi wa elimu wa watumishi wote ufanyike ili viwango vya mishahara vizingatie kiwango cha elimu. Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wafanyakazi kupewa mishahara bila hata kuonyesha uthibitisho wa elimu yao. Kuepukahilitunaomba ukaguzi maalumu wa vyeti vya watumishi ufanyike ili kila mfanyakazi alipwe kwa haki. 3. MAPENDEKEZO YA MSHAHARA Tunapendekeza kuwa mishahara ya walimu iongezwe kuanzia shilingi 640,000/- kwa walimu wenye diploma na 700,000/- kwa walimu wenye digrii. Pia tunapendekeza posho ziongezwe. Ongezeko la kila mwaka liwepo. Vyote hivi viainishwe kwenye mkataba wa ajira. 4. UKAGUZI HURU WA MAPATO NA MATUMIZI Pia tunapendekeza kufanyike ukaguzi huru wa mapato na matumizi ili kuweza kujiridhisha kuwepo au kutokuwepo kwa ubadhrifu wa fedha za shule. Tunashauri ukaguzi huu uende sambamba na kufuatilia mali za msarifu wa shule ili kulinganisha na kipato chake na kama una uhusiano na ubadhirifu wa fedha za shule. Iwapo ubadhirifu huu utadhihirika wazi tunashauri hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote wanaohusika. 5. WALIMU KUKOSA IMANI NA MSARIFU WA SHULE (BURSAR) Kutokana na usimamizi, ukusanyaji na ubadhilifu katika ofisi ya msarifu wa shule walimu wanapendekeza msarifu wa shule apangiwe kituo kingine cha kazi ili aweze kupisha uchunguzi uliopendwekezwa katika kipengele namba tano. Msarifu wa shule amekuwa ni kikwazo kikubwa kwa Maendeleo ya shule. Pia amekuwa akitoa lugha za jeuri kwa nyakati tofauti kwa walimu. Iwapo uongozi wajeshi unataka kuthibitisha hili unaweza hata kupiga kura za siri miongoni mwa walimu na wafanyakazi. 6. ULIPWAJI WA FEDHA ZA KUMALIZA MKATABA (GRATUITY) Mara baada ya Mwalimu kumaliza mkataba alipwe mafao yake kwa wakati ili kukabiliana na kupanda kwa Gharama za maisha na mfumuko wa bei. Malipo haya yamekuwa yakicheleweshwa na hivyo kumuathiri mwalimu katika mipangilio yake. 6. ULIPWAJI WA MALIPO MBALIMBALI IWAPO TAREHE YA MALIPO INAANGUKIA JUMAMOSI AU JUMAPILI Kumekuwa na tabia ya kusogeza mbele malipo mbalimbali iwapo tarehe yake ikiangukia jumamosi, jumapili au hata siku za sikukuu. Walimu wanashauri kuwa iwapo tarehe ya malipo inaangukia jumamosi au jumapili au siku za sikukuu basi malipo hayo yafanyike siku ya nyuma yake. Pia kuwepo na taarifa za mara kwa mara kuwajulisha walimu kuwepo au kutokuwepo kwa malipo badala kuwaacha walimu wakihangaika kutafuta habari hizo. 7. MIKATABA YA KAZI Walimu wanapendekeza mikataba ya kazi kurejewa upya ili kutokiuka sheria za kazi na taratibu za ajira. Pia kumekuwepo na walimu walio katika matazamio ya zaidi ya mwaka kitu ambacho ni kinyume sheria za kazi na nchi. Zaidi ya hapo likizo iweke wazi. 8. MIKOPO YA BENKI Pia walimu wanapendekeza kuwa mikopo iliyokuwa inatolewa na mabenki mbalimbali kwa kudhaminiwa na shule irejeshwe. Kilichotokea ni shule kukosa mikataba ya ajira ambayo itamlazimu Mwalimu kulipa mkopo kabla ya kuondoka. Mikopo hiyo inawawezesha walimu kukamilisha mipango mbalimbali ya Maendeleo. Hapo mwanzo walimu wengi waliweza kukopa mikopo benki mbalimbali na kurejesha mikopo hiyo. Kilichotokea ni kuwa mara kwa mara msarifu wa shule alikata makato katika mishahara ya walimu lakini alichelewesha kupeleka benki kitu ambacho kilisababisha baadhi ya walimu kutozwa riba na taasisi za Fedha kukosa imani na shule. 