K/Mkuu Wizara ya Afya, awaasa wananchi kuacha kuzusha maneno kuwa hospitali zimejaa wagonjwa na kusababisha watu kuogopa kwenda kupata Huduma za Afya

K/Mkuu Wizara ya Afya, awaasa wananchi kuacha kuzusha maneno kuwa hospitali zimejaa wagonjwa na kusababisha watu kuogopa kwenda kupata Huduma za Afya

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
IMG_20210212_182750.jpg

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Mabula Mchembe amewaasa Wananchi kuacha kuzusha maneno ya kuwa hospitali zimejaa na kusababisha wagonjwa kutofika ili kupatiwa matibabu

Profesa Mabula amesema hayo leo FebruarI 12, 2021 mkoani Arusha.
 
Angemjibu yule Mbunge wa Jimbo la Mbulu ,aliyesema kuwa ,alienda Hospital na kukuta mitungi ya kupumulia umeisha yote/ inatumika
 
Wa kuwaamini hawa labda marehemu, mtu mzima na akili zako huwezi kuhangaika na watu waongo waongo kama hawa.
 
Hivi wale wagonjwa wa Chunya ambao serikali ilikanusha uwepo wao wananchi kule walisema je?

Vipi waraka wa yule Prof aliyeishia kuonywa?

Tumesikia wengine kufa kwa ajili ambazo hazikutokea kwenye maeneo tuliyopo!

Kwanini mnatudhania kuwa tu watoto wadogo?

Huu ugonjwa hautaondoka kwa kuukimbia. Bali kwa kuukabili.
 
Huyu jamaa ana kazi ya kukanusha na kupiga picha kweli watu wanataka taarifa za kisayansi yeye yupo busy wodini...
 
Hiyo picha tu aliyopiga inaonesha wodi imejaa na tena kuna mitungi ya gesi kusaidia upumuaji

Inasikitisha sana jinsi siasa ilivyochukua nafasi Tanzania
 
Naona mitungi pande zote,na katibu hana Barakoa, ili amridhishe bwana mkubwa.
Nashika nafasi hapa,Sisemi kitu leo
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hawa wote wanacheza na tune ya Boss wao mkuu. Yaani ukimsikiliza Mollel au yule Mama Gwajima, huruma na aibu unaona wewe.
 
Hiyo picha tu aliyopiga inaonesha wodi imejaa na tena kuna mitungi ya gesi kusaidia upumuaji

Inasikitisha sana jinsi siasa ilivyochukua nafasi Tanzania
Usisahau na wahudumu karibu wote humo ndan wamevaa barakoa maana wao ndio wako na wagonjwa 24hrs
 
Tatizo letu ni siasa tumeweka mbele wanaosema corona inauwa watu wanasukumwa na siasa na wanaosema hakuna corona nao ni siasa,ila likitokea jambo ambalo litakuwa muhimu kuliko haya mabishano yao basi utasikia wanasema corona imepungua.

Tumeona hivyo mwaka jana.
 
Back
Top Bottom