kabambikiwa mtoto

kabambikiwa mtoto

deborahk

New Member
Joined
Jun 26, 2012
Posts
3
Reaction score
0
hivi kama ikitokea ukisingiziwa mtoto na mwanamke halafu ukamlea, kumsomesha na kumpa kila kitu kwa kujua huyu ni mwanao, ikaja siku mtoto amekuwa yuko chuo kikuu anajitokeza mtu ambae ni baba ake biological (kwa ushahidi wa DNA) na anamtaka mwanae...je hamna sheria yoyote inayokulinda wewe uliemlea au hamna sheria yoyote inayomhukumu yule mama aliekusingizia...kiufupi nini kitakulinda wewe au hukumu gani itatolewa kwa yule mama aliekusingizia...na je gharama zako zinaweza kurudishwa, zile za shule na chakula na mengineyo?
 
Mtoto kwenyewe kama ulimlea kwa mapenzi na ukampa Elimu,basi hata akija baba yake mzazi haijalishi tena ndio atakupenda zaidi,na unapolea mtoto awe wako au wamkeo usitegemea malipo sababu hujui yupi atakusaidia.
 
Ipo sheria bana, uko protected. Kama alivyosema huyo kaka hapo juu kama umelea kwa mapenzi huyo mtoto anamtakia nini baba jina.

Ili iweje?
 
Hawezi kumchukua, hata kwa jina... Kisheria atakuwa wa kwako, na atatumia majina yako... Unless uamue kumgawa
 
na huyo mtoto akimkimbilia huyo 'baba' jina, basi atakuwa na walakini
 
kama yamekukuta tulia tu ndugu yangu..kama huyo mtoto ulimlea kwa mapenzi basi usohofu ni wako tu hata iweje..
 
Mimi ni mhanga nampenda na kumthamini baba yangu aliyenilea na kunifikisha hapa nilipo. huyo wa jina ye aendelee na jina lake huko mbele ya safari.
 
hivi kama ikitokea ukisingiziwa mtoto na mwanamke halafu ukamlea, kumsomesha na kumpa kila kitu kwa kujua huyu ni mwanao, ikaja siku mtoto amekuwa yuko chuo kikuu anajitokeza mtu ambae ni baba ake biological (kwa ushahidi wa DNA) na anamtaka mwanae...je hamna sheria yoyote inayokulinda wewe uliemlea au hamna sheria yoyote inayomhukumu yule mama aliekusingizia...kiufupi nini kitakulinda wewe au hukumu gani itatolewa kwa yule mama aliekusingizia...na je gharama zako zinaweza kurudishwa, zile za shule na chakula na mengineyo?

Sijui sheria hasa inasemaje kuhusu jambo hilo lakini kuna haja gani ya kudai yote hayo? Kwani hata watoto wetu wenyewe wote huchukuwa jitihada ya kulipa fadhila za wazee wao, au wanapokufa mapema? Ni jukumu la mtoto kukuelewa wewe ni nani kwake na kwa jinsi unavyosema wewe ndio Baba kwake na wala sie yule anaejitokeza!
 
Sina uhakika kama mtu wa above 18 huwa na yeye anachukuliwa custody kwa sababu tayari ni mtu mzima.
Huyo baba yake wa DNA anataka kumpeleka wapi? Kwani huyo mtoto si ndo anafanya kazi na ana maisha yake kama sisi tulivyo? Custody ya nn sasa?
Yeye hapo atabe 'acknowledged kama baba wa DNA na huyo aliyemlea atajulikana kama baba halisi na mtoto ataendelea kujitegemea na maisha yanaendelea...
 
kwanza kabisa kwa teknolojia ya sasa, mwanaume hupaswi kukubali kubambikiziwa mtoto. mwanamke akidai mtoto ni wako nenda kwa wakili/ustawi wa jamii uombe vipimo vya DNA ukishathibitisha kuwa mtoto ni wako, ndipo uanze kumtunza

kwa suala lako kwanza huyo mwanamke uliyenaye ana matatizo ya akili, kwani endapo alijua mtoto sio wako kwanini alikuingiza katika gharama za kumtunza na kumsomesha au kwann hakukueleza mapema au kwann hakukaa kimya. huyo mwanamke anaonekana sio mwaminifu. kitu kikubwa unachoweza kufanya ni kudai fidia ambayo itazingatia maeneo yafuatayo-
1. matunzo ya mtoto tangu azaliwe( chakula, mavazi, nguo na malazi);
2. gharama za masomo yake hadi leo(chekechea-chuo kikuu),
3.matibabu;
4. fidia ya jumla;
5. fidia ya adhabu;
 
Back
Top Bottom