9. KODI YA MAPATO Msarifu wa shule amekuwa akikata kodi ya mapato katika mishahara ya walimu na wafanyakazi wasio walimu. Pamoja na makato hayo yamekuwa hayawasilishwi sehemu husika na endapo ikitokea yamewasilishwa kiasi kinachowasilishwa ni pungufu ya kile kilichokatwa. Kitendo hiki ni kuhujumu mapato ya serikali. Walimu wanashauri kuwa uongozi wa jeshi uwasiliane na mamlaka ya mapato kwa hatua za kisheria. Pia kumekuwa na kodi inayotozwa katika malipo ambayo mwalimu analipwa pale amalizapo mkataba (gratuity) lakini hata mara moja risiti zinazoonyesha ulipwaji wa mapato hayo katika mamlaka ya mapato hazijawahi kutolewa kwa walimu husika. Hii inawatia mashaka walimu endapo malipo hayo yanaifikia mamlaka hiyo. 10. UWAKILSHI KATIKA BODI YA SHULE Walimu na wafanyakazi hatuna wawakilishi katika Bodi ya Shule, hii inaondoa uwazi wa uendeshaji mzima wa shughuli za shule. Hivyo basi, walimu wanapendekeza wawe na mwakilishi/wawakilishi katika bodi ya shule ili kuweza kufikisha matatizo yao mara yanapotokea. Pia hii itasaidia kupata mrejesho nyuma kwa mambo yanayojiri katika bodi ya shule .Tunapendekeza kuwa mwakilishi achaguliwe na walimu / wafanyakazi wenyewe. Kinachotokea sasa ni kuwa mkuu wa shule ndiye anayechagua wajumbe wote wa bodi .Kitendo hiki kinaweza kusababisha kuwepo kwa bodi inayotekeleza matakwa ya mkuu wa shule bila kujali maslahi ya shule na taifa kwa ujumla. 11. KAMATI YA USIMAMIZI WA SHULE (SCHOOL MANAGEMENT TEAM) Kamati hii huteuliwa na Mkuu wa Shule na kwa maana hiyo hufanya kazi kwa maelekezo ya yake. Hii imepelekea walimu kutokuwa na taarifa muhimu za uendeshaji wa shule au kuwa na usiri mkubwa. Kwa maana hiyo walimu tunakosa imani na kamati hiyo. 12. FEDHA YA KUPANGA NYUMBA Kuna utaratibu wa mkopo wa kupanga nyumba kwa walimu ambao hauendani na hali halisi ya kupanda kwa Gharama za nyumba. Mkopo huu ni wa shilingi 400,000/- kwa mhitaji, ambao huambatana na kujaza fomu. Hata hivyo fomu hii ina utata kwani inaonesha kuwa"shule inampangia Mwalimu nyumba". Walimu wanapendekeza iwekwe wazi kama ni mkopo au la. Iwapo ni mkopo walimu wanapendekeza basi wapewe kiwango kinachotosha kupanga nyumba kwa gharama ya wakati husika. kuliko cha sasa cha shilingi 400,000/- ambacho hakiendani na gharama za nyumba kwa sasa. 13. POSHO ZA KUFANYA KAZI NJE YA KITUO CHA KAZI Kumekuwa na utaratibu wa kuwalipa kiasi cha shilingi elfu kumi (10,000/-) walimu au wafanyakazi wanapotumwa kufanya kazi nje ya shule. Kiasi hiki ni chini ya viwango vya posho vilivyowekwa na serikali kisheria. Huu ni ukiukwaji wa sheria za nchi. Walimu wanapendekeza kuwa viwango vilivyowekwa na serikali vifuatwe. 14. MATIBABU KWA WALIMU Walimu wanapendekeza kuwa kuwepo na utaratibu wa matibabu kwa wafanyakazi kama vile bima ya afya ili kujihakikishia usalama wao pamoja na familia zao. Kwa sasa hakuna uhakika wowote wa matibabu kwa wafanyakazi. 15. UNUNUZI WA BIDHAA KATIKA DUKA LA JESHI Walimu wanaomba uongozi wa jeshi uweke utaratibu maalumu kuwawezesha walimu na wafanyakazi wa shule kuweza kupata huduma ya kununua vitu katika duka la jeshi. Kwa sasa huduma hiyo kwa walimu na wafanyakazi raia haipo.
16. MAHUSIANO/USHIRIKIANO KAZINI
Kumekuwepo na hali ya baadhi ya walimu/wafanyakazi wanajeshi kujiona wao ni bora zaidi na hata kuwanyanyasa walimu/wafanyakazi raia. Wakati mwingine kutolewa matangazo ya kudhalilisha walimu mbele ya wanafunzi kutoka kwa uongozi wa shule. Walimu wanapendekeza kuwa walimu/wafanyakazi wanajeshi waonyeshe mshikamano na ushirikiano na raia kwa kuwa wote wanajenga taasisi moja. Pia matangazo yatolewapo mbele ya wanafunzi yatolewe kwa uangalifu yasiwakwaze walimu. 17. HITIMISHO: Kutokana na mwenendo mzima wa ukusanyaji na usimamizi wa mapato kutoridhisha / kuwa mbovu, walimu hatuna imani na msarifu mkuu wa shule. Hivyo, hatuko tayari kufanya naye kazi. Tunashauri uchunguzi wa kina ufanyike kubaini ubadhiifu huu ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika.



