INAUZWA Kabati portable

Kabati la hovyo sana hilo.
Sina hamu nayo kabisa hayo ma wardrobe.
 
Hilo kabati ukitaka ukae nalo kwa muda kidogo usilijaze nguo, ukijaza linashuka lote😅😅...Atleast yale yenye viungio vya mbao, vile vinabana haviachii achii hovyo.

Nilinunua mwaka 2016 Mutukula nimekaa nalo almost mwaka ndo likaanza kulegea.
 
Kabati zuri kwa mwonekano lakini ni 'delicate' sana. Halihitaji kuguswaguswa, la sivyo litasambaratika ndani ya siku mbili. Niliwahi kulinunua kwa ajili ya kuhifadhia nguo za mapacha wangu, walivyo watundu sasa, kabati lilidumu mwezi mmoja tu.
 
Cha ajabu sasa mi kabla sijanunua niliwahi kuliona kwa mshkaji anatumia, tena alidumu nalo tu na alikuwa akihama chumba anapangua na kulipanga upya fresh tu.

Afadhali umenipa moyo! Ngoja Namie nikanunue Kariakoo maana sina laki tatu A kuchongesha kabati la mbao
 
Kiuhalisia hilo sio kabati la kuweka chumbani, ni kama urembo wa kichina wenye mfanano wa kabati, ni zuri kwa muda mfupi kupendezesha chumba, kupigia picha na kuigizia sinema lakini sio kuliweka ndani na kulitumia kama kabati la kudumu katika mazingira ya kibongo kibongo. Liko delicate mnoo.
 
Wakuu, nataka nikalinunue Kariakoo. Kesho naenda. Ushauri?
 
Reactions: 1gb
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…