Aisay umenichekesha sheikh kachukua sh150,000 huyo ni sheikh au mnafiki tu.Rudia tena!!!! Diwani afumaniwa na mke wa sheikh, ilikuwa ni kama tarehe ya leo mwezi huu mwaka 2010
DIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tunduru amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mmoja wa masheikh mkoani hapa. Katika fumanizi hilo la aina yake, sheikh huyo alipigwa na butwaa baada ya kumshuhudia diwani huyo akiwa amejifunga kiunoni kitenge ambacho alimnunulia mkewe mara baada ya kubisha hodi.
Tukio hilo limetokea juzi saa nane usiku baada ya mume wa mke huyo kupata taarifa kutoka kwa majirani kuwa mkewe ameonekana katika nyumba ya diwani huyo (jina tunalo).
Hata hivyo, katika mahojiano na Mwananchi Jumapili, diwani huyo alikiri kutokea kwa fumanizi hilo lakini akadai kuwa ni njama zilizopangwa na washindani wake wa kisiasa ili kumchafua.
Baadhi ya watu waliodai kushuhudia tukio hilo walisema kwamba mikakati ya kumfumania ilipangwa na majirani baada ya kuona mke huyo wa sheikh ameingia ndani kwa diwani huyo.
Walidai diwani huyo ana tabia ya kula na wake za watu na hiyo imemjengea uhasama kwa watu wengi kiasi kwamba ilibidi watoe taarifa kwa sheikh huyo ili kumkomoa.
Mara baada ya shehe kupata taarifa hizo aliongozana na mwenyekiti wa kitongoji cha Raha leo, Mkwanda Mussa na Mwenyekiti wa kitongoji cha Kitani, Nyenje Madefu hadi nyumbani.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao, jopo hilo lilipofika kwenye nyumba walimokuwemo ndani na kubisha hodi, diwani huyo alifungua mlango akiwa amejifunga kitenge cha mke wa shehe huyo kiunoni na kuwataka waeleze shida waliyoijia.
Walisema diwani huyo alipigwa na butwa na kuonekana kuwa na kigugumizi baada ya jopo hilo kumueleza kuwa limefika kumtafuta mke wa shehe waliyehisi kuwa yumo ndani.
Kabla hajajibu lolote waliingia ndani na kumkuta mke wa sheikh akiwa amelala kitandani na ikawa ni ushahidi wa kumkamata diwani huyo hadi ofisi za kata ili kumhoji.
Baada ya mahojiano ya muda mrefu, inadaiwa kuwa diwani huyo alikiri kosa la kulala na mwanamke huyo na ikaamuliwa alipe Sh300,000 kama faini kwa sheikh.
Alifanikiwa kupata Sh150,000 na kuahidi kiwango kilichobaki atakilipa hara iwezekanavyo.
Baadhi ya wakazi wa kata anayoongoza diwani huyo, walidai kuwa amekuwa akitumia wadhifa alio nao kwa ajili ya kula na wake za watu.
Habari hii imeandikwa na Joyce Joliga, Songea
Na: Yasinta Ngonyani kl
Aisee
NN....huyo mle aliyeenda kufumania, kapata kilichompeleka...yeye alivoambiwa 'nisubiri hapo hapo nje nitakukuta' alifikiri nini? Yaani tuseme angetegemea mumewe atoke ndani kikondoo tu na kujisalimisha?
Nadhani hii ilm ya namna ya kuishi na wenza inahitajika sana kwa watani zetu....wapi The Boss?
Hapana mimi si sheikh mshikaji. mimi nikahuni huni tu kamtaani lakini niko speed kuelekea direction hizo siku za mbele.Wewe ni sheikh nini?
Haya hebu soma bandiko la Geka, bandiko namba 12.
Leo jioni tulikutana mahali marafiki wa3, ikatokea tunazungumzia watu kutoka nje ya ndoa, mwenzetu mmoja(ana mume na mtoto mmoja)akawa anatetea kuwa inasaidia kupunguza stress za ndani ya ndoa, mie nkamuuliza dini inaruhusu kucheat? Akasema hairuhusu, nkamwambia sasa huoni kama unatenda dhambi? Akanambia kwataarifa yako hakuna dhambi kubwa na ndogo, hivyo haoni tatizo kucheat... Nikamwambia sasa kwa nini umeolewa? Akanambia kuolewa kuna heshima yake... Labda mimi sijamwelewa... Hiyo heshima ya kuolewa wanayoisemaga sijajua ni ipi mpaka sasa.Nashindwa kuelewa mtu kama huyo ameoa ili iweje.
Kwahiyo kosa ni la mke?
Kwahiyo kosa ni la mke?
Kuna sehemu nimesema ivo.....?
Aisee
NN....huyo mke aliyeenda kufumania, kapata kilichompeleka...yeye alivoambiwa 'nisubiri hapo hapo nje nitakukuta' alifikiri nini?
Heshima wakati mtu anakukuruka nje ya ndoa?Leo jioni tulikutana mahali marafiki wa3, ikatokea tunazungumzia watu kutoka nje ya ndoa, mwenzetu mmoja(ana mume na mtoto mmoja)akawa anatetea kuwa inasaidia kupunguza stress za ndani ya ndoa, mie nkamuuliza dini inaruhusu kucheat? Akasema hairuhusu, nkamwambia sasa huoni kama unatenda dhambi? Akanambia kwataarifa yako hakuna dhambi kubwa na ndogo, hivyo haoni tatizo kucheat... Nikamwambia sasa kwa nini umeolewa? Akanambia kuolewa kuna heshima yake... Labda mimi sijamwelewa... Hiyo heshima ya kuolewa wanayoisemaga sijajua ni ipi mpaka sasa.
Binafsi siamini mwanamke YOYOTE!Naamini kuwa wanaume ni afadhali kuliko wanawake!
Wakati mwingine haya mambo yanashangaza sana,mtu anacheat halafu anatafuta namna kuhalalisha huo ujinga!
Sasa unapoolewa tabia ya mwenzi wako haitakufanya wewe ubadili mtizamo wako wa ndoa. Sikubaliani na kwamba mwenza kama ni cheater na mwenzie awe cheater kulipiza kisasi.
Unavumilia nini? Haina tofauti na ulivyosema huwezi kutolewa ngeu kwaajili ya mtu asiyekuheshimu. Kuvumilia ni aina nyingine ya ngeu.Kwa hiyo mwenza akiwa cheater cha muhimu na busara kufanya ni kuvumilia?
Aaa c umeona na wewe nacho kisema umekisapoti.Kama wewe ni sheikh na mke wako hafanyi basi shukuru mungu...ila bado sio kigezo cha kukufanya wewe uamini kuwa wake wote wa masheikh hawafanyi. Kucheat ni tabia ya mtu haijalishi kaolewa na sheikh au mchungaji, na ukumbuke tabia haina dawa.