 
Well said mr.katamba kwa sasa hali ni mbaya sana bila kujali nani ni king'amuzi? Hata wapambe zao akina MALONGORI,ODICK,YONA(mchaga asiyejitambua),NGURUBI. nk,wote njaa tupu.MOLARI YA WALIMU IKO CHINI SANA UKIONDOA MISUKULE KAMA VILE Dafa,yona,madelemi, na ndalo. Pia maafisa wa jeshi nao hawajalipwa conso zao toka june mpaka sasa. Kwa sasa hali ilivyo ni kwamba shule inakimbiza kuelekea kufunga kwa likizo ndefu ili wafungue mapema! Ajabu sasa kumezuka ujinga ambao una baraka za shule kuwaibia wazazi pesa mfano; mwl.YONA MASAWE kaanzisha program ya pre form 3,pre form2 na wanafunzi wa f3 kulazimishwa kupiga picha za mwakani watakapokua f4,why now? Katamba,pius,makene(lawyer) na manumbu waliitwa CHADEMA na ni waongo, now is your turn LT.COL.Mwangasi justfy your words the above mentioned guys were not pirates.-" war is drug don't start it, because the end of war is seen by the dead ones"!
 
Kwajinsi jina MAKONGO lilivyojulikana Tz nashauri matatizo yaliopo yashughulikiwe mara moja..maana hapo ni hasara n kwa mwanafunzi nasio kwa maafisa ambao mambo yao ni safi daima kwani bia...sigara chee palepale serikali itawapa.afande mkuu kuwa mzalendo kwa walimu na wadau wa Makongo
 
KATIKA KIKAO NA C.O.T. (chief of trainning)TULISEMA KUWA IWAPO MAJOR KAKUMBI ATAENDELEA KUWA MSARIFU WA SHULE HAKUNA HEAD MASTER ATAKAYE WEZA KUIOKOA SHULE YA MAKONGO KUFA KWA KUWA AFISA HUYU ANATUMIA FEDHA KUWAPUMBAZA WATU AMBAO WANGEMCHUKULIA HATUA. HIVYO HEADMASTER YEYOTE AKIENDA TOFAUTI NA YEYE ANAONDOLEWA. LAKINI AKIKUBALIANA NAYE ATAENDELEA KUDUMU KAMA ILIVYO KWA LT. MWANGASI, PIA TULIUSHAURI UONGOZI WA JESHI UCHUKUE HATUA LAKINI TUKAITWA WAONGO NA PIA NI CHADEMA. HAYA SASA JE MATATIZO YAFUATAYO YAMETOKA WAPI KAMA SI UBADHILIFU?
1. SHULE KUSHINDWA KUWALIPA GRATUITY WALIMU KADHAA(IDADI TUNAYO)
2. KUSHINDWA KULIPA MSHAHARA WA MWEZI WA KUMI NA MWEZI WA KUMI NA MOJA MPAKA
WALIPOSHINIKIZWA NA UONGOZI WA JESHI.
3. SHULE KUSHINDWA KULIPA MADENI MBALIMBALI WANAYODAIWA
4. KUWAKILISHA MAKATO PUNGUFU YA KODI KUTOKA KATIKA MISHAHARA YA WALIMU KWENDA TRA (.
5.SHULE KUSHINDWA KUWALIPA CONSO ASKARI NA MAAFISA KWA MIEZI KADHAA SASA.
MATATIZO YOTE HAYA YANAASHIRIA KIFO KISICHOEPUKIKA KWA SHULE YA MAKONGO PAMOJA NA KUWA MKUU WA SHULE ANAJISIFIA KUWA NI MTU WA MPANGO MKAKATI. KWA SASA NAMSHAURI AJIUZURU NA AWAACHIE WENGINE WAIOKOE SHULE HII KWANI AZINGATIE MSEMO UFUATAO:
"IF YOU HAVE DONE YOUR VERY BEST AND FAILED WHY CAN'T YOU JUST RESIGN".
vivyo hivyo naushauri uongozi wa jeshi kuchukua hatua za haraka katika kuokoa shule hii iwapo maofisa hawa wataendelea kung'ang'ania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…