K-Lyinn amfunga mdomo Zari kwa Pesa

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Miss Tanzania wa mwaka 2000 na mwanamuziki wa bongo fleva, Jackline Ntuyabaliwe aka K- Lyn hatimaye amekuwa mke mke rasmi wa mfanyabiashara maarufu na TAJIRI namba moja nchini, Reginald Mengi baada ya kufunga ndoa iliyohudhiriwa na mastaa mbali mbali wa nchini ufaransa na Tanzania.

Kama ilivyo ada kwa mke wa Rais kuitwa "FIRST LADY vivyo hivyo kwa mke wa tajiri jina hubadilika na kuwa "BOSSLADY ". Kutokana na hali hiyo kuanzia sasa K-Lyn anakuwa ndiye Rais wa ma Bosslady wote Afrika Mashariki kutokana na pesa aliyonayo mumewe mzee Reginald Mengi.

Awali kabla ya K-Lyn kutwaa wadhifa huo, mwanamuziki na mfanyabiashara toka Uganda ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki nguli wa bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hussein aka Zari aliaminika ndiye anayeongoza kwa pesa kwa mastaa Africa Mashariki. Kwa sasa hali imebadilika na taji hilo kuelekea kwa mwana mama mrembo K -Lyn.
 
Hivi mume akiwa tajiri na mke naye anakua tajiri automatically?Zari ni tajiri maana ana biashara zake na hata zile za mumewe ana share yake kwa ninavyosikia.Huyo K-Lyn achakarike naye apate share au biashara zake.Asijibweteke kisa kazaa na mzee Mengi.
 

mi na wewe ni timu mbili tofauti, lakini muda mwingine nakuelewa sana.
 

Muacheni bosslady mpya wa africa mashariki... ivi mke wa mengi yuko wapi jaman? Anavumilia yote haya? Pole yake
 
warumi mke wa Mengi sio mjinga kukaa kimya.Yeye bado ana share zake na mzee ana shida gani? Yule mama anajielewa, anajua anachokifanya.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu warumi mashabiki wote wa ndomo ni mashabiki wa kibibi Zari! Tarajia matusi kutoka kwa #team ndomo! Hawa jamaa hata ndomo akiwapanga foleni kuwa..............baang watakuwa wana-update status kwamba sasa ni zamu ya nani na gem ikoje! Kawashika wakashikika!
 
Last edited by a moderator:

Hahahaaa,wewe jamaa utani wa ngumi aisee.
Subiri waje utayakoga matusi hapa hadi ukome...lol
 
Last edited by a moderator:
Mpwa warumi hivi sasa inaelekea unaanza kuzeeka vibaya! Sasa kama hoja yako ndo hiyo, kwanini huyo Bosslady asiwe mke wa Mo Dewji? Au kwanini asiwe mke wa Rostam? Au kwanini asiwe mke wa Bakhresa?
 
Last edited by a moderator:
warumi mke wa Mengi sio mjinga kukaa kimya.Yeye bado ana share zake na mzee ana shida gani? Yule mama anajielewa, anajua anachokifanya.

Hata mengi nae sio mjinga, k lyn atakua na fungu lake zuri tu na mpacha wake, jaman watu wana bahati nyie sijawahi kuona, mungu ambariki kwa kweli
 
Last edited by a moderator:
Wewe ni mtu wa kupuuzwa na hili jukwaa umelivamia manake ungekuwa ni mwenyeji wa hili jukwaa ungegundua kwamba kuna mashabiki kibao wa Kiba ambao wana-show love kwa Zari!
 

Wameshakuwa mwili mmoja, mali zote zitakazopatikana kuanzia sasa ni za k -lyn na mengi achilia mali walizochuma na mke wake, hakika jack kabarikiwa kuliko wanawake wote africa mashariki, wakina mwafulan ndo mtulie muache umalaya maana mmezidi wenzenu hao mabilionea
 

Wameshakuwa mwili mmoja, mali zote zitakazopatikana kuanzia sasa ni za k -lyn na mengi achilia mali walizochuma na mke wake, hakika jack kabarikiwa kuliko wanawake wote africa mashariki, wakina mwafulan ndo mtulie muache umalaya maana mmezidi wenzenu hao mabilionea sasa ivi
 
Wewe ni mtu wa kupuuzwa na hili jukwaa umelivamia manake ungekuwa ni mwenyeji wa hili jukwaa ungegundua kwamba kuna mashabiki kibao wa Kiba ambao wana-show love kwa Zari!

chige wew ndomo akifa unaweza kuomba umsindikize aisee! Najua ushamalizana na KTMA
 
Last edited by a moderator:
Yeye ajidanganye kwa kuvaa vitu original kutoka kwa ma designer wakubwa asiangalie future ya mapacha wake.
Mzee akianguka ndipo atakapouona mziki wa wachagga.

Tena ukute ni mmachame aka palestina.. Itabidi afunge kibwebwe kuucheza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…