Messi angemalizia tu huo mwaka mmoja. Nakumbuka hata Mbwana Samatta aliwahi kususa kucheza Simba karibia nusu msimu kisha tu ahadi aliyopewa ya Baloon (Toyota Chasser au Mark 2) hakua ametimiziwa.
Kipaji alikua nacho ila Mark 2 ilimfanya asicheze mpira, mark 2 ambayo leo akiamua kuuza assets zake zote anaweza kuzinunua hata 20.
Wakubwa walimshauri arudi uwanjani, hilo la mark 2 litatulika tu, leo ni mchezaji mwenye kipato kikubwa tu pengine kuliko mchezaji yeyote wa kizazi hiki wa mpira wa miguu. Yote ni sababu aligundua kuendelea kususa kunamuharibia yeye.