Kababu za kuku na sosi ya nyanya

Kababu za kuku na sosi ya nyanya

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Kidari cha kuku 1 kilo

Thomu, tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu

Kitunguu kilichokatwa vipande vidogo 1

Pilipili mbichi 1

Pilipili manga 1 kijiko cha chai

Bizari upendayo 1 kijiko cha chai

Siki 1 kijiko cha supu

Mayai 4 5

Mafuta Kiasi ya kukaangia

Sosi

Mafuta 3 vijiko vya supu

Vitunguu vilivyokatwa (chopped) 2

Nyanya zilizosagwa 3

Nyanya ya kopo 1

Pilipili manga 1 kijiko cha chai

Chumvi kiasi

Kotmiri iliyokatwa (chopped)

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kababu

1. Chemsha kidari cha kuku kwa siki, thomu, kitunguu kilichosagwa, pilipili mbichi bizari zote na kufunika kipikike bila ya maji hadi kikauke.

2. Tia katika mashine ya kusagia (blender) na usage bila ya kuta maji, kitasagika wenyewe.

3. Tia katika bakuli na upige mayai na kuchanganya. Mchanganyiko uwe unaweza kufanya viduara vya kababu. Kama umekuwa laini ongeza mayai.

4. Katika karai tia mafuta kiasi kidogo tu ya kuweza kugeuza geuza kababu zipikike.

5. Epua na weka katika sufuria.

Sosi

1. Kaanga vitunguu kisha tia nyanya, nyanya ya kopo, pilipili manga, chumvi na endelea kukaanga iwe sosi.

2. Tia kotmiri, kisha mwagia katika sufuria iliyokuwemo kababu.

3. Pika katika moto mdogo kababu zitokote kidogo hadi ziwive vizuri.

4. Epua na pakua katika bakuli, mwagia kotmiri kidogo.

Tayari kwa kuliwa.
1384523363824.jpg
 
Kidari cha kuku 1 kilo

Thomu, tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu

Kitunguu kilichokatwa vipande vidogo 1

Pilipili mbichi 1

Pilipili manga 1 kijiko cha chai

Bizari upendayo 1 kijiko cha chai

Siki 1 kijiko cha supu

Mayai 4 – 5

Mafuta Kiasi ya kukaangia

Sosi

Mafuta 3 vijiko vya supu

Vitunguu vilivyokatwa (chopped) 2

Nyanya zilizosagwa 3

Nyanya ya kopo 1

Pilipili manga 1 kijiko cha chai

Chumvi kiasi

Kotmiri iliyokatwa (chopped)

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kababu

1. Chemsha kidari cha kuku kwa siki, thomu, kitunguu kilichosagwa, pilipili mbichi bizari zote na kufunika kipikike bila ya maji hadi kikauke.

2. Tia katika mashine ya kusagia (blender) na usage bila ya kuta maji, kitasagika wenyewe.

3. Tia katika bakuli na upige mayai na kuchanganya. Mchanganyiko uwe unaweza kufanya viduara vya kababu. Kama umekuwa laini ongeza mayai.

4. Katika karai tia mafuta kiasi kidogo tu ya kuweza kugeuza geuza kababu zipikike.

5. Epua na weka katika sufuria.

Sosi

1. Kaanga vitunguu kisha tia nyanya, nyanya ya kopo, pilipili manga, chumvi na endelea kukaanga iwe sosi.

2. Tia kotmiri, kisha mwagia katika sufuria iliyokuwemo kababu.

3. Pika katika moto mdogo kababu zitokote kidogo hadi ziwive vizuri.

4. Epua na pakua katika bakuli, mwagia kotmiri kidogo.

Tayari kwa kuliwa.
YaaSalaam Ya salaam lamm lam.... Bint inNass acha bwana afaidi...siye turambe vidole tu!! nice Cook and delesiesoo!!
 
Sasa apo habibty naona utanifilisi akiba yangu. Mana mi na kula hatuna khiyana, nkiona mambo km hayo wanitamanisha ujue.

Lkn kesho lile pilau la nafaka, mchana.

Na andazi jioni.

In sha Allah.
Maasalam
 
Sasa apo habibty naona utanifilisi akiba yangu. Mana mi na kula hatuna khiyana, nkiona mambo km hayo wanitamanisha ujue.

Lkn kesho lile pilau la nafaka, mchana.

Na andazi jioni.

In sha Allah.
Maasalam

Hahaaha sikufilisi habibty lol.....
Basi kesho naja pande za huko lol...
 
Back
Top Bottom