Kabla hujaagiza gari, pitia hapa kujua gharama kamili za ushuru na bandarini

Sawa mkuu nimekuelewa but hiyo calculator si unajaza full description ya hilo gari, sasa iweje bei ibadilke?
kuna gari zimekuwa modified huko Japs kuna Altezaa cif' zinafika Usd 15,000/= nani za mwaka 2002 uko so ni wazi kodi yako itakua tofauti na huyu mwenye Teza wa cif' ya usd 2,000/=
 
Mimi huwa natumia calculator kama base ya ku bargain, maana inanipa makadirio ya bei ya gari husika. Nikiona bei ya gari ni kubwa zaidi ya CIF ya TRA huwa nina assume gari iko over priced. Hivyo nita bargain. Bahati mbaya sana ikiwa underpriced kulingana na calculator ya TRA, wao watatumia CIF ya calculator yao.

Hapa kuna mfano wa magari mawili yanayofanana kila kitu yanayouzwa na watu wawili tofauti (sijasoma miongozo ya TRA mahali popote, ila ni uzoefu niliopata, kama kuna watu wana miongozo wanaweza itoa).

Mfano wa gari ya kwanza
Seller CIF (ambayo itakuja kwenye bill of lading): USD 12,000
TRA CIF (Ipo kwenye calculator): USD 10,000
Status kwa mujibu wa TRA: Overpriced
CIF ipi itatumika kukadiria kodi: ya Seller ambayo ipo kwenye bill of lading

Mfano wa pili gari ileile muuzaji tofauti
Seller CIF (ambayo itakuja kwenye bill of lading): USD 7,000
TRA CIF (Ipo kwenye calculator): USD 10,000
Status kwa mujibu wa TRA: Underpriced
CIF ipi itatumika kukadiria kodi: ya TRA iliyopo kwenye calculator yao kulingana na exchange rate ya dollar siku husika.

Tukumbuke calculator inatoa makadirio, haikupi gharama halisi. Naona calculator inafanya vizuri sana, isipokuwa tunateswa na ukubwa wa ushuru. Halafu kuna magari mengi hayapo kwenye calculator ya TRA, na hata ukijaza fomu kuwataarifu, hawayaongezi.

Sawa mkuu nimekuelewa but hiyo calculator si unajaza full description ya hilo gari, sasa iweje bei ibadilke?
 
Hivi Bill of Lading si hua inatumwa kwa couriee i.e DHL etc au inakuja na meli
 
Habari za muda huu,

Pamekuwa na thread nyingi sana za watu kuomba ushauri/ elimu hasa kwenye suala zima la budget halisi/ kamili ambayo mtu anahitaji kuwa nayo kuweza kumiliki gari...

Jamani mbona mnakuwa wachoyo hata kwa elimu ya bure. Au unataka na wewe upate kitu kidogo kwa kazi ya dakika mbili. Ukitaka kujuwa bei halisia ya gari unayotaka kuagiza tumia used vehicle valuation tool ya TRA. iHii tool inapatika kwenye link hii: Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System Hakikisha una taarifa zote muhimu za gari zinazotakiwa. Usisahau kuongeza bei ya usafirishaji wa gari ambayo haipo.
 

Mkuu naomba kueleweshwa, hivi Bill of Lading hua inataja CIF ya mzigo (gari) au ni invoice peke yake. Na wanachotumia TRA kuverify CIF ni B/L au invoice?
 
Bill of Lading inaweza isiweke thamani ya gari, Invoice ndio inaonyesha thamani ya gari.

Bill of lading hii inaonyesha Nani ni mmliki wa gari na hii ni kama risiti ya kuchukulia mzigo wako melini na kufanya clearing.
 
Bill of Lading inaweza isiweke thamani ya gari, Invoice ndio inaonyesha thamani ya gari.

Bill of lading hii inaonyesha Nani ni mmliki wa gari na hii ni kama risiti ya kuchukulia mzigo wako melini na kufanya clearing.
Mkuu, msaada kwenye tuta kidgo kuhus toyota alphard.
 

Namba yako MAGARI 7 haiko WhatsApp.
 
Calculator ya tra majanga

Utaniambiaje cc 2500 and above ....

Nitaendelea..!
 
Halafu bado mtu anajiuliza kwanini wanawake wanavutiwa na wanaume wenye magari hata kama ni Malaya. Jibu lipo kwenye uthubutu wa kulipia gharama kama hizi
 
Mkuu nakupongeza sana kwa elimu unayoendelea kutoa. Nna maswali mawili:

1. Nimeagiza kagari kadogo Mazda Verisa ya 2006 cc 1500 bei mpaka kanafika dar ni kama USD 2000. Nimecheki kodi TRA ni kama 5.3m. Cha ajabu jamaa wananiambia niandae 1.4m ya clearance, sasa kufuatana na maelezo yako hapa nimebaki nashangaa. Hiyo hela yote itakua ni ya nini?

2. Je, kama nimeshaagiza gari na nimeshachagua agent wa clearing, naweza kumbadilisha?

Asante.
 
Inspection-353000
Agent minimum-200,000
Port charge-
Plate number-
Bima-
Corridor levy-
nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…